Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Nipo
Ila umeelewa vizuri hapo kilichoandikwa? Maana najua walimu wengi upeo ni mdogo
Kweli Aisee Walimu wengi wana upeo mdogo maana Magufuli mwenyewe alishakua ni Mwl na upeo wake tuliouona ulivyokua hafifu.
 
Hebu nisaidieni kwa mnaojua kukokotoa hizo asilimia. Kwa mfano mwenye basic salary ya 940, 000/= hiyo aailimia 23 ndio inakuwa sh. ngapi?

Piga 0.23 zidisha mara 940000 jibu utaona kama 216 yaani laki mbili na 16 ndio ongezeko lako hivo utafika kwenye milioni laki moja na hamsini hivi
 
Una elimu gani mkuu?? Kwahiyo aliyekuwa analipwa 330000 mwanzoni ataendelea kulipwa hivyo kwa akili yako?
Nyongeza ya mishahara inasetiwa kwa kima cha chini ili kubalance kule juu, hivyo nyongeza ya kima cha chini maana yake unawasogeza wengine juu zaidi.
Mwaka jana waliongeza kima cha chini kutoka 170,000/= mpaka 270,000/= lakini wale wa juu hatukuguswa.
 
Sioni sababu ya kitaalamu ya kuonheza mishahara kwa wafanyakazi wa umma.

Serikali unatakiwa kujikita kupandisha thamani ya shilingi ya Tanzania ili pesa inayo patikana kwa wananchi kwa ujumla wao iweze kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

Kuoambana na mufumko wa bei ya bidhaa na huduma mbalimbali.

Upo ushahidi kila mshahara unapo panda bidhaa hupanda bei .

Hivyo inawaumiza wale wasio na mshahara wa mwezi Bali ni wahangaikaji wa vibarua visivyo rasimi.
Mchawi si lazima aruke na ungo
 
Kila mtu akijiajiri nani atafundisha watoto wako utakaowazaa? Vp kuhusu polisi watakaolinda biashara yako uliyojiajiri?
Huyu Jane Lowassa ni mjinga na hajielewi, achana naye...

Hajui kuwa mtu hupata mahitaji yake muhimu ya kila siku i.e chakula, mavazi, malazi (mahali pa kuishi/kulala) nk nk kwa KUFANYA KAZI. Kazi yaweza kuwa ya kujiajiri au kuajiriwa na mtu, taasisi, shirika au serikali ...


Duniani kote na nchi yoyote kuna mgawanyo wa kazi (DIVISION OF LABOUR). Haiwezekani kila mtu ajiajiri na kuwa mfanyabiashara binafsi, machinga, mkulima nk nk..

By the way, hata uwe mfanyabiashara uliyejiajiri mwisho wa siku utahitaji wafanyakazi kukusaidia kazi zako ambao ni lazima uwalipe mshahara. Hawa wafanyakazi mara kwa mara utakuwa unakaa nao mezani ku - negotiate maslahi. This is very common. Ukiwapuuza na kuwadharau shughuli zako zikwame na biashara yako inaanguka..!

Jane Lowassa, suppose kila mtu angekuwa kwenye duka/biashara yake "aliyojiajiri (kama usemavyo), nani sasa angekuwa mhasibu wake? Dereva wake? Mbeba mzigo wake? nk nk

Duniani, binadamu wote tunaishi kwa kutegemeana...

Mfanyabishara aliyejiari kama wewe Jane Lowassa unamhitaji nesi, daktari, dereva wa gari yako, mwalimu afundishe watoto wako shule, msukuma mkokoteni abebe bidhaa zako nk nk..

Si hivyo tu, bali mfanyakazi huyu mwalimu, askari polisi au jeshi, daktari, Mtendaji wa kijiji, dereva, mkatisha tiketi, mwendesha mitambo kiwandani nk nk wanapopata mishahara yao mwisho wa siku wanampelekea mfanyabiashara au mtoa huduma aliyejiajiri in exchange with goods/services...

Jane Lowassa, asikudanganye mtu. Waliojiajiri/wafanyabishara wenye akili huomba na kupigana kufa na kupona kuhakikisha mfanyakazi ana mshahara kila mwezi au kila siku tena ulioboreshwa ili wawe na uwezo kununua bidhaa au huduma zao...

Ni mfanyabishara aliyejiari mjinga pekee anayeweza kuwaponda na kuwaombea wafanyakazi na wakulima mabaya maana hiyo inakuwa ni chanzo cha kudoda kwa bidhaa au huduma zao...!!

Jane Lowassa mpaka hapo umeelewa? Au bado uko gizani?
 
Sekta binafsi ili uongezewe mshahara inabidi uongezewe kazi, ila serikalini mtu anaongezewa mshahara bila kuongezewa kazi?
Sekta binafsi output yako itafanya uongezewe mshahara au ubaki kama ulivyo, huko serikalini wao wanaongezwa tu, vigezo nadhani ni "kupanda kwa gharama za maisha". No wonder watu wengi wanapigania ajira za serikali ili "wakapumzike".
 
Je wewe ni mtumishi wa serikali? Maana kuongeza asilimia za mshahara kwa kima cha chini hakujaanza mwaka huu.
Kumbuka hata kwenye kodi ilipunguzwa kwa wenye kima cha chini ikawa asilimia 8 kwa wenye kima vha chini kama sijakosea wakati ambao hawapo kwenye kima cha chini wanalipa zaidi ya hapo.
Hivyo wanapotumia kima cha chini wana sababu zao za kimahesabu. Hii 23% sio flat rate na utakuja kukiri mwenye hapa.
Kubisha mie siwezi.
kwenye chapisho kumeandikwa IKIWEMO KIMA CHA CHINI kwa 23.3% hii umeelewa vipi!?.
 
Haiwezi ikawa hivyo mkuu - hilo ni ongezeko la jumla na ndio maana inahitajika kujua mtu anafall kweye tax band gani ili kuwa na specific % increase, although wa chini watapata ongezeko kubwa mana kodi ni ndogo... Ngoja tupate jedwali la kodi na jinsi walivyoainisha kwanza, ni mapema kucalculate hivyo.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Okay...

Nimekuelewa ndugu yangu...
 
Ukiongeza mishahara unavutia ongezeko la gharama za maisha.

Hapa tulipo tayari gharama za maisha zipo juu bado tunaongeza mishahara mambo yanazidi kuwa magumu zaidi.

Halafu unapoongeza mishahara ina maana kuna pato la ziada.

Je hilo pato la ziada lipoo?? Au tunafanya siasa tu wakati hali hairuhusu.
Gharama za maisha hazipungui kwa kupunguza uwezo wa raia wako kufanya manunuzi tu.

Hata kuongeza matumizi ya serikali kwa mataifa mengine kama kutoa tenda, kufanya malipo makubwa nje bila kuongeza uwezo wa manunuzi kwa raia wako nako kunaongeza gharama za maisha sababu wananchi wako wanakuwa hawana pesa.

Viwanja vitauzwa hata milioni na hiyo milioni mtu hatakuwa nayo sababu hulipi mishahara na raia hawana uwezo wa maendeleo zaidi ya kula.

Unatakiwa kubalance, ukiona raia wana pesa nyingi unazipunguza, ukiona raia hawana pesa unaziongeza. Wakati mwingine gharama za maisha zinakuwa juu sababu uchumi unakuwa ni wa serikali tu bila kuhusisha wananchi.
 
Back
Top Bottom