Rais Samia akutana na Baraza la Maaskofu (TEC), Kilaini aelezea Historia yake na utaifishaji wa mashule 1970

Kwahio hao viongozi walikaa kimya mpaka leo kuja kulalamika na kushitaki kwa huyu aliyepo..., huenda na huyu wakamshitaki kwa atakayekuja !!!

Bongo Sanaa kila kona...., na waliokuwa wanasema chaguo la Mungu sio hawa ?
 
Mwendazake na team yake kina chakubanga na yule mbunge wa viti maalumu bashiru wote wale hili taifa wangetugawa ni bora mungu alipoamua kuingilia kati
 
Kanisa liache kutaka mteremko
Limeanzisha huduma za Elimu na Afya kibiashara
Basi lilipe kodi lisitake mteremko wa kusamehewa kodi wakati linatengeneza fedha
Naunga mkono hoja ,, lilipe kodi kwani huduma linazotoa halitoi bure, wananchi wanalipia tena hela nyingi tu. Labda waombe kupunguziwa lakini siyo kuondolewa.
 
Mama ni Ester wa Bahati Bukuku kama hamjui, yupo tayari hata aukose uongozi wa term ijayo ila awakomboe watu. Let's pray for her ooh!!
 
Mama aache kutafuta huruma za kisiasa kwa hao wakatoliki,wanafanya biashara walipe kodi
 
ni kweli mkuu, maana hata bei zao haziakisi utofuati na wanaolipa kodi.

yaani shule za kanisa nazo bei sio mchezo
No research no right to speak!!shule za kanisa Katoliki kwa elimu zinatoa na kiwango cha pesa wanachotoza ni sawa na bure tu!! Mfano shule nyingi zinatoza kati ya laki tano mpaka millioni moja na nusu,kiwango cha kawaida tu.
Ninachoona watanzania wengi wamezoea vitu za bure hawajui kama kuna gharama za uendeshaji,kama uwezi kulipa pesa hio,mpeleke mwanao shule ya bure ya kata..tuache ujinga watanzania elimu ni ghali sana,ukiona uwezi acha usisome kabisa.
 
Unataka hospital iendeshwe Kama madrasa ?

Shule iendeshwe Kama mikutano ya hadhara?
Kuna costs za uendeshaji.
swali ni moja, kuondolewa kodi katika hizo huduma italeta unafuu wa bei wanazotoza? au italingana ama kuzidi bei za hospt / shule za private zinazotozwa kodi?
 
usitake nifunguke hicho unacho kiita research
 
swali ni moja, kuondolewa kodi katika hizo huduma italeta unafuu wa bei wanazotoza? au italingana ama kuzidi bei za hospt / shule za private zinazotozwa kodi?

Watoe kwanza hizo kodi ndio uje uhoji hilo swali lako!!

Ni sawa na uulize huyu mwanamke nikimuoa atazaa? Muoe kwanza ndio uone Kama atazaa ama lah.
 
ukute ye ndie alikua kigogo
 
Huu mwandiko ni kama flani hivi.... Utasema ni moja ya ids zake!
 
Kitendo cha Rais Samia kukutana na viongozi wa kanisa Katoliki pekee ni cha kibaguzi sana. Rais anahubiri haki huku akijua kuwa tabia aliyoianzisha ya kuwagawa Watanzania kwa imani ya Dini zao si cha kiungwana.

Tanzania ina madhehebu mengi sana kwa nn ukutane na dhehebu moja tu uyaache mengine huo sio ubaguzi?

Najitahidi sana kulazimisha kukupigiadebe lkn dah yataka moyo kwa hiyo utakutana na wasabato, Walutheri, waanglikani, PAG, Washia wasuni hapana umekosea sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…