Rais Samia akosa imani na Waziri Mashimba Ndaki

Rais Samia akosa imani na Waziri Mashimba Ndaki

Acheni siasa za udini anahojiwa na Mhe Rais kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake sio kwa sababu ya dini yake kama watu wanakwambia samaki wameisha Ziwa Victoria kwa sababu ameshindwa kudhibiti uvuvi haramu na leo bei ya samaki haishikiki, watu wanauana kila siku kwa migogoro ya wakulima na wafugaji wewe unaleta upuuzi wa udini?
Mpuuzi mwenyewe, Makamba umeme unakatika kila saa, mafuta yapo juu na vitu vingine mbona hatuoni akihojiwa?
 
Mmeanza kuwasagia kunguni..anyway hiyo wizara aliiweza luhaga mpina..sa100 amrudishe hapo...ila sijui kama watakaa meza moja kwenye kikao cha baraza na yule kipara.

#MaendeleoHayanaChama
Kwani wanashida na kipara? Labda msomari kwa alivyo muandama na mbolea, Lakini watakua wamesha ya maliza.
 
Acha ujinga tumia akili hakuna anayetaka cheo cha mtu anayetoa uongozi ni Mwenyezi Mungu na sio wewe yaani tusindwe kumuunga mkono Mhe Rais aliyeonyesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa Mashimba wewe unaleta mzaha
Mbona kama wewe ndie unaehaingaika zaidi kuliko hata Rais mwenyewe,tuliza wenge wewe
 
Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji, wafugaji ni wavamizi wa maeneo ya wakulima kutokana na kuhamahama kutafuta malisho ya mifugo yao. Wafugugaji wadhibitiwe kwenye maeneo yao ya kuchungia
 
kwani? inakuwaje nyuzi zote inamtaja Mashimba? sio bure kuna shida
Screenshot_20220904-142845.png
 
Rais Samia Suluhu Hassan amenukuliwa na magazeti mengi ya leo akitoa onyo la mwisho kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki kutokana na usimamizi mbovu wa Wizara yake na kudaiwa huku fedha nyingi zikidaiwa kupotelea kwenye mifuko ya watu.

Naungana na Rais Samia, Mashimba ameonyesha kushindwa kwa kiwango kikubwa kutekeleza majukumu yake hasa katika maeneo kadhaa ikiwemo kusababisha kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji kurudi upya na watu kuuana mfano Kilindi, Rufiji, Kilimanjaro, Mbeya na maeneo mengine ya nchi mambo ambayo hapo nyuma yalitulia.

Mashimba ameshindwa kusimamia Rachi za Taifa na kusababisha Serikali kupoteza mapato mengi kutokana na usimamizi mbovu wa sekta hiyo.

Pia kulikuwa na utaratibu wa kuogesha mifugo kwa dawa za ruzuku jambo hilo Waziri Mashimba ameua utaratibu huo na kusasabisha wafugaji wengi kushindwa kuongesha mifugo yao na mingi kufa kwa magonjwa.

Mashimba pia ameshindwa kusimamia sekta ya uvuvi na kusababisha samaki kupungua sana Ziwa Victoria na maeneo mengine kutokana na kushamiri kwa uvuvi haramu na kusababisha uhaba wa samaki na dagaa na kwamba anadaiwa kuwa hafanyi juhudi zozote za kudhibiti uvuvi haramu kwa kisingizio kuwa Rais amesema watu wasionewe.

Mashimba amekuwa akitumia vibaya jina la Rais kwamba ndiye ameruhusu uvuvi haramu na mifugo iendelee kutoroshwa nje ya nchi jambo ambalo sio la kweli kwani hakuna kiongozi wa Serikali aliyeapishwa kulinda rasilimali za nchi akaruhusu ziharibiwe eti kwa kisingizio cha hataki watu kuonewa wakati Sheria za nchi zinataka mali hizo zilindwe.
Nafasi imetafutwa mpk imepatikana 😀😀😀😀
Serikalini hizi nafasi fitna ni nyingi sana

Hongera sana Waziri mpya wa Mifugo,umeitafuta sana hio nafasi 😀😀😀
 
Mimi nimefanya kazi na Mashimba akiwa kama Manager wangu kwenye shirika kubwa tu na baadae akawa Director, Bampa to Bampa nimekua naye karibu miaka 7 na ninajua uwezo wake wa kwazi ni mkubwa sana, ila kama Kuna fitina za kisiasa basi Kwa sababu aliingia kwenye Siasa hatakosa wanafiki, isitoshe tunajua Kanda ya ziwa inaondolewa kiaina lakini ni watu wenye uwezo mkubwa tu wa kufanya kazi

World Vision kama sikosei
 
Back
Top Bottom