Rais Samia amkabidhi nyumba Rais Mstaafu Kikwete
Mnajua kwanini mmeona picha ya funguo tu?
Hatuwezi kuwaonesha hilo bangaloo mtakufa hasira.

"Nyie mtaitikia kazi iendelee"
 
Mnajua kwanini mmeona picha ya funguo tu?
Hatuwezi kuwaonesha hilo bangaloo mtakufa hasira.

"Nyie mtaitikia kazi iendelee"
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni muhimu Rais mstaafu kuishi kwenye nyumba yenye hadhi ya U Rais mpaka yeye na mwenza wake watakapo tangulia mbele ya haki.

Hizi nyumba ziwepo hata 10 ikiwezekana.

Rais mstaafu akae humo akitaka. Asilazimishwe.

Sababu ni kwamba huko mbeleni inawezekana kabisa kuwapata watu kama Nyerere - wasiopenda kujitajirisha na mpaka ana staafu utakuta ana nyumba ya kawaida sana katika mitaa ya kawaida sana. Sasa akakae humo? Hapana. Huyu alikuwa Rais. lazima akae kwenye hadhi kubwa.

Lakin kila mmoja kumjengea ya kwake hapana aiseee. Utakuwa muendelezo ule ule wa matumizi mabaya ya hela kidogo tulizonazo
 
Mkiambiwa tupiganie Katiba mpya ooh machadema haya .sheria zikitekelezwa ooh inauma sana nyie vipi? Pumbavuu
Wabongo tuna shida sana.wakati wanasiasa wanajitengenezea mazingira mazuri ya wao kuneemeka kilaini sisi tuko busy kupiga umbea,majungu na ushabiki wa vyama na mipira inapofika muda wanasiasa wanajitekelezea kile ambacho walijitengenezea tunaanza kupiga kelele.Sisi tuna shida sio bure.
 
Mh.Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwanza hongera kwa kulitumikia Taifa kwa miaka 40 hadi unastaafu.ushauri wangu kwako ni kuwa usiwasikilize hawa wanaoshutumu kupewa nyumba na serikali yetu adhimu.

Ni haki yako na hawa wanaoandika mitandaoni ni watu ambao wanatumwa au wao wenyewe wanakushutumu kwa wivu wao.Pia wanajulikana kwako na kwetu kukuharibia sifa nzuri ulizonazo.

Wewe ni shujaa wa Watanzania.We tabasamu tu kama kawaida yako.Walishindwa na watashindwa.Nakuombea mwenyezi mungu akuepushe na hawa wanafiki na wazandiki na akupe maisha marefu inshaallah.
 
Pesa ya kununua magari ya zimamoto hakuna si kipaumbele lakini bilioni moja ya kujenga nyumba kwa asiyehitaji kujengewa nyumba na pesa za walipa kodi ipo!!!
 
Majizi yote haya hata aibu hayana.

Wanagawiana utajiri wa nchi hii kama Njugu.

Kikwete mwenye Lijumba lote lile Msoga ana shida gani ya nyumba?

Wanajitungia misheria ya kulipana mibenefits ya kufuru halafu tukiwauliza wanajitetea kwa sheria hizohizo!

Hiyo nyumba wala hajajengewa Kikwete bali ni urithi wa Riziwani, Miraji, Salama, Mama Salma na watoto wa Kikwete.

Mambo mengine ya nchi hii yanatia kinyaa ajabu.
 
Ajengewe ya pili wakati hayupo?
Samia kasema wanarekebisha sheria ili wajane nao wajengewe... yani marehemu Magufuli... as if hajawahi kupata nyumba ya serikali...

Mwafrika wa mwisho kutokea kujali wananchi wenzake na kutokuwa na tamaa ni marehemu Thomas Sankara
 
Back
Top Bottom