Rais Samia akutana na Viongozi wa TEC - Ikulu, Chamwino

Rais Samia akutana na Viongozi wa TEC - Ikulu, Chamwino

Nchi haitawaliki!
Kule Kikwete na VP.
Huku SSH na TEC.
Uzuri TEC si Bakwata... Walikumbushana majukumu na wajibu wao kimkakati!

View: https://www.instagram.com/reel/DbsdLfDuCJs/?igsh=MXh3bmNnMHVxd2JtbQ==

Siasa za ccm ni upofu! Kitima huyo huyo leo wanagundua hawawezi kusonga bila yeye!

Soon, tutaona Maaskofu wakikutanishwa na TAL!
Ila kwa utume wa TAL, sijui... Mwamba ni muadilifu na mkweli kwa Tanganyika yake kupitiliza!
 
Namuona hapo Nkwande amesinzia kabisa...

Itoshe tu kusema kwenye Dunia ya Sasa Umwamba wa Kanisa Katoliki Duniani umeshaporomoka sana kufuatia kuendesha mambo yake mengi kwa kutegemea Wafadhili ambao wamepungua sana.

Kanisa sasa limeshajikabidhi mikononi mwa Serikali na Wakuu wa Serikali wanalitambua hilo.

Hata kwetu hapa Serikali ikiondoa ufadhili mfano wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Binafsi..TEC hawatamudu kuendesha SAUT kwa ufanisi nje ya kupandisha ada juu sana kufidia gepu la Wafadhili na kisha kukoswa Wanafunzi.

Hata Hospitali zao nyingi Teule na Rufaa kama Bugando Serikali ikijitoa na kuondoa ruzuku na kuwaachia TEC watazifunga.

Hii Taasisi kwa sasa ipo kijanja janja sana ila kiundani Uchumi ulishaporomoka hawana ubavu wa kutunishiana misuri na Serikali yoyote.

Mtu kama Trump ndiyo maana alimpa shit Papa baada ya kupigia kelele uvamizi wa Marekani kwa Irani.anajua hana lolote kwani Taasisi anayoiongoza iko taabani.

Vita ya kwanza ya Marekani na Iraq ya Sadam Hussein Papa Yohane Paul-II alienda kwa dharura Marekani kumuomba Bush Mkubwa asianzishe vita hiyo na siku hiyohiyo walipozungumza Usiku wake Bush akatoa amri ya Vita kuanza..

Hii ya hapa pia haishangazi..za akina Kitima zile ni kelele za Kihulka na binafsi tu siyo za Kitaasisi na hata wakubwa wake wakiambiwa wamdhibiti watatii.

Na hiki kikao ndiyo Mwisho wa kelele za Padri Kitima kwa Serikali.Hata Method Kilaini alitulizwa na akatulia.
Movement anazofanya kitima sio za kitaasisi ni hulka zake tu, TEC Haina misuli ya Kuvuambiana na serikali
 
Movement anazofanya kitima sio za kitaasisi ni hulka zake tu, TEC Haina misuli ya Kuvuambiana na serikali
Wakizingua Mafwele na CCM watateka TEC yote,Mashule, Hospital mpaka na Wanafunzi na Wagonjwa wote.

Hapo Kitima kabebwa na akina Nkwande...."..Ahiii!twende yakaishe..."tu..

Labda watumie vitisho vya kumuotesha ndoto za ajabu Samia..maana hiyo Teknolojia Wakatoliki wanayo...Mwezi mzima mfululizo awe anaota anacharaza kinanda na kupiga chetezo St Joseph Kanisani.Samia na yeye ajibu kwa Majini.kiumane..
 
Movement anazofanya kitima sio za kitaasisi ni hulka zake tu, TEC Haina misuli ya Kuvuambiana na serikali
Tec Ina nguvu kuliko serikali! Nguvu ya Tec huioni Wala haitumii mabomu ila 70% ya gvt work force Iko chini ya TEC Kuanzia walimu mpaka mainjinia wa tanesco jwtz Hadi tiss Sasa hao wote wakiamua liwalo na liwe gvt inaanguka hapo hapo.
 
Hapa nani kamuita mwenzake ?
Tujue muelekeo
Wewe ni mtu makini.

Soma mstari wa kwanza aya ya mwisho ya tangazo la mkutano huo.

Inasema hivi: ".....aliwashukuru maaskofu hao KWA KUONA UMUHIMU WA KUKUTANA....".

Haya maneno yamewekwa hapo maksudi kuonyesha kuwa ni maaskofu ndio waliona umuhimu.
Lugha ya kilaghai vile vile inayofahamika kwa tabia za huyu mwanamke mwovu.

Hawa ni wazi wameitwa; ikiwa ni katika mpango ule ule wa kutafuta njia za kujisafisha maovu waliyotendewa waTanzania.
 
View attachment 3647791View attachment 3647792View attachment 3647793

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 10 Agosti, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference - TEC), Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na TEC na kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa yanayoigusa jamii, yakiwemo ya kisiasa, imani na maendeleo, pamoja na kuimarisha amani, mshikamano na kujenga mustakabali mwema wa Taifa.

Aidha, mazungumzo hayo yaligusia umuhimu wa nafasi ya madhehebu na Viongozi wa Dini katika kulea jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano, ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika ustawi na maendeleo endelevu ya Taifa.

Soma Pia: Rais Samia amefanya mazungumzo na Viongozi wa Vyama vya Siasa Ikulu Dar es Salaam

Mheshimiwa Rais aliwashukuru Maaskofu hao kwa kuona umuhimu wa kukutana na kujadiliana naye masuala yenye tija kwa Taifa na kuwahakikishia dhamira yake ya kuendeleza utamaduni wa kushauriana na kushirikisha Viongozi wa Dini na makundi mbalimbali katika jamii kuhusu masuala muhimu ya kitaifa kila inapohitajika.

View attachment 3647795
Hatua nzuri sana katika kujenga utengamano wa kitaifa, Hongereni sana viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom