Rais Samia amesema tuwe na jamii yenye ujasiri wa kuhoji

Rais Samia amesema tuwe na jamii yenye ujasiri wa kuhoji

Serikali yetu chini ya uongozi mahili na shupavu wa Rais samia ilipokea maoni ya watu na wadau wote na ikayafanyiaa kazi mawazo ya wote. Ndio maana wakati wote ilikuwa ikitoa maelezo katika lengo la kututoa hofu watanzania juu ya uwekezaji huo.
Tumbo lenye njaa huwa halikipi kichwa nafasi yake ya kufikiri.
UCHU WA MADARAKAA UNATUZIBA MACHO NA KUFUNGA AKILI ZETU
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hayo ni maneno ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,simba wa nyika, komandoo wa vita,nyota ya matumaini Mama Samia Suluhu Hasssan katika maazimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Ambapo amesema kuwa tunapaswa kuwa na jamii yenye ujasiri wa kuhoji.

Naungana na kumuunga mkono mh Rais katika hili hasa kwa vijana. Kauli hii ni kama ile ambayo imewahi kutolewa na Hayati Baba wa Taifa ambaye yeye alisema tunapaswa kuwa na vijana jeuri wenye ujasiri wa kuhoji na kuwahoji viongozi wao.

Rais Samia Ndio maana amefanikiwa kuongoza Taifa likiwa limetamalaki kwa amani na utulivu ,kwa kuwa ametoa nafasi ya watu kuhoji masuala mbalimbali yanayoendelea nchini au kufanyika au kufanywa na serikali yake na kuwapatia majibu stahiki.kwa hiyo watu wanakuwa hawana dukuduku wala vinyongo katika mioyo na vifua vyao ,kwa kuwa mambo yanayoleta maswali kwao yanapatiwa majibu kwa wakati sahihi na hivyo kuwafanya watu kuwa na taarifa na uelewa au ufahamu wa kila kitu hapa nchini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Yule mwandishi alimhoji Paul Makonda kuhusu tuhuma za Lissu kupigwa Makonda alijibuje?
Kamuulize ma…

Kijana mdogo alimuuliza swali mwenyekiti mpya mkoa wa Arusha mh. Sabaya alijibiwaje?
Kaa chini hilo sio swa…..


Wazari mkuu aliulizwa swali kuhusu alipo makamu wa rais alimjibuje yule muuliza swali?
Yupo kwenye ma…..

Huyo mama aache unafiki!
Kuhoji wanahoji sana shida ni majibu ni ya hovyo.
 
Yule mwandishi alimhoji Paul Makonda kuhusu tuhuma za Lissu kupigwa Makonda alijibuje?
Kamuulize ma…

Kijana mdogo alimuuliza swali mwenyekiti mpya mkoa wa Arusha mh. Sabaya alijibiwaje?
Kaa chini hilo sio swa…..


Wazari mkuu aliulizwa swali kuhusu alipo makamu wa rais alimjibuje yule muuliza swali?
Yupo kwenye ma…..

Huyo mama aache unafiki!
Kuhoji wanahoji sana shida ni majibu ni ya hovyo.
Hoja ni kuwa tuwe na jamii yenye ujasiri wa kuhoji mambo au vitu bila kujali aina ya majibu yatakayotolewa.
 
Umetumia vigezo gani kumpa hizo sifa,Na Tanzania bara ni nchi gani na ilipata uhuru kutoka kwa mkoloni gani.
 
Naomba tuwe jasiri na hodari katika harakati zetu za kujenga mustakabali bora kwa Tanzania. Heri ya Siku ya Uhuru kwa Watanzania wote!,”amesema.
Tunahitaji vijana wabishi nawene uwezo wa kuhoji, hao ndio wanaweza kulitetea Taifa lao. J K Nyerere
Leo hoji kitu chochote kuhusu Taifa lako uone kitakacho kukuta.
 
Rais anaongea km amekatwa kicha hafikilii
Watu kibao leo wamepotea kisa kutoa maoni af saiv anaongea pumba na mashavu yake
 
Kwenye suala la Bandari mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania na nyota ya matumaini mh mama Samia na Serikali yake walitoa uhuru wa kutosha kwa watu, taasisi,vyama na wadau mbalimbali kutoa maoni yao na mwisho serikali yetu ilifanyia kazi maoni na mawazo yote muhimu na kuja na mkataba bora kabisa kuwahi kushuhudiwa katika Taifa letu.ambao utachochea ufanisi wa bandari yetu hasa katika masuala ya mizigo pale bandarini ,ambapo sasa haitakuwa inakaa sana kama awali ambapo ilikuwa inaongeza gharama kwa wenye mizigo.

Chawa unakaz kwel kwel yan kusema tu Raisi unashindwa ad kuongezea uongo eti raisi mpendwa kipenzi cha wananch na nyota ya matumaini duuh kwel uchawa ni kipaji
 
Chawa unakaz kwel kwel yan kusema tu Raisi unashindwa ad kuongezea uongo eti raisi mpendwa kipenzi cha wananch na nyota ya matumaini duuh kwel uchawa ni kipaji
Nilichoandika ni sahihi kabisa maana Rais samia ndiye kiongozi anayependwa na kukubalika sana ndani ya nchi na ndani ya bara zima la Afrika kwa sasa.
 
Back
Top Bottom