Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Kauli inayoonyesha kuwa rais wa JMT hana makuu na hawezi kuwa kiongozi wa kupenda makuu na kujiinua kama Mungu.
Rais Samia akataa tabia ya kutukuzwa.
===
Picha: Rais Samia Hassan Suluhu
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hana tabia ya kutukuzwa wala kulinganishwa na Mungu na kwamba atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu wa kusikiliza maoni ya wengine.
Rais Samia amesema hayo leo Jumanne Februari 22, 2022 katika sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.
Alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi aliyeemuomba Rais Samia kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.
“Baba Askofu katika kufunga hotuba yako umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hii si tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine. Maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie na siyo nijitukuze kwenu kwahiyo nitawatumikia,” amesema Rais Samia.
Amesema atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu na niwe na sikiko la kusikiliza yale yanayosemwa na wengine.
PIA SOMA:
- Askofu Niwemugizi amuomba Rais Samia asikubali kufananishwa na Mungu