Rais Samia aiteka mijadala ya kisiasa mitaani, wananchi waupongeza uongozi wake

Rais Samia aiteka mijadala ya kisiasa mitaani, wananchi waupongeza uongozi wake

Ndugu zangu watanzania,

Rais Samia Ameendelea Kuiteka mijadala ya kisiasa Mitaani,kila mahali Ni Rais Samia,Ni Rais Samia juu ya uchapa kazi wake ulio tukuka,Ni Rais Samia juu ya kuimarisha demokrasia,Ni Rais Samia juu ya kuendesha na kuongoza maridhiano,Ni Rais Samia juu ya kulituliza Taifa letu,Ni Rais samia juu ya kukuza uchumi wetu,Ni Rais samia juu ya kuimarisha mifumo ya haki na utawala Bora,Ni Rais Samia juu ya kuhubiri na kutenda haki,Ni Rais Samia juu ya Uzalendo wake kwa Taifa letu,Ni Rais Samia juu ya mapinduzi ya kilimo,Ni Rais Samia juu ya kuliheshimisha Taifa letu,Ni Rais Samia juu ya usikivu wake,Ni Rais Samia juu ya Ukarimu na Upendo wake,Ni Rais Samia juu ya mazingira Bora ya kibiashara na kiuwekezaji,

Ni Rais Samia juu ya ushupavu na umadhubuti wake,Ni Rais Samia juu ya ujasiri na misimamo yake,Ni Rais Samia juu ya Dira na muelekeo wake ulio Bora kwa Taifa letu,Ni Rais Samia juu ya miradi mikubwa ya kimkakati Ni Rais Samia juu ya utolewaji wa huduma Bora za kiafya na kielimu,Ni Rais Samia juu ya uchumi jumuishi na kugusa kila mtu,Ni Rais Samia juu Ya Tanzania iliyo Bora na yenye kutoa matumaini yaliyo hai.

Rais Samia Mama yetu mpendwa ameamsha mioyo ya Uzalendo kwa Taifa letu,Rais Samia anajadiliwa na kupongezwa kwa kulileta Taifa pamoja na kuliweka katika vifua vya watanzania wazalendo,Rais Samia anatetewa na kupiganiwa na watanzania wengi,kila eneo ana wasemaje wa kumsemea mambo aliyo yafanya na kuyatekeleza kwa hiyari kabisa bila malipo.

Watanzania wanaonesha kuridhishwa na utendaji kazi wa mh Rais wetu mpendwa mama Samia,wanaonesha kukubaliana na hatua mbalimbali anazozifanya katika kuimarisha na kuupa Afya uchumi wetu,wana mpongeza kwa namna alivyoongeza makusanyo ya mapato mpaka kufikia Trioni mbili kwa Mwezi pasipo mavurumai na uhasama na wafanyabiashara.

Kila mmoja Anayo amani katika biashara yake na shughuli yake ya kiuchumi,kila mmoja ana matumaini na kesho yake iliyo Bora.,hakuna Mwenye wasiwasi juu ya biashara yake kuvamiwa au kufirisiwa kiuonevu,Hakuna kutunishiana misuli,Ni majadiliano na kuelimishana,Hakuna kuviziana Wala visasi,hakuna kukomoana Wala kunyanyasana. Rais Samia Ni kiongozi aliyeinuliwa na kupewa baraka zote kwa ajili ya kulivusha Taifa letu kuelekea Kanaan nchi ya Ahadi yenye maziwa na Asali.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627

Mtaani watu wanajadili simba na Yanga, hayo mengine ni uchafu kwao.
 
