Rais Samia akataa kutukuzwa, asema yeye hawezi kujilinganisha na Mungu

Ni jambo jema kama hataki kutukuzwa,basi itapendeza awaeleze watu wa chini yake kupunguza matumizi yasiyo na maana na kupoteza muda badala ya kwenda kutatua shida za wananchi,wanajazana airport kumpokea na maujinga jinga mengi pale......inatia kinyaa sana
 
Kauli inayoonyesha kuwa rais wa JMT hana makuu na hawezi kuwa kiongozi wa kupenda makuu na kujiinua kama Mungu.
Rais Samia akataa tabia ya kutukuzwa.

===

View attachment 2127410
Picha: Rais Samia Hassan Suluhu

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hana tabia ya kutukuzwa wala kulinganishwa na Mungu na kwamba atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu wa kusikiliza maoni ya wengine.

Rais Samia amesema hayo leo Jumanne Februari 22, 2022 katika sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.

Alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi aliyeemuomba Rais Samia kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.

“Baba Askofu katika kufunga hotuba yako umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hii si tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine. Maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie na siyo nijitukuze kwenu kwahiyo nitawatumikia,” amesema Rais Samia.

Amesema atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu na niwe na sikiko la kusikiliza yale yanayosemwa na wengine.

PIA SOMA:
- Askofu Niwemugizi amuomba Rais Samia asikubali kufananishwa na Mungu
Sawa lakini na wanaomkosoa wafanye kwa ustaarabu. Yaani kuwe na kusikilizana na kuheshimiana.
 
Ni vipi atakana kutukuzwa na wakati katiba imempa utukufu huo. Ni vema aangalie suala LA katiba mpya ndio tutamuamini vinginevyo ni kauli kinzani juu ya madhabahu.
 
Kwani nani alikuwa anapenda kutukuzwa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Askofu Niwemugizi amepiga kwenye mshono, maana alisikika akisema "Rais hakosei" [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] asiyekosea ni Mungu tu
 
Hakuna ufisadi uliokithiri kufanyika nchi hii kama enzi ya KIKWETE!! Nchi ilianza kupoteza dira ya maendeleo pale huyu mkwere alipoanza kutembea hovyo kwenda kuomba omba huku akiuza mbuga zetu za wanyama na fedha kuzificha nchi za nje!! Aliuza wanyama pori 600 kwa waarabu wa UAE na wao wakaanzisha mbuga yao ya wanyama pori huko jangwani kwao! Mpaka Leo hizo fedha walizolipwa na Waziri wake Nyalandu hazimo kwenye vitabu vya serikali!!
Kumbuka pia kuwa hata kashfa kubwa kubwa za fedha nyingi ikiwemo ile ya IPTL ,chimbuko lake ni Kikwete!!
Wizi nchi hii umeanza kabla ya JK. Kama unakumbuka suala la GAPCO enzi za Nyerere awamu ya kwanza. Masuala ya vivuko enzi za Nyang'anyi awamu ya kwanza.

Hizi tuhuma za kuuza wanyama ni story za mtaani za kunywea kahawa, huwa hazina ushahidi. Ni sawa na zile za mke wa Mwinyi Mama Siti kutorosha meno ya tembo pale uwanja wa ndege, eti Mrema ndio akazuia hiyo biashara, ni hadithi za kupakana matope.
 
Utasemaje kuwa tuhuma za kuuza wanyama ni story za mtaani za kunywea kahawa wakati tuliona ndege za Jeshi la UAE zikibeba wanyama toka KIA? Unataka Ushahidi gani zaidi ya kuwa huko UAE wameanzisha park ya wanyama kutoka Tanzania na ni kivutio cha watalii huko? Bado unataka ushahidi gani? Kwani Mrema hakukamata dhahabu pale uwanja wa ndege kutoka kwa yule mfanyabiashara kutoka Zanzibar? Wewe ulikuwa wapi? Hizi sio hadithi ni ukweli unaodhihirika.

