Rais Samia ameua Mhimili wa Bunge, bado kumalizia wa Mahakama. Haya si ya kushangilia

Rais Samia ameua Mhimili wa Bunge, bado kumalizia wa Mahakama. Haya si ya kushangilia

Umesema vyema. Huyu mama adhibitiwe kidogo. So far ana mema mengi kafanya ila ili la kushurutisha muhimili mwingine sio afya kwa demokrasia
Mengi ameyafanya kwa sababu ya mkopo huo wa Covid wa billion 10 kwa mpigo; hauwezekani kuwepo miaka yote minne iliyobaki na hata mitano itakayofuata. Hiyo ndiyo ilikuwa pointi ya ndugai kuwa ni lazima watu wakubali tozo; lakini dah! kuna mhimili na mhimili. Kuna mhimili wa chuma, mhimili wa zege na mhimili wa mbao.
pamoja na kuwa mama alilichochea sana kuliweka kwenye headline, tatizo kubwa limekuwa ni kwenye mihemko ya wana CCM wachumia tumbo. Nape aliyewahi kusema Bungeni apewe taarifa ya mikopo, sasa hivi hasemi lolote katika mkopo huu mkubwa kuliko yote iliyowahi kupokelewa katika historia ya nchi.
 
Wewe acha kushabikia uozo kumbuka trump na yule mama spika wa senate? Yule mama alichanachana document ya Trump mbele ya Trump.
Hii ni precedent aliyoiacha yule muovu aliye kaburini na kusema mhimili mmoja umejichimbia zaidi. Siku mtakaposhtuka mtakuta Hang hire amehamishia kila kitu Zenj ndiyo mumuelewe Ndugai! na uovu wake.
Hakuna unachoongea,alikuwa chama gani huyo aliyechana docs?

Uozo gani naotetea?
 
Hakuna unachoongea,alikuwa chama gani huyo aliyechana docs?

Uozo gani naotetea?
Uozo unaotetea ni ule wa yule shetani aliyetuharibia uwajibikaji wa mihimili ya utawala bora! Na sasa unaona ni haki mkuu wa mhimili wa serikali kukandamiza kiongozi wa mhimili wa bunge! Ni hatari sana!
 
Si mahakama Wala Bunge vilivyokuwepo, Jiwe ndio aliua kabisa huyu mama tuyamsingizia.

Spika alikuwa anaagizwa na Jiwe Kama Dc, eti deal nao hivyo hivyo b ungeni Wana immunity wakija huku nami nitawashughulikia.

Samia asionewe jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilichofanyika kwenye uchaguzi mkuu uliopita ndiyo kuchonga mzinga huko na hata 2025 itakuwa hivyo hivyo ndiyo maana chief Hangaya anajiamini kupita maelezo kwani ameshaona kumbe inawezekana kabisa kupata kura za kishindo bila kupigiwa kura na wapiga kura.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Fact yenye uchungu
 
Mhimili wa Bunge uliuliwa tangu awamu ya 5 kwa bunge kuwa kibogoyo Mama anataka kulirudisha Bunge la Samuel Sitta
 
Achaaa:

Kwa hiyo mama hana analofanya kila kitu kielekezwe kwa mwingine? Au akifanya zuri ni lake baya ni la mwingine?
Mimi nasema zuri lake baya lake,
Ila kuna wanaosema baya lake zuri la aliyetangulia
Labda huko ndio ungeelekeza mawazo yako au swaki lako
 
Back
Top Bottom