Rais Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na Mshindi wa Miss World 2025 huko Kizimkazi, Zanzibar

Rais Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na Mshindi wa Miss World 2025 huko Kizimkazi, Zanzibar

Kwanini alikimbia mkuku dodoma jana na kurudi kizimkazi
Ina maana mambo ya mamis ni muhimu sana kuliko mustakabali wa chama chetu cha ccm?
Ingekua draft hapo ni king tatu zimeliwa na kete mbili, yaani maza kaahirisha mchujo wa wagombea,so waliokua wamejipanga na fitna zao,wakajipange tena
 
Ikulu ya Dodoma ni hadi sasa ni upotevu wa rasilimali za walipa kodi.

Sasa iidhinishwe tu kila rais awe anakaa kwao ili kupunguza gharama za posho za usafiri na kazi kwenye msafara wa rais.
Sio Ikulu tu.

Mpango mzima wa kuhamishia mji mkuu Dodoma ulikuwa ujinga mtupu usio na tija ya kiuchumi.

Kiufupi nchi masikini yenye matatizo mengi yanayohitaji pesa nyingi kuyatatua imeenda kutatua tatizo ambalo halipo kwa pesa nyingi, huku matatizo yaliyopo yanakosa pesa za kuyatatua.
 
Wewe lofa hiyo picha sio ya leo
Aliingia Tanzania tarehe 15.07.2025, yaani Jumanne. Sijui kama bado yupo Bongo
1753016272150.jpeg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mshindi wa Miss World 2025 Bi. Opal Suchata Chuangsri mara baada ya mazungumzo yaliofanyika Kizimkazi, Zanzibar tarehe 20 Julai, 2025.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Miss World Limited ulioongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wake Bi. Julia Evelyn Morley, Mshindi wa Miss World 2025 Bi.Opal Suchata Chuangsri kutoka Thailand, Miss World Africa Bi. Hasset Dereje Admassu kutoka Ethiopia, Kizimkazi Zanzibar tarehe 20 Julai, 2025. Pia kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi wa Wizara ya Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, pamoja viongozi wa Maliasili na utalii. Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilijadili namna ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya Miss World 2026.

View attachment 3412092



Hapa chini Rais akiwa anacheza

View: https://www.instagram.com/reel/DMUyqs7MO-F/?igsh=NTc4MTIwNjQ2YQ==






View attachment 3412105

Anaangaika sana...
 
Back
Top Bottom