Kila mtu akijiajiri nani atafundisha watoto wako utakaowazaa? Vp kuhusu polisi watakaolinda biashara yako uliyojiajiri?
Huyu
Jane Lowassa ni mjinga na hajielewi, achana naye...
Hajui kuwa mtu hupata mahitaji yake muhimu ya kila siku i.e chakula, mavazi, malazi (mahali pa kuishi/kulala) nk nk kwa KUFANYA KAZI. Kazi yaweza kuwa ya kujiajiri au kuajiriwa na mtu, taasisi, shirika au serikali ...
Duniani kote na nchi yoyote kuna mgawanyo wa kazi (DIVISION OF LABOUR). Haiwezekani kila mtu ajiajiri na kuwa mfanyabiashara binafsi, machinga, mkulima nk nk..
By the way, hata uwe mfanyabiashara uliyejiajiri mwisho wa siku utahitaji wafanyakazi kukusaidia kazi zako ambao ni lazima uwalipe mshahara. Hawa wafanyakazi mara kwa mara utakuwa unakaa nao mezani ku - negotiate maslahi. This is very common. Ukiwapuuza na kuwadharau shughuli zako zikwame na biashara yako inaanguka..!
Jane Lowassa, suppose kila mtu angekuwa kwenye duka/biashara yake "aliyojiajiri (kama usemavyo), nani sasa angekuwa mhasibu wake? Dereva wake? Mbeba mzigo wake? nk nk
Duniani, binadamu wote tunaishi kwa kutegemeana...
Mfanyabishara aliyejiari kama wewe
Jane Lowassa unamhitaji nesi, daktari, dereva wa gari yako, mwalimu afundishe watoto wako shule, msukuma mkokoteni abebe bidhaa zako nk nk..
Si hivyo tu, bali mfanyakazi huyu mwalimu, askari polisi au jeshi, daktari, Mtendaji wa kijiji, dereva, mkatisha tiketi, mwendesha mitambo kiwandani nk nk wanapopata mishahara yao mwisho wa siku wanampelekea mfanyabiashara au mtoa huduma aliyejiajiri in exchange with goods/services...
Jane Lowassa, asikudanganye mtu. Waliojiajiri/wafanyabishara wenye akili huomba na kupigana kufa na kupona kuhakikisha mfanyakazi ana mshahara kila mwezi au kila siku tena ulioboreshwa ili wawe na uwezo kununua bidhaa au huduma zao...
Ni mfanyabishara aliyejiari mjinga pekee anayeweza kuwaponda na kuwaombea wafanyakazi na wakulima mabaya maana hiyo inakuwa ni chanzo cha kudoda kwa bidhaa au huduma zao...!!
Jane Lowassa mpaka hapo umeelewa? Au bado uko gizani?