Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 21,593
- 46,759
Yale yalikua maigizo, si unasemea wale kina Aisha, Mwajuma na kina Athumani waliojivika ukatoliki kwa muda.??Hivi zile hehaheka za jumuiya sijui gani, Kombo kwenda kuwashtaki TEC kwa papa, n.k zikiishia wapi?
Si kweli,mi najua hospital kubwa za katoliki ni mbili tu,bugando na ndanda/peramiho
Ohooo !Ooohooo...
Kumbe !Mwenzake Nchimbi kaenda kuonana na kikwete
Unataka awasikilize hao TEC ili atoke madarakani?.Degree za maana sasa zimeenda ikulu
Hopefully wamempa Mama madini ya kutosha, na hao ndio watu wa kuwasikiliza Sasa.
Siyo wale vichaa machawa wanaotishia kukata watu vichwa.
Atokaje madarakani wakati yeye ndiye Rais hadi 2030!?Unataka awasikilize hao TEC ili atoke madarakani?.
Akiwasikiliza TEC anatoka!. Labda awapuuze!. UKWELI,HAKI & UWAJIBIKAJI hautamuacha salama!Atokaje madarakani wakati yeye ndiye Rais hadi 2030!?
Watamshauri namna nzuri ya kufanyaAkiwasikiliza TEC anatoka!. Labda awapuuze!. UKWELI,HAKI & UWAJIBIKAJI hautamuacha salama!
Serikali ni wananchi ambao kwa asilimia kubwa hawaungi mkono huu uongozi uliopo..Movement anazofanya kitima sio za kitaasisi ni hulka zake tu, TEC Haina misuli ya Kuvuambiana na serikali
Tunapoongelea Maaskofu wa Katoliki, tunaongelea TEC! Akitokea Askofu mmoja akasema hayo maneno, huo unabakia kuwa mtazamo wake na siyo wa Kanisa. Haya nipe hapa huo waraka au tamko la TEC lilimtambua Kikwete kama chaguo la Mungu hiyo 2005.2005 hao wasomi wa falsafa walimuita jakaya 'chaguo la Mungu' na kauli nyingi za kichawa,alipokata maslahi yao waka-activate mfumo wao, propaganda dhidi ya jakaya zikaanza
Kanisa katoliki lilichangia anguko la USSR..Tec Ina nguvu kuliko serikali! Nguvu ya Tec huioni Wala haitumii mabomu ila 70% ya gvt work force Iko chini ya TEC Kuanzia walimu mpaka mainjinia wa tanesco jwtz Hadi tiss Sasa hao wote wakiamua liwalo na liwe gvt inaanguka hapo hapo.
Hakuna masikini anayelazimishwa kutoa sadaka. By the way RC ni taasisi inayojimudu. Tutoe tusitoe, bado wataishi maisha yao ya kawaida kabusa. Huo ndiyo ukweli. Hawana njaa kama wale masheikh wako ubwabwa wa bakwata.Wala na kusaza jasho la masikini kwa tozo(sadaka,zaka,fungu la kumi,ruzuku hazina)
Unatafsiri Kanisa kama nini,?Namuona hapo Nkwande amesinzia kabisa...
Itoshe tu kusema kwenye Dunia ya Sasa Umwamba wa Kanisa Katoliki Duniani umeshaporomoka sana kufuatia kuendesha mambo yake mengi kwa kutegemea Wafadhili ambao wamepungua sana.
Kanisa sasa limeshajikabidhi mikononi mwa Serikali na Wakuu wa Serikali wanalitambua hilo.
Hata kwetu hapa Serikali ikiondoa ufadhili mfano wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Binafsi..TEC hawatamudu kuendesha SAUT kwa ufanisi nje ya kupandisha ada juu sana kufidia gepu la Wafadhili na kisha kukoswa Wanafunzi.
Hata Hospitali zao nyingi Teule na Rufaa kama Bugando Serikali ikijitoa na kuondoa ruzuku na kuwaachia TEC watazifunga.
Hii Taasisi kwa sasa ipo kijanja janja sana ila kiundani Uchumi ulishaporomoka hawana ubavu wa kutunishiana misuri na Serikali yoyote.
Mtu kama Trump ndiyo maana alimpa shit Papa baada ya kupigia kelele uvamizi wa Marekani kwa Irani.anajua hana lolote kwani Taasisi anayoiongoza iko taabani.
Vita ya kwanza ya Marekani na Iraq ya Sadam Hussein Papa Yohane Paul-II alienda kwa dharura Marekani kumuomba Bush Mkubwa asianzishe vita hiyo na siku hiyohiyo walipozungumza Usiku wake Bush akatoa amri ya Vita kuanza..
Hii ya hapa pia haishangazi..za akina Kitima zile ni kelele za Kihulka na binafsi tu siyo za Kitaasisi na hata wakubwa wake wakiambiwa wamdhibiti watatii.
Na hiki kikao ndiyo Mwisho wa kelele za Padri Kitima kwa Serikali.Hata Method Kilaini alitulizwa na akatulia.
Wale kina Mwajuma, Sikuzani na wenzao wa Temeke Mikoroshoni? Think-tank ya CCM ndiyo ilitengeneza mkakati ule.Hivi zile hehaheka za jumuiya sijui gani, Kombo kwenda kuwashtaki TEC kwa papa, n.k zikiishia wapi?
Consolata Hospital Ikonda: Njombe