Rais Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na Mshindi wa Miss World 2025 huko Kizimkazi, Zanzibar

Rais Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na Mshindi wa Miss World 2025 huko Kizimkazi, Zanzibar

Sasa Chawa wanapotosha kwa maslahi ya nani? Su ni kweli kasusa...!!?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mshindi wa Miss World 2025 Bi. Opal Suchata Chuangsri mara baada ya mazungumzo yaliofanyika Kizimkazi, Zanzibar tarehe 20 Julai, 2025.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Miss World Limited ulioongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wake Bi. Julia Evelyn Morley, Mshindi wa Miss World 2025 Bi.Opal Suchata Chuangsri kutoka Thailand, Miss World Africa Bi. Hasset Dereje Admassu kutoka Ethiopia, Kizimkazi Zanzibar tarehe 20 Julai, 2025. Pia kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi wa Wizara ya Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, pamoja viongozi wa Maliasili na utalii. Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilijadili namna ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya Miss World 2026.

View attachment 3412092



Hapa chini Rais akiwa anacheza

View: https://www.instagram.com/reel/DMUyqs7MO-F/?igsh=NTc4MTIwNjQ2YQ==






View attachment 3412105

cc. britanicca
 
Yote kwa yote ,muda ni mwalimu mzuri giza litaingia na kutakucha
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan anaendelea kuwa Kiongozi anayependwa na mwenye ushawishi zaidi Duniani Kwote, anaendelea kuwa kiongozi mwenye nguvu na mvuto wa kisiasa na kiuongozi Duniani Kwote, anaendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa kila mtu.

Kila mmoja sasa anatamani kuonana na Rais wetu ,kila mtu maarufu anatamani kupata picha na Rais Samia ,kila mtu anatamani kufika Tanzania na kuonana na Rais Samia. Sasa Dunia yote kwa sasa inaiangalia Tanzania kama Nchi ya Ndoto ambayo kila mmoja anatamani walau katika Maisha yake aweze kupata Bahati ya kuitembelea Nchi yetu.

Sasa Dunia na walimwengu wanakimbilia kuitembelea Nchi yetu,sasa kila mtalii anataka kufika kwanza Tanzania,sasa kila kiongozi,mwana michezo ,mwana mziki anataka kufika Tanzania ya Rais Samia.

Hii leo Dunia Nzima imeshuhudia Mrembo wa Dunia au waweza kusema miss world Bi Opal Suchata akitua ndani ya Kizimkazi Zanzibar kuonana na kupata picha ya pamoja na Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Nuru na Mwanga wa Tanzania. Ambapo mrembo huyo amefurahi sana kupata bahati ya kipekee ambayo wengi wanaitafuta usiku na mchana kuweza kuonana na Rais wetu.

Hii maana yake nini? Hii maana yake ni kubwa Dunia ina imani kubwa sana na Rais Samia pamoja na nchi yetu iliyo katika mikono salama na safi ya Rais Samia. Dunia inaitazama Tanzania kama kisiwa cha amani ,utulivu na usalama zaidi ambapo au mahali au sehemu ambapo mtu anaweza kufika au kutembelea na kupumzika kwa amani na utulivu wa hali ya juu kabisa na akarejea Nchini kwake vizuri kabisa.

Ndio sababu ya kuona idadi ya watalii ikiongezeka na kupaa kama ndege vita ,ndio sababu ya kuona mapato yatokanayo na utalii yakiongezeka ,ndio sababu ya kuona ajira za moja kwa moja pamoja na zile zisizo za moja kwa moja zikiongezeka zaidi katika secta hii ya utalii. Ndio sababu ya kuona Nchi yetu ikiwa chaguo nambari moja la watalii kutoka kila kona ya Dunia pale wanapotaka kutua ndani ya Bara la Afrika.

Hii yote ni kazi ya akili ya Rais Samia aliyekuja na wazo la Royal Tour iliyoifungua na kuifumbua Dunia macho kujua nini kipo na kinapatikana Tanzania. Hii ndio maana ya kusema kiongozi mwenye maono ,akili ,maarifa na upeo wa kiuongozi. Sasa wote tumeanza kuona matunda ya kazi ya mikono ya Mama yetu Mpendwa. Sasa Leo Dunia imemtizama na kumuonea sana wivu Miss World kwa kupata Bahati ya kipekee kabisa ya kuonana na Rais wetu Mpendwa
Screenshot_20250720-213457_1.jpg
Screenshot_20250720-213422_1.jpg
Screenshot_20250720-213443_1.jpg
Screenshot_20250720-213422_1.jpg
.

Kwa hakika Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe na ni zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kuitunza na kuilinda kwa wivu mkubwa sana.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mshindi wa Miss World 2025 Bi. Opal Suchata Chuangsri mara baada ya mazungumzo yaliofanyika Kizimkazi, Zanzibar tarehe 20 Julai, 2025.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Miss World Limited ulioongozwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wake Bi. Julia Evelyn Morley, Mshindi wa Miss World 2025 Bi.Opal Suchata Chuangsri kutoka Thailand, Miss World Africa Bi. Hasset Dereje Admassu kutoka Ethiopia, Kizimkazi Zanzibar tarehe 20 Julai, 2025. Pia kikao hicho kimehudhuriwa na Viongozi wa Wizara ya Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, pamoja viongozi wa Maliasili na utalii. Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilijadili namna ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya Miss World 2026.

View attachment 3412092



Hapa chini Rais akiwa anacheza

View: https://www.instagram.com/reel/DMUyqs7MO-F/?igsh=NTc4MTIwNjQ2YQ==

😀😀😀😆 kumbe kweli buana!




View attachment 3412105
 
Back
Top Bottom