Rais Samia ameua Mhimili wa Bunge, bado kumalizia wa Mahakama. Haya si ya kushangilia

Umesema vyema. Huyu mama adhibitiwe kidogo. So far ana mema mengi kafanya ila ili la kushurutisha muhimili mwingine sio afya kwa demokrasia
Mengi ameyafanya kwa sababu ya mkopo huo wa Covid wa billion 10 kwa mpigo; hauwezekani kuwepo miaka yote minne iliyobaki na hata mitano itakayofuata. Hiyo ndiyo ilikuwa pointi ya ndugai kuwa ni lazima watu wakubali tozo; lakini dah! kuna mhimili na mhimili. Kuna mhimili wa chuma, mhimili wa zege na mhimili wa mbao.
pamoja na kuwa mama alilichochea sana kuliweka kwenye headline, tatizo kubwa limekuwa ni kwenye mihemko ya wana CCM wachumia tumbo. Nape aliyewahi kusema Bungeni apewe taarifa ya mikopo, sasa hivi hasemi lolote katika mkopo huu mkubwa kuliko yote iliyowahi kupokelewa katika historia ya nchi.
 
Hakuna unachoongea,alikuwa chama gani huyo aliyechana docs?

Uozo gani naotetea?
 
Hakuna unachoongea,alikuwa chama gani huyo aliyechana docs?

Uozo gani naotetea?
Uozo unaotetea ni ule wa yule shetani aliyetuharibia uwajibikaji wa mihimili ya utawala bora! Na sasa unaona ni haki mkuu wa mhimili wa serikali kukandamiza kiongozi wa mhimili wa bunge! Ni hatari sana!
 
Si mahakama Wala Bunge vilivyokuwepo, Jiwe ndio aliua kabisa huyu mama tuyamsingizia.

Spika alikuwa anaagizwa na Jiwe Kama Dc, eti deal nao hivyo hivyo b ungeni Wana immunity wakija huku nami nitawashughulikia.

Samia asionewe jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fact yenye uchungu
 
Mhimili wa Bunge uliuliwa tangu awamu ya 5 kwa bunge kuwa kibogoyo Mama anataka kulirudisha Bunge la Samuel Sitta
 
Achaaa:

Kwa hiyo mama hana analofanya kila kitu kielekezwe kwa mwingine? Au akifanya zuri ni lake baya ni la mwingine?
Mimi nasema zuri lake baya lake,
Ila kuna wanaosema baya lake zuri la aliyetangulia
Labda huko ndio ungeelekeza mawazo yako au swaki lako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…