Rais Samia amteua Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

Rais Samia amteua Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

Intelligence services do not like their officers to remain in one place indefinitely lest they become too comfortable, in the same way agent runners are ROTATED ,to ensure that they do not lose objectivity or end up too heavily invested in one case or a single spy,....Mwisho wa kunukuu
Sio kwa chini ya mwaka. Wakati huohuo intelligence services hazipendi kuwa na wastaafu wengi na watu wengi wanaotemwa nje. Zinapenda retention zaidi, ni gharama kulinda siri na kadri wanavyokuwa nazo wengi ndio risk inakuwa kubwa.

Btw the longest serving CIA Director, Allen Dulles anasemekana ndiye the best kuwahi tokea shirika hilo. Yuri Andropov pale KGB kapiga kazi nyingi ngumu na ndio kadumu muda mrefu.

FBI na predecessor agency yake ilikuwa na J. Edgar Hoover kaongoza miaka zaidi ya 40 na kuweka misingi imara sana. Hao unaosema wabadilishwe ni waliokuwa posted vituo vya kimataifa sio udowee uko uwe na michepuko na ujulikane.
 
Sio kwa chini ya mwaka. Wakati huohuo intelligence services hazipendi kuwa na wastaafu wengi na watu wengi wanaotemwa nje. Zinapenda retention zaidi, ni gharama kulinda siri na kadri wanavyokuwa nazo wengi ndio risk inakuwa kubwa...
Ndio hizi mambo tunahoji? TISS Sio ofisi ya DC Masasi
 
Kuna tatizo kubwa la katiba ndio maana unaona hizi reshuffle nyingine. Kenya nafasi kama hii ni mpaka bunge likupitishe kupitia open interview na raisi wa kenya anapelekewa majina halafu analiachia bunge lifanye due diligence.
Na bado wanavurugana
 
Hayawezi kuwa maamuzi yasiyo na ground..hofu haikosekan,nadhani alikua mzee sefue
Balozi hana umuhimu sana kwenye ujasusi pale embassy, hana umuhimu kuliko attaché wa intelligence services. Vilevile Balozi hana umuhimu kuliko military attaché kwenye mambo ya kijeshi pale ubalozini.

Balozi ni kioo, kila anapokwenda na anachofanya anajulikana kwenye hiyo nchi. Huwezi mkuta anapambana kukusanya data za siri au anasimamia kufanya recruitments za mole, double agent wala nini, wanakwepa kumpa majukumu hatarishi na ya kutia doa diplomasia ya nchi endapo atakamatwa au kujulikana. Hata Diwani au huyu Said uwape ubalozi kwa nchi zinazojielewa hawatishiki kwa lolote.

Mara kibao nchi zinafukuza wanadiplomasia wanausalama na zinawaacha mabalozi wao. Anaweza teuliwa daktari wa mifugo na ujasusi ukapigwa kuliko maelezo.
 
Sio kwa chini ya mwaka. Wakati huohuo intelligence services hazipendi kuwa na wastaafu wengi na watu wengi wanaotemwa nje. Zinapenda retention zaidi, ni gharama kulinda siri na kadri wanavyokuwa nazo wengi ndio risk inakuwa kubwa...
Na hoover alikuwa hapendwi na marais karibia wote waliokuwa mabosi zake . Maana alikuwa anajua dili chafu chafu za hao marais ndio maana inadaiwa alikuwa haguswi kwa kutumbuliwa.
 
Watu watengeneze mfumo kula hela, watu wasione hatari mkataba wa bandari, watu wasione hatari mijadala ya udini kwenye mambo ya kitaifa, watu wasigundue kujipenyeza kwa washindani kwenye mijadala ya ndani, nk nk nk. Bado ubaki na mkurugenzi!?
Wameonesha udhaifu mkubwa. Naipongeza serikali kwa kuona hilo na kuchukua hatua mapema.
 
Ninatafakari,
Mambo ni mengi lkn nguvu ya Taifa la Asili yangu ni kubwa Sana. TISS mna Uhakika na DG MPYA ?
Je, kufika alipo sio kazi nzuri ya Jirani?
Je, hajawa compromised akiwa Kigali ?
Je, hakuwahi pata mwanamke wa Kigali?
Je , mawasiliano yake muhimu na Biodata zake haziko Kigali,
Je, Udhaifu wake na uimara wake hauko Kigali ?
Tuna Uhakika gani ? DPW wana nguvu gani kwenye kumfikisha huyu hapa.

Kuhusu uwezekano wa DPWD KUWA NYUMA YA HUU UTEUZI

"Kati ya mwaka 2001 mpaka 2014, Balozi Mstaafu Ndugu Siwa alikuwa Afisa Mambo ya Nje, Mkuu katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Abu Dhabi iliyoko nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates); Moscow, nchini Urusi na baadaye Berlin, nchini Ujerumani"

Huyu DG Mpya Amefanya kazi na kujamiiana na hawa jamaa wawili wenye kiu na Rasilimali zetu Dubai na Kigali. Je, alikuwa smart kiasi cha sasa kuwakwepa? Au wanajua na wamemtuma kazi ?
Usiwe na shaka. Kagame mwenyewe ni zao la system yetu.
 
Na hoover alikuwa hapendwi na marais karibia wote waliokuwa mabosi zake . Maana alikuwa anajua dili chafu chafu za hao marais ndio maana inadaiwa alikuwa haguswi kwa kutumbuliwa.
Zile ndio nchi zenye mifumo. Mkurugenzi anateuliwa na Rais na anapitishwa na Bunge, Senator yeyote anaweza weka pingamizi na evidence juu ya uhalali, uaminifu, elimu, uwezo, uzalendo wa huyo mtu na akakataliwa. Hivyo Rais anaumiza kichwa kuteua sio kuchagua machawa. Mpaka sasa Joint Chiefs of Staff wa Marekani hawajatimia sababu kuna pingamizi.
Rais akitaka kufukuza Jenerali jeshini mpaka hilo jopo likubali na kesi juu ya mfukuzwa.

Hakuna mambo ya kubadilishwa kitengo. Ukikosea ni kesi kama ni jinai kisheria hamna mambo ya kusamehewa sijui kujitafakari.
 
Back
Top Bottom