Huwezi kufananisha wizi wa kivuko cha UNIFLOAT cha Mustapha Nyanganyi na wizi wa enzi ya Kikwete unless you are joking bwana Phillipo?
 
Ila ukitembelea vibanda vya magazeti utaona namna magazeti yanavyomsifia utadhani wapo kwenye mashindano ya nani anaweza kuandika habari za kusifu kuliko mwenzake.

Hakuna habari za kiuchunguzi tena ni sifa tu.
Taarifa ya habari ya vituo mbali mbali vya Tv ndiyo balaa,jina lake linatajwa kila habari
 
Kauli inayoonyesha kuwa rais wa JMT hana makuu na hawezi kuwa kiongozi wa kupenda makuu na kujiinua kama Mungu.
Rais Samia akataa tabia ya kutukuzwa.

===

View attachment 2127410
Picha: Rais Samia Hassan Suluhu

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hana tabia ya kutukuzwa wala kulinganishwa na Mungu na kwamba atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu wa kusikiliza maoni ya wengine.

Rais Samia amesema hayo leo Jumanne Februari 22, 2022 katika sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.

Alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi aliyeemuomba Rais Samia kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.

“Baba Askofu katika kufunga hotuba yako umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hii si tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine. Maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie na siyo nijitukuze kwenu kwahiyo nitawatumikia,” amesema Rais Samia.

Amesema atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu na niwe na sikiko la kusikiliza yale yanayosemwa na wengine.

PIA SOMA:
- Askofu Niwemugizi amuomba Rais Samia asikubali kufananishwa na Mungu
sikio la kusikia ya wengine,wakati ndugai aliposema ya kwake alichanwa chanwa na kuanikwa hadharani
 
Ilikuwa nafasi nzuri ya Mheshimiwa Rais kupiga marufuku utukuzaji unaoendelea. Kusema tu kuwa hapendi haitoshi. Ujumbe ungefika kama angesema hataki kusikia mtu anamfananisha na Mungu na sifa nyingine za kipuuzi. Kwa hili alilosema, ngonjera zitaendelea kupamba moto.

Amandla...
 
Kauli inayoonyesha kuwa rais wa JMT hana makuu na hawezi kuwa kiongozi wa kupenda makuu na kujiinua kama Mungu.
Rais Samia akataa tabia ya kutukuzwa.

===

View attachment 2127410
Picha: Rais Samia Hassan Suluhu

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hana tabia ya kutukuzwa wala kulinganishwa na Mungu na kwamba atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu wa kusikiliza maoni ya wengine.

Rais Samia amesema hayo leo Jumanne Februari 22, 2022 katika sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.

Alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi aliyeemuomba Rais Samia kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.

“Baba Askofu katika kufunga hotuba yako umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hii si tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine. Maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie na siyo nijitukuze kwenu kwahiyo nitawatumikia,” amesema Rais Samia.

Amesema atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu na niwe na sikiko la kusikiliza yale yanayosemwa na wengine.

PIA SOMA:
- Askofu Niwemugizi amuomba Rais Samia asikubali kufananishwa na Mungu
Mbona anataka asisimuliwe vibaya??!
 
Ajitafakari kwanini ameambiwa hivyo?
Aliyemwambia hayo ni mpuuzi kama wapuuzi wengine. Angetoa ushahidi wa uungu alionao Mh Samia. Pumbamvu kabisa huyo askofu
 
Aonyeshe kwa vitendo..kupiga marufuku mapokezi na usindikizaji usio na msingi..kupiga marufuku sherehe yake ya kuzaliwa kufanywa maulidi ya taifa...apige marufuku hawa uvccm wanaojipendekeza na tuvimisemeo vyao vya nyuki wa mama n.k.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kauli inayoonyesha kuwa rais wa JMT hana makuu na hawezi kuwa kiongozi wa kupenda makuu na kujiinua kama Mungu.
Rais Samia akataa tabia ya kutukuzwa.

