Rais Samia akutana na Viongozi wa TEC - Ikulu, Chamwino

Rais Samia akutana na Viongozi wa TEC - Ikulu, Chamwino

Namuona hapo Nkwande amesinzia kabisa...

Itoshe tu kusema kwenye Dunia ya Sasa Umwamba wa Kanisa Katoliki Duniani umeshaporomoka sana kufuatia kuendesha mambo yake mengi kwa kutegemea Wafadhili ambao wamepungua sana.

Kanisa sasa limeshajikabidhi mikononi mwa Serikali na Wakuu wa Serikali wanalitambua hilo.

Hata kwetu hapa Serikali ikiondoa ufadhili mfano wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Binafsi..TEC hawatamudu kuendesha SAUT kwa ufanisi nje ya kupandisha ada juu sana kufidia gepu la Wafadhili na kisha kukoswa Wanafunzi.

Hata Hospitali zao nyingi Teule na Rufaa kama Bugando Serikali ikijitoa na kuondoa ruzuku na kuwaachia TEC watazifunga.

Hii Taasisi kwa sasa ipo kijanja janja sana ila kiundani Uchumi ulishaporomoka hawana ubavu wa kutunishiana misuri na Serikali yoyote.

Mtu kama Trump ndiyo maana alimpa shit Papa baada ya kupigia kelele uvamizi wa Marekani kwa Irani.anajua hana lolote kwani Taasisi anayoiongoza iko taabani.

Vita ya kwanza ya Marekani na Iraq ya Sadam Hussein Papa Yohane Paul-II alienda kwa dharura Marekani kumuomba Bush Mkubwa asianzishe vita hiyo na siku hiyohiyo walipozungumza Usiku wake Bush akatoa amri ya Vita kuanza..

Hii ya hapa pia haishangazi..za akina Kitima zile ni kelele za Kihulka na binafsi tu siyo za Kitaasisi na hata wakubwa wake wakiambiwa wamdhibiti watatii.

Na hiki kikao ndiyo Mwisho wa kelele za Padri Kitima kwa Serikali.Hata Method Kilaini alitulizwa na akatulia.
Huwezi kuitwa ikuli ukagoma, ni ama uende na usimamie unachokiamini au uende usikilize, unyamaze ama kukubaliana na ulichoitiwa.

Uamuzi utabakia kwa aliyeitwa.
 
Huwezi kuitwa ikuli ukagoma, ni ama uende na usimamie unachokiamini au uende usikilize, unyamaze ama kukubaliana na ulichoitiwa.

Uamuzi utabakia kwa aliyeitwa.
Aliyeitwa hana maamuzi hapo, kila kitu atapangiwa na atatii
 
View attachment 3647791View attachment 3647792View attachment 3647793

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 10 Agosti, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference - TEC), Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na TEC na kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa yanayoigusa jamii, yakiwemo ya kisiasa, imani na maendeleo, pamoja na kuimarisha amani, mshikamano na kujenga mustakabali mwema wa Taifa.

Aidha, mazungumzo hayo yaligusia umuhimu wa nafasi ya madhehebu na Viongozi wa Dini katika kulea jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano, ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika ustawi na maendeleo endelevu ya Taifa.

Soma Pia: Rais Samia amefanya mazungumzo na Viongozi wa Vyama vya Siasa Ikulu Dar es Salaam

Mheshimiwa Rais aliwashukuru Maaskofu hao kwa kuona umuhimu wa kukutana na kujadiliana naye masuala yenye tija kwa Taifa na kuwahakikishia dhamira yake ya kuendeleza utamaduni wa kushauriana na kushirikisha Viongozi wa Dini na makundi mbalimbali katika jamii kuhusu masuala muhimu ya kitaifa kila inapohitajika.

View attachment 3647795
Anatafuta picha za kutuma kwa Mabeberu kuwazuga kuwa reconciliation inaendelea vizuri.
 
Naona Desert mission vs YUDA mission wamekutana!!

Baada ya kuchapana sanaaaa!

Mission bado mbichi sana hizi!!

Common wealth wanawapa nguvu sana desert mission au TEC,YUDA mission kila wakipanga zinavuja na juzi YUDA katumwa alopoke eti "SIWEZI JIUZULU HADI KATIBA MPYA IPATIKANE"

Ukiukataa upinzani walau wa kutengeneza unatengeneza mpasuko wa ndani kisayansi,yaani CCM mtandaao vs wenye CCM halisi a.k.a TEC au DEEP STATE!

Kazi na utu,tunasonga mbele!!
 
Wangekuwa wanamsimamo wangeitika ikulu?
Kitila alishambuliwa walifanya nini?
Mtu akishakuwa karibu na meza ya siasa ni walewale tu.
Hakuna dola duniani inatishika na watu nje ya mfumo.
Duh! Ulitaka wafanye Nini?.
 
Wakizingua Mafwele na CCM watateka TEC yote,Mashule, Hospital mpaka na Wanafunzi na Wagonjwa wote.

Hapo Kitima kabebwa na akina Nkwande...."..Ahiii!twende yakaishe..."tu..

Labda watumie vitisho vya kumuotesha ndoto za ajabu Samia..maana hiyo Teknolojia Wakatoliki wanayo...Mwezi mzima mfululizo awe anaota anacharaza kinanda na kupiga chetezo St Joseph Kanisani.Samia na yeye ajibu kwa Majini.kiumane..
Waambie wafanye hivyo. Shida yenu mnawaza kuumiza watu baadala ya maendeleo. Tangu mmeteka watu mpaka Leo mmefaidika na Nini? Zaidi ya deni la taifa kuongezeka.
 
Kweli kabisa. Sijui aliwaza Nini?
Siku zote watu wa mwilini wanaona nyayo za miguu yao zinapoishia.

Hawaamini kwamba kuna maisha baada ya maisha haya!. Ndio maana hata kuua ikibidi wapo tayari ili tu kuhangaika kuzishibisha nafsi zao zisizoshiba!.

MHUBIRI 1
7 Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.

8 Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.
 
Back
Top Bottom