Profesa
Mohamed Yakub Janabi ni Mkurugenzi mtendaji wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu
Oktoba 2022 mpaka sasa. Kabla ya Hapo alikuwa Mkurugenzi mtendaji wa
Hospitali ya Jakaya Kikwete.
Mwaka
2005 alichaguliwa kuwa daktari binafsi wa
Rais mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Disemba 8 2024 ameteuliwa kuwa mshauri wa Raisi kwenye maswala ya afya, akiwa anaendelea na majukumu yake kama Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya taifa Muhimbili.
Elimu
Dkt. Janabi amepata kusoma katika vyuo mbali mbali ndani na nje ya Tanzania. Vyuo hivyo ni pamoja na:-
- Kharkov Medical Institute (Russia)
- Liverpool School of Tropical Medicine (England)
- University of Queensland Medical School (Australia)
- Graduate School of Medicine Osaka University Hospital (Japan)
- Bergen University (Norway)
NYONGEZA
MKURGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi, juzi aligeuka kivutio kijijini kwake Mtakanini, Kata ya Msindo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, ambako na timu yake ya wataalamu walikwenda kutoa huduma za afya.
Wananchi hao walifurahi kumwona mtoto wao ambaye ni maarufu kwa kutoa ushauri wa kutunza afya kwa kula vyakula vinavyofaa na umuhimu wa kufanya mazoezi, huku wakishukuru kwa uamuzi huo na kuomba muda zaidi kwa wataalamu kutoa huduma.
Daktari huyo bingwa ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ni mzaliwa wa kijiji hicho ambaye elimu yake ya msingi alianzia kijijini hapo.
Prof. Janabi alikwenda kuungana na madaktari bingwa watatu waliokuwa wakiendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wa moyo, kisukari, tezi dume na saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa gazeti hili, wananchi hao walisema wamefurahishwa na mtoto wa nyumbani kuwakumbuka na kutumia utaalamu wake na wenzake kwenda kuwasaidia.
“Tulimsubiri yeye na wataalamu wengine kwa hamu kubwa. Wamekaa nasi kwa wiki moja tunatamani wangeendelea kukaa nasi au kwenda kwenye vituo vingine. Tunatamani mpango huu uwe endelevu tupate alimu ya afya kama anavyotoa kwa wengine huko aliko,” alisema Cartas Nyoni.
“Profesa Janabi ni mwanetu, amekuja kwa muda mfupi tunatamani angekaa muda mrefu ili watu waelewe vizuri, tunawaomba wawe wanatutembelea wakiwa na vifaa vya kisasa kama walivyokuja navyo sasa. Wananchi wanyonge wamepata huduma vizuri na bure wangekwenda kwenye vituo vya afya, hospitali za rufani wangetozwa fedha nyingi, tunaomba huduma kama hizi kwa wananchi tunaoishi vijijini,” alisema.