Rais Samia ameshazidiwa na wapigaji suala la bei ya petroli?

Hopeless
 
The Boss,

Fuatilia bei ya mafuta kwenye soko la dunia, na utaona tangu mwezi wa 6 uanze, bei imekuwa ikipanda tu...

Kwa Zambia, siwezi kushangaa bei kuwa chini kwa sababu mwanzoni mwa mwaka huu kuna baadhi ya kodi waliziondoa kwa kampuni zinazoagiza mafuta!!

Sina uhakika na hiyo bei ya Rwanda ulikoitoa, lakini kwa mujibu wa mtandao wa Global Oil Price, inaonesha bei ya petrol Rwanda ipo juu tena pengine kuliko Tanzania.

Sipo Kenya, lakini kwa mujibu wa EWURA ya Kenya, bei ya petrol kwaMombasa ambayo tunaweza kuiweka kundi moja na Dar ipo KSH 124.72 ambayo ni zaidi ya Sh 2600 za Tanzania. Labda Manyan'au akina Tony254, Teargas, na MK254 waje ku-verify hizo bei za Kenya kutoka Energy & Petroleum Regulatory Authority ambapo inaonesha Nairobi, lita moja ya petrol (super) ni KSh. 127.14 ambazo ni takribani TSh. 2700/=

Je, wewe hizo bei umezitoa wapi?
 

 
 
Sahau
 
Watu wamepigia kelele sana kuhusu VAT wafanyabiashara wengi kwa sasa hawatoi receipt, mpaka iweje??? Pale mtaa wa Kongo wana bango la matangazo TRA lakini maduka ya jirani tu receipt yanazingua

Swala la kodi wafanya kazi wataendelea kuumia maana hawawezi kwepa kama business people...
 
Ulichoandika hapa Mkuu Boss ni sababu tosha ya kumkabili Maza na kupinga bajeti yake ambayo ina kodi kubwa sana kwa walipa kodi. Kama nchi zote zinanunua Petroli kutoka soko lile lile la iweje bei ya petroli nchini iwe kubwa sana kuliko nchi nyngine?
hao wanaojitapa wana master ya uchumi wametengeneza bajeti ya ovyo sasa hivi tutaona umeme soon utapanda
 
Kwani kipindi cha Magufuli bei ilikuwa shilingi ngapi kwa lita? Bei ilikuwa 2,200 hadi 2,100 ambapo bado ilikuwa juu zaidi ya Zambia na nchi jirani zinazopokelea mafuta kwenye bandari zetu.
Over 500tsh increment, mkuu ni parefu apo
 
Hii nchi inashangaza sana, mtu aliye straight utatungiwa kila aina ya uchafu lakini wakilenga kulinda issues zao tu
 
Wewe ndio wa hovyo kabisa!

Magu alikuata mafuta yanauzwa kati ya 1900 hadi 2100 na alimaintain bei isivuke 2200 kwa muda wake wa miaka yote 5

Hiyo bei yako ya 1200 ni ya Mkapa!

Ni suala la muda tu tutaelewana tu
Isije ikawa unakumbuka sana bei ya mafuta kwa mwaka 2020 ambapo kote duniani ilishuka kutokana na corona!! No one can control oil price unless nchi husika iwe imeondoa mzigo wa kodi kwa kampuni za uagizaji wa mafuta!

Kama bei wakati wa Magu ilikuwa chini basi ilitokana na bei ya mafuta soko la dunia kuwa chini! Kama alivyoshindwa ku-control bei ya korosho na mbaazi, pamoja na mazao mengine ndivyo ambavyo asingeweza ku-control bei ya mafuta!!

Kwahiyo hoja kwamba eti ali-maintain isivuke 2200, sio kweli bali soko la dunia ndilo lilifanya bei isivuke hapo! Kwa mfano, angalia hizi historical data za bei ya mafuta soko dunia kama zilivyotolewa Trading Economics:-



Utaona hapo bei 2020 kuna wakati ilishuka sana, but somewhere in 2018, bei ilikuwa juu kama ilivyo sasa, na ukiingia EWURA, utakuta wakati husika bei elekezi ilikuwa:-


Hapa ndipo ilipo hatari ya kuongeza kodi kwenye bidhaa muhimu kama mafuta!
 
Hata mafuta ya kula yamepanda.
 
Halafu mtu anajinasibu eti yeye Ni kama Magufuli tusiwe na wasiwasi! Na sisi wananchi tunaitikia Kwa Chorus: "Mama ameanza vizuri na amerudisha Furaha"! Hivi kauli zingine huwa tunatafakari au zinatutoka tu kama udenda wa mtoto mchanga?
Hovyo tu, alikuta mafuta shilingi elfu 1200 tu ikapaa mpaka 2200 kwa lita, saruji juu, mabati juu, mafuta ya kula juu

Sent from my Infinix X652 using JamiiForums mobile app
Wewe unaishi Tz peke yako? 2015 mafuta yalikuwa 1200?? Ukiacha kipindi ambacho dunia nzima yalishuka????
 

Mkuu hongera Kwa bandiko zuri!
Magu walikuwa wanamuogopa Kuliko...
Walikuwa hawathubutu kwa “Sababu yeyote kupandisha Bei” justification ya Kupanda bei ilikuwa ngumu mnoo kwa magu!
2.Mkuu kwanini Unafikiri TPDC watashindwa kuuza Mafuta Kwenye vituo vyao kama ulivyosema?nini Kitawazuia wakwame?
Au Hao big Oil companies?
 

Mkuu labda wanachukua tofauti na Kunapochukulia sisi[emoji3516][emoji12][emoji12]Au Gharama za Usafirishaji ni toka huko kuja bongo ni Tofauti na sisi!
Hope hatuagizi kwa pamoja
 

Unajua kodi mwaka huu imeongezeka kiasi gani kwenye kila lita ya mafuta? Tunalipa kodi mazee ili tujenge nchi. Ili wabunge wapate mishahara
 

Kwani hao Zambia tunaagiza Bulk wote kwa Pamoja?
Hii Vita ni Ngumu Mkuu...Alisikika Mmoja akisema vita ya Kiuchumi ni Ngumu kuliko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…