Rais Samia akutana na rais wa TLS, Mwabukusi - Ikulu ya Chamwino Dodoma

Takbiriiii........Allahuakbar
 
Raisi wa chama Chama Cha wanasheria(TLS)wakili Boniface mwabukusi akutana na raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mwabukusi ambaye ameongea kwa bashasha ameongeza kuwa wao kama TLS wanamuunga mkono raisi Samia kwani ni kiongozi msikivu ambaye ametumia mda mrefu wa zaidi ya masaa matatu kuwasikiliza na kuwapa majibu ya baadhi ya hoja zao
 

Attachments

  • Screenshot_20250827-220111.png
    343.8 KB · Views: 24
Rafiki kipenzi cha Lissu amemwakilisha Lissu......au nasema uongo ndugu zangu?
 
Ni moja ya majukumu yake na ni lazima jukumu hilo lifanywe kitaaluma na sio kisiasa. Sasa ukiangalia sehemu kubwa mambo mengi yanaendewa kisiasa hadi imefika hatua TLS inaonekana kama ni Chadema B
 
Hapana sio kweli, enzi za Lisu ni aliileta tu kwenye public eyes ila sio kuwa ndio ilikuwa na nguvu bali ndio ilianza kupoteza nguvu zake. Kuna tofauti kubwa kati ya nguvu na umaarufu.

Na ukiangalia wote hawa wawili ni wanasiasa tena wa wazi wazi na hapo ndipo tulipokosea kuendelea napo kama chama. Hauwezi kuwatenga wakiwa viongozi na maslahi binafsi kisiasa.

Wakati TLS ikiwa na utulivu ndio wakati ina nguvu sana.

Sasa hivi kuna matamko mengi sana lakini ni matamko mfu yasiyotekelezwa kwa namna yoyote kitaaluma, matokeo yake na TLS inakuwa inalalamika kama wananchi wasioijua sheria.

TLS leo imeshindwa kuondoa vishoka wa sheria, imebaki kuanzisha mara vikoba vya mawakili. Hii ni aibu kubwa sana.
 
Sasa mbona hawakupigana jamani?
 
Ubabe wote wa mwabukusi kumbe hamna hamna ni kilele tu walisema wao ni wanasheria kumbe madem tu

USSR
Kama unaona ni rahisi na wewe omba appointment na rais, au hata mkuu wa wilaya ya Kisarawe.
Sidhani hata kama ungepata hiyo fursa ya kukutana na rais ungekua na la kumuambia zaidi ya kuomba kazi.
 
Napata picha zaidi kwamba Polepole na Gwajima sio watu wa kawaida. Wametisha!
 
Hilo la kumuunga mkono umeongeza chumvi
 
Ni moja ya majukumu yake na ni lazima jukumu hilo lifanywe kitaaluma na sio kisiasa. Sasa ukiangalia sehemu kubwa mambo mengi yanaendewa kisiasa hadi imefika hatua TLS inaonekana kama ni Chadema B

..TLS wanaponzwa na haiba ya Chadema ktk kutetea HAKI.

..yeyote anayetetea haki sasa hivi anaonekana kama ni mfuasi wa Chadema.

..hata viongozi wa Dini wakitetea haki wanaambiwa wanachanganya dini na siasa, na kuwa ni wana Chadema.

..vivyo hivyo kwa asasi na vyama vya kitaaluma.

..kwa upande wangu naamini TLS walipaswa kufanya zaidi ya wanavyofanya sasa hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…