Rais Samia aiteka mijadala ya kisiasa mitaani, wananchi waupongeza uongozi wake


Mtaani watu wanajadili simba na Yanga, hayo mengine ni uchafu kwao.
 
Nakujibu hoja zote mkuu wangu na rafiki yangu. Kuhusu suala la Ajira kwa vijana,mh Rais alipoapishwa kuwa Rais wetu alianza kutoa ajira kwa secta karibu zote zikiongozwa na secta ya Elimu na Afya zinazofikia elfu 42, lakini pia mh Rais kwa kutambua kuwa serikali haiwezi kuajiri wahitimu wote alifanya jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa secta binafsi Ina imarika na kustawi ili iweze kutoa fursa za ajira kwa vijana, akafanya kazi kubwa ya kuvutia wawekezaji ili wawekeze nchini na hivyo kuongeza wigo wa ajira kwa vijana pamoja na kuongeza mapato ya kikodi.

Pia kupitia halmashauri mikopo imeendelea kutolewa kwa vijana kupitia vikundi vyao jambo ambalo limewasaidia vijana kujiajiri na kukuza mitaji yao na kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.

Suala la Afya,mh Rais amefanya kazinkubwa ya kuboresha huduma za Afya hapa nchini kwa kuhakikisha vifaa Tiba ,madawa na wataalamu wa Afya wanakuwepo kuanzia ngazi ya zahanati,vituo vya Afya,hospitali za wilaya,mkoa,rufaa,Kanda na Hadi Taifa,Tumeona ujenzi wa vituo vya Afya kila Kona ya nchi ikiwepo vituo 234 ambavyo vilijengwa miez michache iliyopita, huduma za kibingwa kwa Sasa zinapatikana hapa hapa nchini na kufanya watu kuzipta hapa pasipo kwenda nchi za nje.

Suala la mfumuko wa Bei,suala Hili lilipiganwa kihodari na kikomandoo na mh Rais wetu Jasiri na shupavu,mfano katika mafuta mh Rais alitoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi wakati katika kilimo hasa mbolea alitoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini Hali iliyo pelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu,yote hii Ni katika kumpunguzia maumivu mwananchi ,lakini pia bajeti ya kilimo imeongezeka kutoka billioni Mia mbili na point Hadi kufikia billioni Mia Tisa na point na Ikumbukwe kuwa bidhàa hizo hazikupandishwa Bei na serikali yetu Bali uliotokana na mfumuko wa Bei katika soko la Dunia hasa baada ya Vita ya ukrein.

Suala la maji,hapa pia miradi mbalimbali imeendelea kujengwa kila Kona ya nchi yetu Hali ambayo imesaidia upatikanaji wa maji kwa watanzania, na Ikumbukwe kuwa Mahitaji ya maji yanaongezeka kila Siku kutokana na idadi ya watu kuongezeka kila Siku na kila mwaka.

Matabaka katika Elimu,hili Ni upotoshaji wa makusudi imeifanya,kwa sababu kwa Sasa Elimu na mazingira ya Elimu yameboreshwa vizuri Sana ndio maana u aona hata matokeo ya mwaka Jana yalionyesha shule za serikali kwa matokeo ya kidato Cha nne na sita yalionyesha shule za serikali zikiwa miongoni mwa shule zilizofanya vizuri na kuwa na ufaulu mzuri,hata hivyo juhudi bado zinaendelea katika kuboresha secta hii,kwa kuboresha maslahi ya walimu,vitendea kazi vya kisasa kupongezwa,kuhakikisha maabara na vifaa vyake vinakuwepo kwa masomo ya sayansi ili kurahisisha usomaji wa masomo ya sayansi.
 
Mtaani watu wanajadili simba na Yanga, hayo mengine ni uchafu kwao.
Rais Samia kwa Sasa Ni Zaid ya Simba na yanga na Ni zaidi ya habari za feisali salumu na sakata lake la kwenda Azam fc,ElRais Samia Ndio habari ya mjini kwa sasa
 
Rais Samia ana nafasi kubwa mno ya kung'aa zaidi na zaidi kama atachanga karata zake vizuri sababu mtangulizi wake alikuwa kivuruge.
 
Mkuu unatafuta udc? Ameiteka mijadsla ipi labda, watu wanalia maisha magumu wewe unatuletea mapambio hapa. Umekula maharage ya wapi wewe
Angalia majibu yangu hapo chini nimetoa majibu kwa kina yanayojibu swali lako
 
Siku anaapishwa tu tulijua anaweza kuchukua marks za bure nyingi mno !! nafikiri na yeye anajua anachokifanya ni mdogo mdogo anawateka wananchi wa vicheko
Rais Samia kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuijenga nchi hii ndani ya muda mfupi hakika ndio sababu ya Kuendelea kuvuma Kama upepo masikioni na midomoni mwa watanzania,kila secta Kuna Alama za mh Rais,kila mahali amepeleka fedha za kutosha,miradi imejengwa kila mahali,huduma zimesogezwa karibu ya mwananchi
 
Rais Samia kwa Sasa Ni Zaid ya Simba na yanga na Ni zaidi ya habari za feisali salumu na sakata lake la kwenda Azam fc,ElRais Samia Ndio habari ya mjini kwa sasa

Unadhani kwakuwa unalipwa kupiga propaganda ndio utabadilisha ukweli?
 
Unadhani kwakuwa unalipwa kupiga propaganda ndio utabadilisha ukweli?
Tindo ndugu yangu Mimi silipwi na yeyote yule hata Mia Wala kuchangiwa hata hela ya vocha,Ni uzalendo wangu na kuridhishwa na uchapa kazi wa mh Rais Ndio unaonifanya niandike Yale nayoyaona na kuyasikia kutoka mitaani juu ya sifa kubwa anazopewa mh Rais
 

Kujipendekeza kwa rais ndio uzalendo? Mtaa upi huo wanamjadili rais wakati watu wameipuuza siasa baada ya kuingizwa mambo ya kishenzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…