Mfano Rais ameambiwa Barabara ya Geita kwenda Kahama ni kms 58 na imewekwa kwenye Ilani ya ccm vipindi viwili na haijafanyiwa kazi hakujibu chochote...
Sh57 bilioni kupeleka umeme kwa wachimbaji Geita
Muktasari:
Wizara ya Nishati imetenga Sh57 bilioni kwa ajili ya kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu mkoani Geita.
Mwanza. Wizara ya Nishati imetenga Sh57 bilioni kwa ajili ya kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu mkoani Geita.
Akizungumza leo Jumamosi, Oktoba 10, 2022 kwenye mkutano wa hadhara unaofanyika katika viwanja vya Kalangalala mjini Geita, Waziri wa Nishati, January Makamba amesema huo ni mpango mahususi wa wizara hiyo kuwapelekea umeme wachimbaji hao wanaotumia majenereta katika utafutaji wa madini hayo.
“Tumetenga jumla ya Sh57 bilioni kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo, kati ya hizo Sh7 bilioni ni kupitia REA katika maeneo 39 na Sh50 bilioni ni za Tanesco kupeleka umeme katika maeneo ambayo wachimbaji wadogo wanahitaji,”amesema Makamba.
Amesema wamepeleka umeme mwingi (Megawati 90) mkoani Geita kuliko unaohitajika kwa sababu matumizi yatakua na umeme utakaohitajika miaka ijayo tayari utakuwepo.
“Sisi kama Wizara kwa muongozo na maelekezo yako tumeamua kuweka mkazi mahususi kwa kitu tunakiita gridi ya Magharibi.
“Yaani kwa upande wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na Magharibi kuwe na gridi yake mahususi ambapo tutajenga vituo vingi zaidi vya kupokea umeme, tutajenga njia nyingi zaidi za kusafirisha umeme na tutazalisha umeme mwingi katika mikoa hii,” amesema
Amesema kwa sasa mipango ya kuzalisha umeme katika mikoa hiyo ambayo ina fedha ni karibu megawati 400 ambapo gridi hiyo itakuwa inajitegemea ili yakitokea matatizo ya umeme eneo hilo lipate umeme wa kutosha.