Rais Samia amteua Dkt. Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)

Rais Samia amteua Dkt. Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)

Pia, alisema mchakato wa kuwapata wajumbe hao umefanywa ndani ya miaka mitatu.
Hivyo?

Hii kazi ngumu ya kuwapata hao wajumbe imefanyika kwa miaka mitatu?

Hawa watu watakuwa ni wa kipekee sana hawa. Ngoja tusubiri matokeo ya kazi ya watu muhimu kama hawa!

Namkumbuka "Abbas" wa Magufuli, kama yule 'comical Ally', wa Sadam, kumbe aliishia kwenye wizara ya Utalii?
 
RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk. Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbasi, alisema Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa naye, amewateua wajumbe sita wa bodi hiyo.

Aliwataja wajumbe hao niJacqueline Woiso, ambaye ni Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania, Tindi Mndolwa Mkuu wa Itifaki, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kitengo cha Diplomasia
na Said Kamugisha, ambaye ni Mtaalamu wa Masuala ya uhamiaji naMwanasheria.

Wajumbe wengine ni Omar Mohammed, ambaye ni Mkurugenzi wa Utaratibu na Usimamizi wa Utalii, kutoka Tume ya Utalii Zanzibar na Mdau wa Utalii Zanzibar, Mozza Salim Mauly ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Utali, inayojulikana kama Mauly Tours and Safari na Mdau wa Utalii Bara pamoja na Dk. Tereza Mugobi, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii na Mtaalamu wa Utalii.

Pia, alisema Damas Mfugale atakuwa Katibu wa Bodi hiyo ya Utalii, atakuwa na jukumu kubwa la kuwasimamia
wajumbe hao, kutekeleza majukumu yao ya kikazi.

Wakati huohuo, Waziri Mchengerwa alimthibitisha Dk. Tereza Mugobi, kuwa Mkurugenzi wa Idara ya
Utalii nchini, awali alikuwa anakaimu nafasi hiyo.

Waziri Mchengerwa ameteua wajumbe hao, kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 3(2) cha Sheria ya Bodi ya Utalii, Sura ya 364 kama ilivyorekebishwa na kifungu cha Sheria ya Mabadiliko ya Sheria mbalimbali namba 4 ya mwaka 2019. Pia, alisema mchakato wa kuwapata wajumbe hao umefanywa ndani ya miaka mitatu.
Yani huyu Dau fisadi na mwizi wa kutisha bado anakula shavu, sa100 ni janga
 
Wajumbe wengine ni Omar Mohammed, ambaye ni Mkurugenzi wa Utaratibu na Usimamizi wa Utalii, kutoka Tume ya Utalii Zanzibar na Mdau wa Utalii Zanzibar.
Tunarudi pale pale, Utalii na Maliasili ni jambo la Muungano? . Huyo Mzanzibar anaingia hapo kwa lipi?

Ni Mtanganyika gani anaingia Bodi ya Utalii Zanzibar?
Ikiwa hakuna kwanini Bodi ya Tanganyika itumike kama kitengo cha ajira kwa Wazanzibar.

Haya ndiyo mambo Wazanzibar wanalalamika kwamba tusiongeze mambo yasiyo ya muungano kinyemela.

Wazanziba wanataka 11 tu, sasa kuwateua kwenye bodi za mambo nje ya Muungano si kuwatendea haki

Tuheshimu malalamiko ya Wazanzibar akini pia nao kama wanataka HAKI hawanabudi kuheshimu na kuitenda HAKI.

Vipi wanalalamika kunyimwa haki halafu wanakubali kula haramu inayotokana na kunyimwa haki

Huu ndio unafiki wa Wazanzibar, Nguruwe haramu mchuzi wake halali.

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Tunaemfahamu Dau tunahisi kama hili ni jukumu dogo sana kwake.

Ningetamani sana Dau apewe majukumu makubwa na mazito zaidi, lakini naamini Rais anaelewa anachokifanya. Dau ni trouble shooter mzuri sana na bila shaka jukumu hili halitamzuia kufanya mengine mengi zaidi.
 
Tunarudi pale pale, Utalii na Maliasili ni jambo la Muungano? . Huyo Mzanzibar anaingia hapo kwa lipi?

JokaKuu Pascal Mayalla
Mkuu Nguruvi3, kwanza nani kakudanganya Dr. Dau ni Mzanzibari?. Mkuu Maalim Mohamed Said naomba atusaidie hapa!.

Pili hata ikitokea kweli ni Mzanzibari, Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye uraia mmoja tuu, uraia wa JMT, ambapo raia wote wa JMT kutoka pande zote za muungano, wana haki sawa, kwenye uraia hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari, wote ni Watanzania na wote ni sawa na wana haki sawa!.

Ila japo Tanzania ni nchi moja ya JMT, lakini ina sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Hii Tanzania Zanzibar is an archipelago yenye utawala wake wa ndani, ambao umeweka restrictions kwa mambo ya Zanzibar sio kwa Watanzania wote, bali ni kwa wale Watanzania wenye ukaazi wa Zanzibar pekee.