Nilimwambia mwashambwa Lucas alete CV yake hapa ili tujipime tunajadili na mtu WA Aina gani! Hilo alilikimbia

Mjadala mkubwa kuhusu Rais mitaani.
-Kupanda kwa gaharama za maisha kiasi watu kushindwa kumudu mfumuko mkubwa wa Bei.
-Uduni wa huduma za afya hebu tuzama tu yaliyotokea Huko uyui ni reflection ya maeneo mengi nchini
-Gharama za mafuta zilizopaisha kila Aina ya huduma!
-Matabaka katika elimu (state schools, community schools) na elimu duni isiyomsaidia Mwananchi kuweza kukabiliana na changamoto za maisha, elimu Bure ambayo ni Bure kwa kwa kuwa ni Bure!
-Kukua haraka na kuongezeka kwa matabaka ya walio nacho na wasiokua nacho! (Hasa wanasiasa na wafanyabishara) huku kundi la wakulima na wafanyakazi likiwa katika dimbwi la maskini.

-UKOSEFU WA AJIRA BADO NI TATIZO SUGU na nchi imekua ya wachuuzi (machinga badala ya wazalishaji)
--Hakuna sectorial linkage Kati ya kilimo na viwanda Ili kuongeza wigo wa Ajira na mnyoro wa thamani
-umeme usiokuwa wa hakika kuanzia mijini mpaka vijijini
-Huduma za maji sio za uhakika mmebakia kusifu mega projects Ila kufikia watumiaji ni Siku mradi unazinduliwa.
Mambo ni mengi tukiyataja hayaishi!
Juzi nimesikia huko morogoro upatikanaji wa mbolea ni kupitia usajili kwa mitandao ya simu! (Eneo husika linalalamikiwa kufikiwa na network, vipi kuhusu kupanda kwa gharama za mawasiliano? )
-matumizi mabaya ya fedha za umma kama serikali inavyojitapa kutangaza watu walitumia vibaya fedha za umma hatuoni hatua zozote za kisheria zikichukuliwa dhidi ya wahusika Ila tunaona wakihamishwa vituo vya Kazi!
Mwashambwa uandishi WAKO ni kama hii nchi ni Canada au Nchi iliyoendelea kupita nchi yoyote duniani! Kila kitu Kiko okay wakati Kuna watu wanajifungulia majumbani na wanafunzi wanakaa nchini!
Nakujibu hoja zote mkuu wangu na rafiki yangu. Kuhusu suala la Ajira kwa vijana,mh Rais alipoapishwa kuwa Rais wetu alianza kutoa ajira kwa secta karibu zote zikiongozwa na secta ya Elimu na Afya zinazofikia elfu 42, lakini pia mh Rais kwa kutambua kuwa serikali haiwezi kuajiri wahitimu wote alifanya jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa secta binafsi Ina imarika na kustawi ili iweze kutoa fursa za ajira kwa vijana, akafanya kazi kubwa ya kuvutia wawekezaji ili wawekeze nchini na hivyo kuongeza wigo wa ajira kwa vijana pamoja na kuongeza mapato ya kikodi.

Pia kupitia halmashauri mikopo imeendelea kutolewa kwa vijana kupitia vikundi vyao jambo ambalo limewasaidia vijana kujiajiri na kukuza mitaji yao na kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.

Suala la Afya,mh Rais amefanya kazinkubwa ya kuboresha huduma za Afya hapa nchini kwa kuhakikisha vifaa Tiba ,madawa na wataalamu wa Afya wanakuwepo kuanzia ngazi ya zahanati,vituo vya Afya,hospitali za wilaya,mkoa,rufaa,Kanda na Hadi Taifa,Tumeona ujenzi wa vituo vya Afya kila Kona ya nchi ikiwepo vituo 234 ambavyo vilijengwa miez michache iliyopita, huduma za kibingwa kwa Sasa zinapatikana hapa hapa nchini na kufanya watu kuzipta hapa pasipo kwenda nchi za nje.

Suala la mfumuko wa Bei,suala Hili lilipiganwa kihodari na kikomandoo na mh Rais wetu Jasiri na shupavu,mfano katika mafuta mh Rais alitoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi wakati katika kilimo hasa mbolea alitoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini Hali iliyo pelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu,yote hii Ni katika kumpunguzia maumivu mwananchi ,lakini pia bajeti ya kilimo imeongezeka kutoka billioni Mia mbili na point Hadi kufikia billioni Mia Tisa na point na Ikumbukwe kuwa bidhàa hizo hazikupandishwa Bei na serikali yetu Bali uliotokana na mfumuko wa Bei katika soko la Dunia hasa baada ya Vita ya ukrein.

