Kwa wanaojua hesabu, ili mtu apate chake calculation zake zinakuwa vipi....?
Je, kila mtu anaongezewa 23.3% ya kiwango chake cha sasa cha mshahara [basic salary] anaupata sasa, kwa mfano;
MTUMISHI: Joseph Mang'ula
KADA YA UTUMISHI: Afya
NGAZI YA MSHAHARA: TGSS D.
KIWANGO: TZS 760,000
## Hii 23.3% itaingia kama ilivyo? Kwa maana ya;
760,000 × 23.3/100 = 177, 080
##KWA HIYO; Kwa ukokotozi huo, maana yake nyongeza ya 23.3% kwa mtumishi huyu itakuwa TZS 177, 080
##Na ukijumulisha na basic salary yake ya zamani, mtumishi huyu basic salary yake kuanzia July, 2022 itakuwa;
TZS 177,080 + 760,000
= TZS 937,000 [BS]
## Kama inakokotolewa hivi, basi naweza kusema SIYO HABA. Serikali imefanya vizuri...
I stand to be corrected