Rais Samia akataa mwananchi kueleza shida kwenye mkutano, amtaka amfikishie kupitia mbunge

Za uraisi, anaomba kwa wabunge wabunge wanaenda kumuombea kwa raia anakua hapati shida ya kukutana na raia wenye ziki na matatizo mengi yasiyoisha
Hata asipoomba kabisa hizo kura italeta tofauti gani,
Magufuli alifanya mikutano mingapi ya kampeni mwaka 2020 huko Kusini??
 
Ni hopeless person and can not share love and hope to people. Leaders are meant change things and offer immediate solutions to issues. Hopefully ako low sharpness kwenye brain
Alichosema Rais ni kweli,
Na kama ni kweli basi sijaona haja ya yeye kusimama hapo.
 
Sababu ya msingi ya Rais kusimama barabarani ni nini hasa, huku ni kutokujitambua na kutojua uwajibikaji, in rare occasion chipping from the grassroots it's a good thing, a big shame and worse empty mind
Rais anaweza kusimama popote,
 
Kidumu CHAMA CHA MASELA
ukoloni mamboleo umetupa UHURU wa bendera,tuone kufuru za wenye HELA.
 
Kwani akisikiliza alafu akaliacha kwa RC,kuna shida gani?
Moja ya sifa ya Kiongozi bora ni kusikiliza!
Ili mawasiliano yakamilike,lazima kuwe na feedback kutoka kwa hadhira.
Communication ni 2 way process,na siyo 1 way.
 
Kilichomsimamisha njiani ni nini kama sio mataizo binafsi ya wananchi? Kwanini ana sima simama njiani ikiwa anaogopa maswali? Kwanini ana simama simama?
Kazi ya Rais sio kutatua matatizo binafsi ya raia. Kazi ya Rais ni kushughulika na kuzungumzia mambo ya kitaifa na kimataifa sehemu yoyote anayoona inafaa kufanya hivyo.
 


Point za bure zinapotea.
 
Kwani akisikiliza alafu akaliacha kwa RC,kuna shida gani?
Moja ya sifa ya Kiongozi bora ni kusikiliza!
Rais katika nchi kubwa kama hii akianza kusikiliza kesi za mirathi, ugomvi wa mke na mume, kuibiana kuku n.k tutafika kweli??
 
Sasa yeye Rais kasimama pale kwenye kadamnasi kufanya nini,si angepita speed na kuwapungia mkono!
Rais anaweza kusimama popote kama vile raia mwingine yeyote anavyoweza kusimama popote.
 
Unakuta mwananchi keshafikisha kero zao kwa ngazi za chini na ameshashugulikiwa ila unakuta hajaridhika anataka aende kwa Rais..Hilo lilijitokeza mara nyingi awamu ya Magufuli ambapo unakuta wamama waalishindwa kesi na rufaa zote kwenye ngazi za chini wakafanya vituko kwenye mikutano ya Magufuli wakidai kuwa wamedhulumiwa, kumbe hawakuwa na haki na wao ndio walikuwa wakosaji
 
Kama ameenda hasikilizwi,afanyeje?
Kwanza, kwanini mnaweka assumption kuwa anataka kuongea mambo personal.Wengine huwa Wanaongea mambo ya Hospitali, Barabara,umeme nk,vitu ambavyo viongozi wa sehemu husika hawavifanyii kazi.
Unakumbuka ile shule ya Ubungo ilivyokuwa ovyo,watu wakarusha clip,Rais Magufuli akaiona na kuagiza ijengwe mara moja na ilijengwa.Je,wangekaa kimya ingejengwa?
Viongozi wa Tanzania Wilayani na Mikoani ni wazembe sana,Kwaiyo kwa Rais unayeijua tabia ya viongozi wako ni lazima utumie njia mbadala pia kujua matatizo ya Wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…