Rais Samia aipa Zambia ardhi hekari 20 katika bandari kavu Kwala mkoa wa Pwani

Zambia nao watupatie bure hekta 20 eneo la Copper belt tuna shida nalo!
Wazambia waamesema njooni muwekeze bure, mnachotaka, wewe unasema eka 20 walizotengewa kwa faida yetu?

Hivi unaelewa mwendazake alivyowakorofisha wafanyabiashara wengi sana wakakimbilia kuanzisha mabiashara Zambia? Hususan wale ma transporter wakubwa. Wamepewa ma eka na ma eka bure wafanye yadi za magari yao.
 
Huyu mama hakuomba kura na hana uchungu na wapiga kura . Atagawa kila kitu bure mwisho wa siku tutakuja kujuta na tukiamini muungano ulitupatia kiongozi kupitia kile kitabu.
Pia huyu mama kichwa chake hapendi kuingiza mambo mengi ili nchi iende atatoa kila kilichopo mbele yake.

Sasa chuo kikuu cha Zambia kinajiandaa tena kumpatia Phd.
 
Nasikia watampatia tena Phd!!
Hadi atoke madarakani atapewa phd 40
 
 

Attachments

  • D0FC9EA1-F5A1-40B9-BB65-FAA64D27CB85.jpeg
    98.5 KB · Views: 1
Uwezo wa machawa kutafakari na kutumia akili na mama ni zero na kila upande tutapigwa.

Akija kuondoka madarakani tutskuwa tumebaki na mashati na kofia za ccm tu , mengine atakuwa ameyatoa yote
 
Kazi ya Mungu haina makosa.

Kwanini haukuwa wewe mgombea mwenza 2020?
 
Bandari ya Dar ameipa DP world, Zambia ameipa eneo la bandari kavu.

Kwa mahesabu rahisi Samia ameipatia Zambia DP world!!
 
Taratibu mtaanza kuelewa falsafa ya Kiislam ya "Reconciliation" maana yake nini.

Mlifikiri inafanya kazi kwa kina Mbowe tu?
 
Bahati mbaya baadhi yenu hamjui hali au changamoto za biashara duniani. Kwani hizo hekta zilizotolewa kwa Zambia si ni kwa manufaa ya Tanzania pia ? Tafakari.
hawatafakari kuwa hiyo ni long term investment na ni kama kivitio kwa Zambia kutumia bandari ya Dar.
 
Maoni yangu

Hadi tukifika mwaka 2030 Tanganyika itabidi kuomba uhuru upya ili tujikomboe kwa sababu nchi nzima itakuwa mikononi mwa wachache.
Kwanini asingewakodisha? Wallah Kuna SIKU ikulu itakua genge la wahuni
 
Kwani zanzibar kuna njia ya kunyooshea zambia? Chadema akili zao siku zote ni mbofu mbofu, hawajui hata "extremely firmly lobbying" majinga kweli kweli. What 20 acre?.
 
Changamoto za biashara duniani zinahusu kugawa maeneo ya nchi yako kwa wengine?
Hakuna njia nyingine za kukabiriana na changamoto hizo?
Nadhani ni njia ya ushindani kibiashara ili tum'contain Zambia asituhame kuelekea bandari mpya ya Angola inayojengwa.
So watz tusiwe pingapinga ardhi ya Tanzania ambayo haina matumizi bado kubwa sana. Pia tuwe tunatazama mambo kwa maslahi mapana ya taifa.
Tuache roho za kimaskini.
 
Simuelewi huyu rais. Nani kampa kibao cha kugawa ardhi ya watanzania kwa Zambia?
Amewapa wazambia ekari ishirini kwa ajili ya storage ya mizigo yao kama ilivyo Malawi cargo, wewe nenda morogoro ukachukuwe ekari 100 ukaanzishe kilimo, wewe nenda ukachukue ekari 100 ulime, tunakupendelea mara tano zaidi ukalime uisaidie familia yako nyau kweli.
 
Watanzania bwana sijui tukoje, hebu fatilieni huko bandarini eneo la MUKUBA ni la nchi gani kwa miaka yote na huu umoja wa TAZARA na TAZAMA uliasisiwa lini, naona kuna nongwa na chuki kubwa sana humu inasambazwa.
Hiyo bandari ya kwala ni moja ya mkakati wa kupunguza msongamano mjini na hiyo sehemu ya MUKUBA hapo bandarini ni mpango huo hou wa dry port hapo kwala.

Humu kuna watu nimeamini ata bandarini hawapajui nanwanapinga vitu kwa kufuata nani anapinga.

Nadhani wale wanasiasa wenye biashara za usafirishaji wanajua huu mkakati ni kwa ajili ya nini tena hao hao wa upinzani.
 
Watanzania wengi kitu biashara na lobbying zake ni akili ambazo hawana kabisa nani mazuzu mzungu wa reli, watu wamejazwa chuki za kijinga kabisa na kipumbavu.
 
Watanzania wengi kitu biashara na lobbying zake ni akili ambazo hawana kabisa nani mazuzu mzungu wa reli, watu wamejazwa chuki za kijinga kabisa na kipumbavu.
Mkuu wengi wanatazama mambo kihisia hasa Uzi kama huu,comment ya kwanza huwa INA athari sana kwenye mtiririko mzima wa mjadala. Watanzania tunapenda lawama sana.
 
Be fair,unafahamu Zambia anapitisha mizigo kiasi gani pale bandarini, vipi unajua kuna bandari nyingine inajengwa huko Angola na mlengwa mkuu ni Zambia na Congo? Katika biashara unajisikia vipi mteja wako akikuhama?
Tuwe logical, bandari tusipoifanyia biashara,hata pato letu LA kitaifa litashuka.....bandari ni ya watanzania lakini tokea huu mwaka uanze ni asilimia ngapi ya watanzania wamepitishia mizigo yao pale?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…