===

View attachment 2127410
Picha: Rais Samia Hassan Suluhu

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hana tabia ya kutukuzwa wala kulinganishwa na Mungu na kwamba atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu wa kusikiliza maoni ya wengine.

Rais Samia amesema hayo leo Jumanne Februari 22, 2022 katika sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.

Alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi aliyeemuomba Rais Samia kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.

“Baba Askofu katika kufunga hotuba yako umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hii si tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine. Maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie na siyo nijitukuze kwenu kwahiyo nitawatumikia,” amesema Rais Samia.

Amesema atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu na niwe na sikiko la kusikiliza yale yanayosemwa na wengine.

PIA SOMA:
- Askofu Niwemugizi amuomba Rais Samia asikubali kufananishwa na Mungu
Nadhani hili ni dongo kwa 'hayati'. Huko aliko kazi anayo.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Nawakumbusha tu wakati hayati raisi Mkapa (RIP) anaanza uraisi kuna watu hasa wasoma taarifa za habari na waandishi wa magazeti walikuwa wanaanza kwa kutamka/kuandika MTUKUFU RAISI BENJAMIN MKAPA. Hayati raisi Mkapa alitoka hadharani mwenyewe akakataza tena kwa ukali kuitwa hivyo na akasema aitwe mheshimiwa/ndugu raisi kwani mwenye utukufu ni Mungu tu.

Kwenye suala hili la kutukuzwa wakati mwingine sio lazima watu watamke bali tu hata matendo ya watu wanaokuzunguka yanaweza kuonyesha kuwa unatukuzwa kama Mungu. Tunayaona haya mitaani, maofisini, kwenye nyumba za ibada, n.k. na wengine wanafurahi kabisa. Lakini suala kubwa mimi ninaliona sio kutukuzwa kama Mungu bali wewe unayetukuzwa unachukua hatua gani kukemea/kukataza hadharani kutukuzwa kama Mungu kama alivyofanya hayati raisi Mkapa.

Kwa upande wangu alichozungumza baba askofu Niwemugizi jana nadhani yupo sahihi kwa sababu alikuwa anamkumbusha tu mheshimiwa raisi kuwa awe makini. Kwani wale waliompa utukufu wa kimungu mtangulizi wake kiasi cha wengine kumuita/kumfananisha na Mungu/Yesu/Mtume Muhamad hadharani tena wengine walikuwa viongozi wakubwa tu wa kiserikali na kidini wameshaanza taratibu kumpeleka huko.

Na jambo zuri kwa mheshimiwa raisi jana ile ile katamka kwa kinywa chake mwenyewe na kila mtu kasikia kuwa hataki huo utukufu wa kimungu yeye ni mtu wa kujishusha sana. Na kwa kuwa raisi ni msikivu sana basi na tumaini hili jambo atalitafutia tu jukwaa na kulikemea hadharani tena kwa ukali ili hii mbegu mbaya iliyoaanza kumea ife kabisa mazima. Na kama alichozungumza jana alikuwa anaamanisha basi tutaona huko mbele ya safari maneno na matendo yake na ndio tutakuwa nafasi ya kuhukumu kwani muda ni mwalimu na wakati mwingine ni mwamuzi mzuri wa kila jambo.

Kwa ufahamu wangu mimi na imani yangu ya dini pamoja na kusoma maandiko mbalimbali nafahamu na naamini kuwa utukufu ni wa Mungu tu. Na Mungu ana wivu sana na utukufu wake. Na mara nyingi Mungu amedhihirisha utukufu wake kwa wale wote wanaojaribu kujipa utukufu kama yeye kwa aidha wao wenyewe au kupewa na watu wengine halafu wao wakaukubali.

Ni mtizamo tu.
 
Back
Top Bottom