Rais Samia Akabidhi Nyumba Kwa Mjane wa Dkt Magufuli (Mama Janeth Magufuli)

Rais Samia Akabidhi Nyumba Kwa Mjane wa Dkt Magufuli (Mama Janeth Magufuli)

ana-1-71.png
 
Sidhani kama kuna kiongozi wa Tanzania anaweza kuwa na mali na nyumba nyingi kama Magufuli! Nina hakika kwenye mgao kila mtoto ana nyumba zaidi ya mbili na bado mifugo na mashamba!
Ila kanuni ya dunia ndivyo ilivyo mwenye nyingi hupewa nyingi
 
Rizini ni mwanafunzi kwa huyu Abdul maana huyu ni hatari sn
Wiki iliyopita Rais wa Nigeria Mzee Tinubu kamtoa nduki kikaoni mtoto wake wa kiume,jamaa aliingia kwenye mkutano wa Mzee Tinubu na Wafanyabiashara bila mwaliko.
Mzee kamchana live mwanae kuwa Mimi kuwa Rais haimpi nafasi Mwanangu kuudhuria ata vikao ambavyo havimuhusu.
Mzee Tinubu kauzu sana!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
First gentleman atakuwa hapendi dhuluma wala wizi.
Mzee wa watu yupo kimya ameridhika na life lake.
Abdul fisi kweli labda ni right hand ya mamake
Design ya prince wa awamu ileeee
 
Kila siku nasema hawa jamaa hawajui kula na vipofu...; Hakuna sababu ya ku-publicize neema wanayopata kwa watu ambao kesho yao hawana hata pensheni let alone wale wazee ambao mafao yao hata panadol hayanunui...

Alafu wanakuja watu kwa kuuza sura na kupeana cake ambayo wanasema haitoshi ila kwa wao wanajipa na makombo....

In short they are out of touch..., ndio maana wanadai mafao kwa kila mke wa kigogo

By the way simuongelei huyu mama per-se, bali muendelezo wa hii animal farm...
Elite capture... Tumeingizwa kwenye mfumo
 
TZ bana, majumba yote aliyokuwa nayo Magufuli, mengine alikwapua za Serikali, mengine akagawa hadi kwa hawara zake wameona hazitoshi? Huku wananchi kibao wakilala kwenye mapagale na mitaro?
Elite capture... Tumeingizwa kwenye mfumo
 
Kila siku nasema hawa jamaa hawajui kula na vipofu...
Facts!

Hivi, najiuliza, shabaha ya hizi nyumba ni nini? Kwamba akitoka kuishi Ikulu apate pa kukaa??? Sasa hii miaka miwili Mama Magufuli alilala wapi ? JK alipewa nyumba miaka 5 baadae. Aliishi kwa nani hiyo miaka 5 ?

Haya, Samia anasema lazima tuwatunze hawa wastaafu. Na yeye atataka kutunzwa. Sasa hivi anajenga mjengo wa kufuru wa luxury apartments kule Kenyatta Drive, lakini na yeye tuje tumtunze! Daaah... Nchi zetu za Afrika zinabakwa non-stop, bila huruma.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mjane wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Mama Janeth Magufuli wakati wa hafla fupi ya kukabidhi nyumba ya kuishi iliyopo wilaya ya Kinondoni ambayo imejengwa na Serikali kwa mujibu wa sheria, Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023.
Kwanini hawa viongozi wanaendelea kujaziwa utajiri ilhali wameshalimbikiza vya kutosha? Kwanini wanajengewa Dar tu na sio mikoani?
 
Wiki iliyopita Rais wa Nigeria Mzee Tinubu kamtoa nduki kikaoni mtoto wake wa kiume,jamaa aliingia kwenye mkutano wa Mzee Tinubu na Wafanyabiashara bila mwaliko.
Mzee kamchana live mwanae kuwa Mimi kuwa Rais haimpi nafasi Mwanangu kuudhuria ata vikao ambavyo havimuhusu.
Mzee Tinubu kauzu sana!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
😕😕😕 yule mzee mnafiki mno
 
Back
Top Bottom