Nawashauri msipigie sana kelele jambo hili, tumeshauri tuwe ni nchi moja yenye serikali moja na rais mmoja, hivyo restrictions zitakwisha!, Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
P
 
Mkuu Nguruvi3, kwanza nani kakudanganya Dr. Dau ni Mzanzibari?. Mkuu Maalim Mohamed Said naomba atusaidie hapa!.
Soijamuongelea Ramadhan Dau, nimemuongelea huyo Mzanzibar kwa jina la Omar Mohamed ambaye ni Mkurugenzi wa Uratibu kutoka Tume ya Utalii Zanzibar. Rudia kusoma vizuri nukuu yangu ipo clear.

Nadhani ima hukusoma bandiko langu vizuri au umelisoma na unakusudia ku mislead wasomaji.
Bandiko la msingi limemueleza nani Omar Mohamed, na nimenukuu sehemu hiyo tu.

Pili hata ikitokea kweli ni Mzanzibari, Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye uraia mmoja tuu, uraia wa JMT, ambapo raia wote wa JMT kutoka pande zote za muungano, wana haki sawa, kwenye uraia hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari, wote ni Watanzania na wote ni sawa na wana haki sawa!.
Omar Mohamed ni Mzanzibar, rudia kusoma bandiko la msingi na nukuu yangu kwanza.
Hatuongelei Urai, tunaongelea mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano

Wazanzibar wana bodi ya Utalii na mambo ya utalii na maliasili si ya Muungano

Wazanzibar hawataki mambo kuongezwa kinyemela, kumteua Mzanzibar kwa kazi za Tanganyika si kuwatendea haki. Kumteua Mzanzibar kunafanya TTB kuwa jambo la Muungano, Wazanzibar hawataki.

Tuwatendee haki, waondolewe katika mambo yasiyo ya Muungano, hayawahusu kama walivyosema Bandari haiwahusu.

Watuachie yetu wahangaike na yao. Kama unadhani nakosema Muulize OMO na ACT Wazalendo jinsi wanavyoichukia Tanganyika na mitusi yao.

Waacheni Wazanzibar wafanye yao, Tanganyika si shamba la ajira ni nchi inayohitaji watu wenye uchungu nayo.
Ila japo Tanzania ni nchi moja ya JMT, lakini ina sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Hii Tanzania Zanzibar is an archipelago yenye utawala wake wa ndani, ambao umeweka restrictions kwa mambo ya Zanzibar sio kwa Watanzania wote, bali ni kwa wale Watanzania wenye ukaazi wa Zanzibar pekee.
Hakuna Tanzania Bara, kuna Tanganyika kwa mujibu wa Katiba ya 1977.

Ikiwa kuna Tanzania Bara, Tanzania visiwani ipo wapi? Katiba ya Zanzibar ya 1984 iliyorekebishwa 2010 inastambua Tanzania kama nchi iliyoundwa na Tanganyika na Zanzibar.

Wazanzibar hawataki Utanzania, wanataka Uzanzibar. Wanataka Utanzania pale tu penye mafao.

Nawashauri msipigie sana kelele jambo hili, tumeshauri tuwe ni nchi moja yenye serikali moja na rais mmoja, hivyo restrictions zitakwisha!.
P
Tanganyika mbona inarudi ! hakuna jinsi itarudi tena mapema sana.

Hoja ya Msingi ni kuwatendea haki Wazanzibar kwa kuwaondoa katika mambo yasiyo ya muungano.

Lakini pia ya Muungano wapewe ajira 21% na walipe ajira hizo kwa kodi za Zanzibar.

Wanapodai 21% wanadai haki, lakini haki inakuja na wajibu ambao ni kulipa hao 21%.

Unafiki wa Wazanzibar kuomba nafasi wasizotaka kuzilipia. Wanataka Wabunge hawawezi kuwalipia.

Wanataka teuzi hawana mchango hazina! Haki inaambatana na wajibu, tunataka kuwaona wanawajibiika.

OMO, Jussa na ACT wanatukana Watanganyika,waacheni Wazanzibar! Hatuna upungufu wa Watanganyika wenye uwezo na uchungu na Taifa lao. Wazanzibar hawataki Muungano waacheni msiwalazimishe teuzi
 
