Namuona hapo Nkwande amesinzia kabisa...
Itoshe tu kusema kwenye Dunia ya Sasa Umwamba wa Kanisa Katoliki Duniani umeshaporomoka sana kufuatia kuendesha mambo yake mengi kwa kutegemea Wafadhili ambao wamepungua sana.
Kanisa sasa limeshajikabidhi mikononi mwa Serikali na Wakuu wa Serikali wanalitambua hilo.
Hata kwetu hapa Serikali ikiondoa ufadhili mfano wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Binafsi..TEC hawatamudu kuendesha SAUT kwa ufanisi nje ya kupandisha ada juu sana kufidia gepu la Wafadhili na kisha kukoswa Wanafunzi.
Hata Hospitali zao nyingi Teule na Rufaa kama Bugando Serikali ikijitoa na kuondoa ruzuku na kuwaachia TEC watazifunga.
Hii Taasisi kwa sasa ipo kijanja janja sana ila kiundani Uchumi ulishaporomoka hawana ubavu wa kutunishiana misuri na Serikali yoyote.
Mtu kama Trump ndiyo maana alimpa shit Papa baada ya kupigia kelele uvamizi wa Marekani kwa Irani.anajua hana lolote kwani Taasisi anayoiongoza iko taabani.
Vita ya kwanza ya Marekani na Iraq ya Sadam Hussein Papa Yohane Paul-II alienda kwa dharura Marekani kumuomba Bush Mkubwa asianzishe vita hiyo na siku hiyohiyo walipozungumza Usiku wake Bush akatoa amri ya Vita kuanza..
Hii ya hapa pia haishangazi..za akina Kitima zile ni kelele za Kihulka na binafsi tu siyo za Kitaasisi na hata wakubwa wake wakiambiwa wamdhibiti watatii.
Na hiki kikao ndiyo Mwisho wa kelele za Padri Kitima kwa Serikali.Hata Method Kilaini alitulizwa na akatulia.