Rais Samia akataa mwananchi kueleza shida kwenye mkutano, amtaka amfikishie kupitia mbunge

Huyo Mama ana kiburi na dharau sana!
 
Ili iweje? Rais hawezi kusikiliza kero za mtu mmoja mmoja, na hata akisikiliza hawezi kufanya maamuzi hapo kwa hapo, maana inawezekana huyo mwananchi akawa anapotosha pia. Kama yule mama wa Tanga alivyompotosha Magufuli
Kwani akisikiliza alafu akaliacha kwa RC,kuna shida gani?
Moja ya sifa ya Kiongozi bora ni kusikiliza!
 
Ni kweli Rais hawezi kusikiliza kero za mwananchi mmoja mmoja, itakuwa jau sana .... mwingine kapigwa na mumewe anataka kesi apeleke kwa Rais, tutamaliza saa ngapi?
Alisimamisha msafara kwa maana gani sasa?
 
Kwanini asingetembea tuu hadi Nagwanda kuhutubia tuu au uwanja wa Ilulu kuhutubia? Kilichomsimamisha njiani ni nini?
Au kama anaona Tanzania ni kubwa arudi kwao Zanzibar akaongoze wachache. Au Tz igawanywe, kanda ya ziwa iwe taifa linalijitegemea. Kwa kifupi huyu ni rais wa matajiri. Maskini watasubiri sana.

Kwa mfano hapo angekuwa ni rostam au tajiri fulani ana hoja yake binafsi, angeacha kumsikiliza?
 
Lost a chance to get it from the horse's mouth. What a waste?
 
Sasa kilichomfanya asimame njiani ni nini? Kwanini asingelikwenda moja kwa moja uwanjani?[emoji23][emoji23][emoji23]
Rais anaweza kusimama popote anapotaka
 
Lakini pia malalamiko mengi kwenye eneo yanampa Rais picha pana juu ya uwezo wa viongozi aliowateua katika eneo husika.
 
Kwani akisikiliza alafu akaliacha kwa RC,kuna shida gani?
Moja ya sifa ya Kiongozi bora ni kusikiliza!
Maana ya kuwa na wasaaidizi au kuwa na viongozi wa serikali ni nini?

Wewe umewahi shuhudia wapi rais akisikiliza kero za mtu mmoja mmoja hapa duniani? At huyo wa marekani ushawai sika?
 
Ni kweli Rais hawezi kusikiliza kero za mwananchi mmoja mmoja, itakuwa jau sana .... mwingine kapigwa na mumewe anataka kesi apeleke kwa Rais, tutamaliza saa ngapi?
Tungejiuliza kwanza kwanini kuwe na wananchi wengi wanaotaka kumweleza rais shida zao wakati ngazi za chini kuna wateule wa rais chungu nzima! Hili ndilo tatizolinalotakiwa kutatuliwa. Wabunge kwa nini hawatimizi majukumu? Wakuu wa wilaya nk kwa nini hawatekelezi majukumu? Jibu ni kuwa hawajioni kama wanawajibika kwa raia. Wanajiona kuwa rais ndiyo bosi wao. Bila kubadisha mfumo ni bure.
 
Ule mtindo wa Magufuli ulikuwa ni upumbavu tu kwa wananchi wapumbavu. Hakukuwa na leadership pale. Hivi Rais mmoja utawezaje kumsikia kila mwananchi?

Endelea hivyo hivyo Samia na wala usiingie mtego wa kugawa hela barabarani
Sasa kwani na huyu anaendeleza huo unaoitwa upumbavu wa kusimama njiani? Alisimama kuongea na nani hapa kama sio hao wananchi ambao hataki kujibu maswali yao hata moja? Au wakuuliza maswali hakuandaliwa?
 

Attachments

  • IMG_0974.jpeg
    54.6 KB · Views: 2
Hapana, Rais anatakiwa ashughulike na mambo ya kitaifa. Huyo raia unaweza kukuta analalamikia kesi ya mirathi ya familia yao au kucheleweshwa mshahara kazini kwake.
Sasa yeye Rais kasimama pale kwenye kadamnasi kufanya nini,si angepita speed na kuwapungia mkono!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…