Rais Samia akataa kutukuzwa, asema yeye hawezi kujilinganisha na Mungu

Rais Samia akataa kutukuzwa, asema yeye hawezi kujilinganisha na Mungu

Hata Petro alikataa kuwa siyo mfuasi wa Yesu lakini matendo yake tu yalionyesha, hatuoni anavyoshangiliwa akitoka Ulaya watu wanaacha kazi zao kama vile ametoka mbinguni na kutumia gharama kibao za walipa kodi
Hakuna aliyeambiwa na Rais,aache kazi,ni mapenzi yao kwa Rais wao.
 
Mama kwa nukta hiyo tuu Mungu akubariki sana.

#SSH
 
Baba Askofu Niwemugizi amemuona ana uelekeo huo wa kupenda kutukuzwa na kuabudiwa kama MUNGU ndio maana amegonga nyundo palepale utosini.

Amemuonya ili asije akaingia mtego wa Jiwe aliyechanganyikiwa; akakubali kuabudiwa na wakina Kangi Lugola katika uchawa wao wa kujipendekeza na hatimaye akatwaliwa kizembe zembe!!
 
Marais wa kiislam huwa ni wanyenyekevu hawana makuu. Wanajua kujishusha siku zote. Simuoni SSH akienda tofauti na JK, simuoni akienda tofauti na Mwinyi.

Hawana ule ushamba wa kutaka kutatua matatizo yote ya dunia eti wayamalize watakapokuwa wameondoka ikulu.
Ndio wanaongoza kwa kuuza mbuga na maliasili bure.
 
Uliujulia wap kama hauandikwi?
Wavaa kanzu ni hopeless na maisha yao ndio siasa nje ya siasa ni wala pweza tu na urojo.
Ndio wastaafu marais walio hai mpaka dakika hii, ni waungwana wasio na kiburi wala ubabe wa kijinga.

Hawaweki vitu moyoni, na Mungu anawapa siku nyingi za kuishi duniani.
 
Ndio wastaafu marais walio hai mpaka dakika hii, ni waungwana wasio na kiburi wala ubabe wa kijinga.

Hawaweki vitu moyoni, na Mungu anawapa siku nyingi za kuishi duniani.
Kuwa hai haijustify ni wema Mungu anawacha hai ili watubu mazambi yao.
Mungu anasema hafurahii kifo cha mwenyen dhambi bali kutubu kwake.
 
Wanasiasa wote wanapenda KUABUDIWA.

Utasikia wengine wanaitwa MWAMBA, CHUMA, KAMANDA WA ANGA, RAIS WA MIOYO, MKOMBOZI KATUMWA na MUNGU😀😀😀😀
 
Mkuu roho yako ni nzito sana kwa urais wa SSH, unatumia nguvu kubwa kujaribu kupotosha maana ya kauli aliyoisema kuhusu ujenzi wa mwendo kazi itakayotumia umeme.

Alisema huenda baada ya miaka mitano au sita tukawa na treni zinazotumia umeme kama ulaya.
Sasa unanipigia kelele mimi kwani hiyo habari ni ya kwangu au ni ya BBC?🐒🐒🐒
 
🐒🐒🐒
QS3Pr.jpg
 
Mama hana tabia hiyo, mmeanza kumsingizia hamuoni ametufundisha kulipa kodi kwa lazima kwa maendeleo yetu, Ameweka mawaziri wenye uelewa mkubwa juu ya Hotspot 😄Kazi iendelee mazee
 
Ila ukitembelea vibanda vya magazeti utaona namna magazeti yanavyomsifia utadhani wapo kwenye mashindano ya nani anaweza kuandika habari za kusifu kuliko mwenzake.

Hakuna habari za kiuchunguzi tena ni sifa tu.
 
Kwani hata kama hatujui kusoma hata picha hatuoni? kwanini baba Askofu aseme/amwambie hivyo?
Wale CHAWA walioenda uwaja wa ndege kumpokea na kujifanya wamachinga wanajisikiaje?
 
Umesahau mabaya ya viongozi wa kikristo, ufisadi usioandikwa magazetini lakini upo na ni mkubwa.

Hakuna ufisadi uliokithiri kufanyika nchi hii kama enzi ya KIKWETE!! Nchi ilianza kupoteza dira ya maendeleo pale huyu mkwere alipoanza kutembea hovyo kwenda kuomba omba huku akiuza mbuga zetu za wanyama na fedha kuzificha nchi za nje!! Aliuza wanyama pori 600 kwa waarabu wa UAE na wao wakaanzisha mbuga yao ya wanyama pori huko jangwani kwao! Mpaka Leo hizo fedha walizolipwa na Waziri wake Nyalandu hazimo kwenye vitabu vya serikali!!
Kumbuka pia kuwa hata kashfa kubwa kubwa za fedha nyingi ikiwemo ile ya IPTL ,chimbuko lake ni Kikwete!!
 
Kauli inayoonyesha kuwa rais wa JMT hana makuu na hawezi kuwa kiongozi wa kupenda makuu na kujiinua kama Mungu.
Rais Samia akataa tabia ya kutukuzwa.

===

View attachment 2127410
Picha: Rais Samia Hassan Suluhu

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hana tabia ya kutukuzwa wala kulinganishwa na Mungu na kwamba atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu wa kusikiliza maoni ya wengine.

Rais Samia amesema hayo leo Jumanne Februari 22, 2022 katika sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 inayofanyika wilayani Ngara mkoani Kagera.

Alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi aliyeemuomba Rais Samia kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile.

“Baba Askofu katika kufunga hotuba yako umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hii si tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine. Maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie na siyo nijitukuze kwenu kwahiyo nitawatumikia,” amesema Rais Samia.

Amesema atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu na niwe na sikiko la kusikiliza yale yanayosemwa na wengine.

PIA SOMA:
- Askofu Niwemugizi amuomba Rais Samia asikubali kufananishwa na Mungu
Kauli ya kistaarabu kabisa ya rais. Mheshimiwa rais kwa hii kauli yake anatoa matumaini na imani kwa umma. Ni kauli ya ukomavu na anaonyesha ni kiasi gani anavyokwenda kuleta mustakabali mzuri wa Taifa hili. Angekuwa ni mtu mwingine angeona amevunjiwa heshima kwa kuelekezwa namna ya kuishi na walio chini yake. Gradually rais anaenda kukonga nyoyo za binadamu wa Tanzania
 
Back
Top Bottom