Rais Samia amemaliza ziara ya Mkoa wa Geita bila kuruhusu wananchi kuuliza maswali?

Rais Samia amemaliza ziara ya Mkoa wa Geita bila kuruhusu wananchi kuuliza maswali?

Kero zao wapeleke kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ndiyo wawakilishi wa Rais
Kauli yako ni sawa umerudi nyumbani kutoka Safari, na hautaki watoto wakupe kero za hapo nyumbani kwa hoja kwamba wanapaswa kuwasilisha hoja zao kwa dada yao wa kazi kwa sababu tu yeye ndio umemuamini ahudumie watoto kwa niaba yako!!
 
Nimeona maajabu Mkoa wa Geita.

Kila Rais anakopita haruhusu wananchi watoe yaliyo moyoni mwao kwa nini?

Ukweli wananchi wana kero nyingi ambapo JPM alikuwa anawasikiliza na watu kuuliza sasa mikutano imekuwa kinyume.
Magufuli alikuwa anapenda uchonganishi, Dhulma, uonevu. Pia alikuwa mpenda sifa na alitatumia najukwaa haya kuwachonganisha watumishi wa umma na wananchi. Samia anafanya mambo kibusara na anajua matatizo ya kila sehemu apitayo
 
Samia hadi sasa hajajua bei Za kg moja ya maharagwe, mahindi na mchele ila angeruhusu wananchi waongee angelijua.
Viongozi wa ccm wamepiga kimya ila 2025 wataanza kuongea
 
JPM alikuwa hasikilizi kero bali ilikuwa inaandaliwa watu wanamuuliza maswali ya kutafutia kiki za kisiasa. Ilikuwa ikitokea bahati mbaya akauliza mtu ambaye hajapangwa, alikuwa anaishia kumkejeli na vitisho. Yale maigizo tulikuwa tunayoana.
Alikuwa bingwa wa Comedian sana.

Eti mtoto anaenda kumueleza kero ya shule.

Mara Babu kampelekea jogoo na yeye kamnunua.

Mara ananunua mahindi ya kuchoma kule Dumila, huku muuzaji akiwa na Bastola mfukoni.

na maigizo mengine mengi..
 
Huyu mama akiondoka madarakani utakuwa wa kwanza kumsema vibaya. Ccm mko kama Hali ya hewa
 
Ujinga ni kukosoa jambo kwa kufananiza na jambo la mtu bila kupima na kutambua hulka zinatofautiana na huo ndio huitwa unazi mambo tujalie kwa mtazamo wako kuwa kupokea kero mbele ya halaiki ndio solution ya kutatua matatizo hio sio kweli kwa sababu naweza kuleta visa kadhaa hapa ambavyo vilifikishwa kimlengo ule ule na mtu yule yule lakin yalishindwa kusolviwa ishu ni kwamba kila kiongozi ana mtazamo wake kwenye kuongoza cha kuzingatia katiba ndio kiranja kwake
 
Back
Top Bottom