Soijamuongelea Ramadhan Dau, nimemuongelea huyo Mzanzibar kwa jina la Omar Mohamed ambaye ni Mkurugenzi wa Uratibu kutoka Tume ya Utalii Zanzibar. Rudia kusoma vizuri nukuu yangu ipo clear.
Sorry
Nadhani ima hukusoma bandiko langu vizuri au umelisoma na unakusudia ku mislead wasomaji.
Bandiko la msingi limemueleza nani Omar Mohamed, na nimenukuu sehemu hiyo tu.
Sorry
Omar Mohamed ni Mzanzibar, rudia kusoma bandiko la msingi na nukuu yangu kwanza.
Hatuongelei Urai, tunaongelea mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano
Naendelea kusisitiza Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu wa Tanzania!. Kila Mtanzania, regardless ni M-bara au Mzanzibari ana haki zote sawa za Utanzania ikiwemo kuteuliwa popote.
Wazanzibar wana bodi ya Utalii na mambo ya utalii na maliasili si ya Muungano
Sawa
Wazanzibar hawataki mambo kuongezwa kinyemela, kumteua Mzanzibar kwa kazi za Tanganyika si kuwatendea haki. Kumteua Mzanzibar kunafanya TTB kuwa jambo la Muungano, Wazanzibar hawataki.
Mbona tunakywa wazito hivi kulielewa hili jambo dogo hivi, Wanzanzibari wana haki zote za Utanzania ikiwemo kuteuliwa kushika nafasi yoyote ndani ya JMT kwa Utanzania wao!.
Tuwatendee haki, waondolewe katika mambo yasiyo ya Muungano, hayawahusu kama walivyosema Bandari haiwahusu.
Kama Wazanzibari ni Watanzania, mambo yote ya Tanzania hayawahusu kwa Utanzania wao
Watuachie yetu wahangaike na yao.
Uraia wa JMT ni mmoja tuu, hakuna yetu ila kuna yao!. Yetu yote ni ya wote maana ni Watanzania, ila yao ndio sio ya wote, yao ni ya Wazanzibari tuu pekee!.
Kama unadhani nakosema Muulize OMO na ACT Wazalendo jinsi wanavyoichukia Tanganyika na mitusi yao.
OMO ni issue kama alivyo Lissu!. Niliwahi kushauri Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii ila alipoingia GNU, nikampigia chapuo la 2025 apewe Zanzibar, Dr. aje huku, Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke humo nilisema
, hivyo hata saa hizi ninapoandika hapa, usikute huyu jamaa wala hajajijua kuwa yeye ndiye anapaswa aje awe rais ajaye wa Zanzibar!. Hii nibkufuatia dhulma kubwa iliyokuwa ikifanyika Zanzibar kwa miaka na miaka, Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda lakini sasa kwavile Samia ni mpenda haki, msema haki na mtenda haki, for the first time in Zanzibar tangu baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 12, 1964, uchaguzi wa 2025 unaweza kuwatendea haki!.

Waacheni Wazanzibar wafanye yao na Tanganyika si shamba la ajira ni nchi inayohitaji watu wenye uchungu nayo.
Kwenye uraia wa Tanzania, hakuna Wanzanzibari, kuna Watanzania tuu na wote wana haki sawa!.
Hakuna Tanzania Bara, kuna Tanganyika kwa mujibu wa Katiba ya 1977. Ikiwa kuna Tanzania Bara, Tanzania visiwani ipo wapi?
Sorry on this, hakuna Tanganyika, kuna Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Tanzania Visiwani ni ile iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Katiba ya Zanzibar ya 1984 iliyorekebishwa 2010 inastambua Tanzania kama nchi iliyoundwa na Tanganyika na Zanzibar.
Ni kweli ila katiba ya Tanzania, haiyatambui mabadiliko hayo ya katiba ya Zanzibar.
Wazanzibar hawataki Utanzania, wanataka Uzanzibar. Wanataka Utanzania pale tu penye mafao.
Ni haki yao.
Tanganyika mbona inarudi ! hakuna jinsi itarudi tena mapema sana.
Wish you all the best, ila utasubiri sana!, au utangoja sana!.
Hoja ya Msingi ni kuwatendea haki Wazanzibar kwa kuwaondoa katika mambo yasiyo ya muungano.
Huku ni kutaka kuwabagua, Wazanzibari kama Watanzania wana haki zote za Utanzania!.
Lakini pia ya Muungano wapewe ajira 21% na walipe ajira hizo kwa kodi za Zanzibar. Wanapodai 21% wanadai haki, lakini haki inakuja na wajibu ambao ni kulipa hao 21%.
Hili litatibiwa na serikali moja!.
Unafiki wa Wazanzibar kuomba nafasi wasizotaka kuzilipia. Wanataka Wabunge hawawezi kuwalipia. Wanataka teuzi hawana mchango hazina! Haki inaambatana na wajibu, tunataka kuwaona wanawajibiika.
Serikali moja itamaliza hili.
OMO, Jussa na ACT wanatukana Watanganyika, sasa waacheni Wazanzibar!
Hatuna upungufu wa Watanganyika wenye uwezo
Nasisitiza, kwenye uraia, hakuna Watanganyika wala Wanzanzibari tuna Watanzania na wote wana haki sawa!.
P
 
Diuu gorofa lake linamfikirisha sana floor zaidi 15 sio mchezo acha ajikombe .....safari zbar zilikuwa nyingi sanaaaa.....matokeo ndio haya
 
Back
Top Bottom