Rais Samia akizindua Jukwaa la Mfumo wa Chakula barani Afrika leo tarehe 17 Machi, 2023 Ikulu, Dar es Salaam

Rais Samia akizindua Jukwaa la Mfumo wa Chakula barani Afrika leo tarehe 17 Machi, 2023 Ikulu, Dar es Salaam

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizindua Jukwaa la Mfumo wa Chakula barani Afrika leo tarehe 17 Machi, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 
Rais Samia siku ya leo amefungua mkutano mkubwa wa wadau wa kilimo ulimwenguni kote. Mkutano umefanyika Ikulu jijijini Dar es Salaam. Tunakushukuru kwa juhudi kubwa kwenye sekta ya kilimo na kwa kuonesha kwa watanzania kuwa, tusipoteze muda na chochote siku hii ya leo ila tuchape kazi na kuboresha kilimo chetu.

Hongera kwa uchapa kazi wako!
 
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa Afrika wa masuala ya chakula na kilimo utakaofanyika Septemba 5 mpaka 8 mwaka huu.

Ijumaa wiki hii (Machi 17), Rais Samia Suluhu Hassan atazindua maandalizi ya mkutano huo Ikulu, Dar es Salaam, hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Zuhura Yunus.

Mkutano wa Afrika wa chakula wa Septemba unatarajiwa kuhudhuriwa na watu takribani 3,000 kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika na duniani, ikiwemo marais, mawaziri na wakuu wa taasisi za kimataifa.

Mkutano huo utaweka msisitizo kwenye Vijana na Wanawake kama Msingi wa Mfumo Endelevu wa Chakula.

Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na hatua kubwa za kimageuzi ambazo serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imezichukua tangu alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita.

Hatua hizo ni pamoja na kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mara nne kwa mwaka wa fedha 2022/2023, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu tupate uhuru.

Serikali ya Rais Samia pia imetambuliwa kwa mradi wake wa ubunifu wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), ambao unalenga kuwawezesha vijana, ambao ndiyo nguvu kazi kubwa nchini, kuingia katika kilimo.

Serikali yake pia imewekeza kwenye miundombinu ya umwagiliaji, huduma za ugani, pembejeo na ruzuku ya mbolea na mbegu kwa viwango ambavyo havijawahi kufanyika miaka ya nyuma.

Serikali ya Rais Samia pia imekuwa ikitekeleza mpango wa kilimo unaojulikana kama Ajenda 10/30 yenye lengo la kufanya kilimo kiwe cha biashara na kikue kwa wastani wa asilimia 10 kwa mwaka ifikapo 2030.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizindua Jukwaa la Mfumo wa Chakula barani Afrika leo tarehe 17 Machi, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Kilimo kinazinduliwa Dar es Salaam? Utani mbaya sana mmekusanyana kujilipa posho kodi za wananchi kwa mambo ya kufikirika
 
Mama Samia rais wetu siku ya leo amefungua mkutano mkubwa wa wadau wa kilimo ulimwenguni kote. Mkutano umefanyika Ikulu jijijini Dar es Salaam. Tunakushukuru kwa juhudi kubwa kwenye sekta ya kilimo na kwa kuonesha kwa watanzania kuwa, tusipoteze muda na chochote siku hii ya leo ila tuchape kazi na kuboresha kilimo chetu. Hongera kwa uchapa kazi wako!
tusipoteze muda na chochote siku hii ya leo ila tuchape kazi na kuboresha kilimo chetu[emoji23]
 
Rostam ndani ya Nyumba

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Huyu bwana na Mshika remote, si wakawapiga watu kwa kuwauzia hisa za voda....

Kuna mjuvi amesema serikali imempa mkopo akajenge kiwanda Kenya, sijui ikoje hii ila kwa akili zao hawa, naona no bora niamini kwa 99.9% kwakuwa ndo walivyo.
 
Mama Samia rais wetu siku ya leo amefungua mkutano mkubwa wa wadau wa kilimo ulimwenguni kote. Mkutano umefanyika Ikulu jijijini Dar es Salaam. Tunakushukuru kwa juhudi kubwa kwenye sekta ya kilimo na kwa kuonesha kwa watanzania kuwa, tusipoteze muda na chochote siku hii ya leo ila tuchape kazi na kuboresha kilimo chetu. Hongera kwa uchapa kazi wako!
Chawa km chawa,mi nitamsifia siku akisema TZ hatutaki mashoga as Kenya na ug vinginevyo nitamuona mnafiki na muuza nchi Kwa mashoga
 
Muosha huoshwa, nae ikifika zam yake watamfyeka tu na itabakia story🤣
Unakumbuka kipindi kile jamaa anafanya teuzi kujaza nafasi na wakati huo ata mwili wa waziri wetu haijapumzishwa? Hii ilikuwa inaashiria hakuna kupoteza siku kwenye mambo ya uombolezaji.
 
Back
Top Bottom