Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Sio kweli! % inapungua kila unapopanda juu, usije shangaa kule juu wanaambulia 5% ambayo inaweza kuwa huo mshahara wako baada ya nyongeza ya hiyo 23.3%[emoji41][emoji41]
Inaishia 9% Hawa ni wale ealiopo kwenye bar. Nadhani mtawekewa jedwali humu kila mtu ajione amekaa wapi. Cha muhimu wa chini kabisa ndo 23.3%
 
Mimi nadhani pia JPM aliwaangalia sana watuwa chini(sio waajiriwa) aliwapa uhuru mkubwa sana katika kutafuta riziki zao, hadi kufikia kuamua wao wafanye biashara popote, na hili lilifanya mtu wa chini asilalamike, tofauti na mfanykazi ambaye mda wote kipindi cha JPM alikuwa haishi kulalama.
Watu wasiokua na ajira ndio wengi

Wenye ajira za serikali hawazidi milioni moja.

Sasa kuwafurahisha watu milioni moja na kuacha milioni 50 wasononeke sidhani kama ni wazo zuri.
 
Chadema mlikuwa mnamsifia Kenyatta kuongeza asilimia 15 mkatukana CCM na Raisi Mama Samia mbona siwaoni njooni huku mumsifie Raisi Mama Samia

Mumekalia kusifia nje tu maruhuni nyie msio na uzalendo.Mama Samia kavunja rekodi ya Kenyata mliyekuwa mkimsifia hadi mkawa mnajisikia haja kubwa kwa kumsifia
 
Watu wasiokua na ajira ndio wengi

Wenye ajira za serikali hawazidi milioni moja.

Sasa kuwafurahisha watu milioni moja na kuacha milioni 50 wasononeke sidhani kama ni wazo zuri.
Sasa hivi low class wanaumia zaidi, trust me. Lakini pia hata wafanyabiashara wanaumia kwa sababu uwezo wa kununua wa watu umepungua hivyo biashara nyingi hazifanyi vizuri.

Tuombe hili ongezeko liwe chanya kwa kila mtu, hata asiye mwajiriwa wa serikali, kwa maana ya mfanyabiashara.
 
Hii 23.3% kwa kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma? Ina maana gani hasa? Msishangilie kwa hili​

Kwa hiyo wasio kima cha chini wanapata ngapi?
Hiyo sentensi ya "kwa kima cha chini" ni tata.
Kuna mtego mkali umesukwa, subiri vilio hiyo July.
Si mnakumbuka kwenye chama alivyofanya?
N.B: Shangilia ukiwa na uelewa.
 
Watu wasiokua na ajira ndio wengi

Wenye ajira za serikali hawazidi milioni moja.

Sasa kuwafurahisha watu milioni moja na kuacha milioni 50 wasononeke sidhani kama ni wazo zuri.
Wewe jamaa mbona una akili za kichawi sana ?. Hebu basi tufanye hao watumishi wa serikali wasiwe hata wanapokea mshahara maana umeumia sana kuongezewa hako ka nyongeza .
 
Basic salary yako itakuwa hivi.
940,000 + (940,000 x 23.3%) = 1,159,020

Kutokea hapo sasa utakata
NHIF
PSSF
CWT/ TALGWU etc
PAYE nk

Mfano hai sasa.
BASIC SALARY ... 1,159,020
PSSF 5% (57,951)
INCOME TAX (128,000 + (101,069 × 30%)) = (158,320.7)
NHIF 4% ..............
TALGWU/CWT 5% ..............

HAPO UTAONA JINSI MSHAHARA UTAVYOKATWA PAKUBWA ZAIDI.

NB nimeashume tu haudaiwi HESLB, BENKI wala SACCOS yoyote. Na hizo % za NHIF na CWT na vyama vya wafanayakazi sina uhakika kama zinafanana.

Utajionea mwenyewe jinsi hiyo 23.3% itakavyoenda kukupasua.
Na yeye sio kima cha chini🤣🤣🤣
 
Tujiylize
Mkuu
KWA kima cha chini pesa itakayo ongezeka ni 62,910/=
Hivyo
940000+62910= 1,002,910/=
Hiyo ni kama ongezeko likiwa constant KWA wote!!!

Sio kweli asilimia 23.3 ya 940000 ni hii 62910?
 
Naelewa nachosema, nchi zote Duniani hutumia hiyo standard katika kuset mishahara. Unapongeza mshahara huwezi sema kila kada itakuwa hivi na hivi, Unataja kwa ujumla sasa kima cha chini kitapanda kwa % kadhaa, hapo una maanisha wengine wataongezeka kutokana na asilimia hizo hapo.

SERIKALI INAPANDISHWA MISHAHARA KWA WATUMISHI WAKE WOTE KWA UJUMLA NA RATE SAWA. MTATOFAUTINA POSHO KULINGANA NA TAASISI.
Mwaka jana kima cha chini walitoka 170000 hadi 270000. Wengine huku tukaongezewa buku mbili mia tank 2500.
 
Wewe jamaa mbona una akili za kichawi sana ?. Hebu basi tufanye hao watumishi wa serikali wasiwe hata wanapokea mshahara maana umeumia sana kuongezewa hako ka nyongeza .
Elite mwenzangu Kongolee
 
Mwaka jana kima cha chini walitoka 170000 hadi 270000. Wengine huku tukaongezewa buku mbili mia tank 2500.
Hawakuongeza mshahara mwaka jana, walipunguza KODI na kupandisha level ya kipato ambacho mtu atalipia KODI.

WE ULISIKIA MTU AMEPANDISHWA MSHAHARA???
 
Wengi mnajadili hiyo 23.3% mbona hamuangalii hiyo mkupuo 33% au hilo mmeshalisahau. Hilo lingeangaliwa kwa jicho la pili mjadala ungependeza.
 
Back
Top Bottom