Suala la maji,hapa pia miradi mbalimbali imeendelea kujengwa kila Kona ya nchi yetu Hali ambayo imesaidia upatikanaji wa maji kwa watanzania, na Ikumbukwe kuwa Mahitaji ya maji yanaongezeka kila Siku kutokana na idadi ya watu kuongezeka kila Siku na kila mwaka.

Matabaka katika Elimu,hili Ni upotoshaji wa makusudi imeifanya,kwa sababu kwa Sasa Elimu na mazingira ya Elimu yameboreshwa vizuri Sana ndio maana u aona hata matokeo ya mwaka Jana yalionyesha shule za serikali kwa matokeo ya kidato Cha nne na sita yalionyesha shule za serikali zikiwa miongoni mwa shule zilizofanya vizuri na kuwa na ufaulu mzuri,hata hivyo juhudi bado zinaendelea katika kuboresha secta hii,kwa kuboresha maslahi ya walimu,vitendea kazi vya kisasa kupongezwa,kuhakikisha maabara na vifaa vyake vinakuwepo kwa masomo ya sayansi ili kurahisisha usomaji wa masomo ya sayansi.
 
Mtaani watu wanajadili simba na Yanga, hayo mengine ni uchafu kwao.
Rais Samia kwa Sasa Ni Zaid ya Simba na yanga na Ni zaidi ya habari za feisali salumu na sakata lake la kwenda Azam fc,ElRais Samia Ndio habari ya mjini kwa sasa
 
Rais Samia ana nafasi kubwa mno ya kung'aa zaidi na zaidi kama atachanga karata zake vizuri sababu mtangulizi wake alikuwa kivuruge.
 
Mkuu unatafuta udc? Ameiteka mijadsla ipi labda, watu wanalia maisha magumu wewe unatuletea mapambio hapa. Umekula maharage ya wapi wewe
Angalia majibu yangu hapo chini nimetoa majibu kwa kina yanayojibu swali lako
 
Siku anaapishwa tu tulijua anaweza kuchukua marks za bure nyingi mno !! nafikiri na yeye anajua anachokifanya ni mdogo mdogo anawateka wananchi wa vicheko
Rais Samia kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuijenga nchi hii ndani ya muda mfupi hakika ndio sababu ya Kuendelea kuvuma Kama upepo masikioni na midomoni mwa watanzania,kila secta Kuna Alama za mh Rais,kila mahali amepeleka fedha za kutosha,miradi imejengwa kila mahali,huduma zimesogezwa karibu ya mwananchi
 
Rais Samia kwa Sasa Ni Zaid ya Simba na yanga na Ni zaidi ya habari za feisali salumu na sakata lake la kwenda Azam fc,ElRais Samia Ndio habari ya mjini kwa sasa

Unadhani kwakuwa unalipwa kupiga propaganda ndio utabadilisha ukweli?
 
Unadhani kwakuwa unalipwa kupiga propaganda ndio utabadilisha ukweli?
Tindo ndugu yangu Mimi silipwi na yeyote yule hata Mia Wala kuchangiwa hata hela ya vocha,Ni uzalendo wangu na kuridhishwa na uchapa kazi wa mh Rais Ndio unaonifanya niandike Yale nayoyaona na kuyasikia kutoka mitaani juu ya sifa kubwa anazopewa mh Rais
 
Tindo ndugu yangu Mimi silipwi na yeyote yule hata Mia Wala kuchangiwa hata hela ya vocha,Ni uzalendo wangu na kuridhishwa na uchapa kazi wa mh Rais Ndio unaonifanya niandike Yale nayoyaona na kuyasikia kutoka mitaani juu ya sifa kubwa anazopewa mh Rais

Kujipendekeza kwa rais ndio uzalendo? Mtaa upi huo wanamjadili rais wakati watu wameipuuza siasa baada ya kuingizwa mambo ya kishenzi?
 
Back
Top Bottom