Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Rais Samia akubali ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma

Kuna watu wengi hawajui kikokotoa asilimia 23.3 ya mshahara wao....Hatari sana
 
Legacy pekee ambayo Magufuli angeiweka na kukubarika ni kupandisha mishahara ila yeye alichagua kuikacha na kuweka legacy ya ubabe na udikteta uchwara
 
Hebu ngoja hapa:-
23.3/100=0.233
0.233×270000/= =62,910
KWA hiyo:-
270000+62910=332,910/=
KWA kima cha CHINI hicho!!
Nakaribisha masahihisho kama yapo!!
Mimi Raisi ajaye nimeona hivi KWA lima cha CHINI ya wewe je!!?
Lakini Kuna issue moja: Hadi Sasa kima Cha chini kilikuwa hakitozwi Kodi, je baada ya ongezeko hili kitaendelea kutozwa Kodi? Kama kikitozwa Kodi bado take home itasinyaa!
 
Kumbuka wa kima cha juu hata akiongezwa 23.3%, makato yake ni makubwa kuliko huyu wa kima cha chini, kuanzia PAYE, PSSSF, BIMA, vyama vya wafanyakazi etc.
Ni kweli lakini nimesema kutokana na uzoefu maana hii si Mara ya kwanza kupandisha kima Cha chini. Haijawahi kutokea kuwa watumishi wote wakaongezwa kwa asilimia zinazofanana. Labda ianzie Mwaka huu!!
 
kwenye chapisho kumeandikwa IKIWEMO KIMA CHA CHINI kwa 23.3% hii umeelewa vipi!?.
Maana yake ni kuwa mishahara imepanda Ila kwa kima Cha chini imepanda kwa asilimia 23. Haiwezekani kuainisha kiasi kwa Kila mshahara. Kwa kawaida asilimia ya ongezeko hupungua kwa kadri mshahara unavyokuwa mkubwa. Ila kwa kuwa tuna MAMA na anajua kuwa wafanyakazi wamesota kwa miaka 6, anaweza kuagiza watumishi wa ngazi zote wapate ongezeko la asilimia 23.3!! Tutafurahi!
 
The increament is between 9% and 23.3%...

Defenetely, YES, it's not flat rate...

Pamoja na hayo, siyo haba hii...

Mathalani mtu mwenye BS ya 3,000,000 ukimwekea 9% maana yake ni almost TZS 300,000...

Hii siyo ndogo, ni kubwa...
Hii umeipata wapi? weka ushahidi!
 
Ila

TUCTA kupendekeza mafao ya wastaafu walipwe asilimia 33 ni usaliti mkubwa kwa wafanyakazi. Jambo zito kama hilo TUCTA walipaswa waendeshe zoezi la kupata maoni ya wafanyakazi kila sehemu ya ajira ( taw) ndipo wawasilishe kikokotoo kinachotokana na wafanyakazi wenyewe. Kwa kikokotoo hicho kuna wafanyakazi wengi wataambulia sh milioni saba mpaka 25 badala ya kati ya shilingi milioni 40 hadi mia walizokuwa wanapata awali kwa wale waliostaafu bila cheo. Ninamaanisha malipo ya mkupuo.

Kupunguzwa kwa rate ya kikokotoo ni suicide rope kwa wafanyakazi
TUCTA ni tawi la CCM usitarajie hata siku moja wakafanya hivyo, katika awamu ya 5 ndo hawakusikika kabisa wamekuja kuibuka awamu hii wakiwa na hayo mapendekezo mkononi
 
Inaishia 9% Hawa ni wale ealiopo kwenye bar. Nadhani mtawekewa jedwali humu kila mtu ajione amekaa wapi. Cha muhimu wa chini kabisa ndo 23.3%
Kama Hilo jedwali unalo tuwekee hapa! Utakuwa umefanya la maana Sana!
 
Fomula ya kukokotoa asilimia 23 ya kima cha mshahara ipo hivi:
Kima Cha chini Cha mshahara Tanzania ni 300000/=
23/100x300,000=69,000/=
Hivyo 69000-18% ya makato yote utaona umeongezewa sh.ngapi?
18/100x69,000=12,420/=
Sasa 69,000-12,420=56,580/=
Hivyo basi nyongeza ya mashahara ni 56,580/= kwa kila mtumishi.
Hivyo tegemeeni nyongeza ya 56,000/= kwenye mshahara.
Ndugu zangu msije pigia 23%ya basic eti ndio nyongeza mtakuta Julai ni tofauti kabisa.
 
Inaishia 9% Hawa ni wale ealiopo kwenye bar. Nadhani mtawekewa jedwali humu kila mtu ajione amekaa wapi. Cha muhimu wa chini kabisa ndo 23.3%
Mkuu, ikiwezekana hilo jedwali ulifungulie uzi maalumu kwani hili jambo limekuwa ni mjadala mkubwa mitandaoni.
 
Back
Top Bottom