Rais Samia amteua Dkt. Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)

Rais Samia amteua Dkt. Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk. Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbasi, alisema Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa naye, amewateua wajumbe sita wa bodi hiyo.

Aliwataja wajumbe hao niJacqueline Woiso, ambaye ni Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania, Tindi Mndolwa Mkuu wa Itifaki, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kitengo cha Diplomasia
na Said Kamugisha, ambaye ni Mtaalamu wa Masuala ya uhamiaji naMwanasheria.

Wajumbe wengine ni Omar Mohammed, ambaye ni Mkurugenzi wa Utaratibu na Usimamizi wa Utalii, kutoka Tume ya Utalii Zanzibar na Mdau wa Utalii Zanzibar, Mozza Salim Mauly ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Utali, inayojulikana kama Mauly Tours and Safari na Mdau wa Utalii Bara pamoja na Dk. Tereza Mugobi, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii na Mtaalamu wa Utalii.

Pia, alisema Damas Mfugale atakuwa Katibu wa Bodi hiyo ya Utalii, atakuwa na jukumu kubwa la kuwasimamia
wajumbe hao, kutekeleza majukumu yao ya kikazi.

Wakati huohuo, Waziri Mchengerwa alimthibitisha Dk. Tereza Mugobi, kuwa Mkurugenzi wa Idara ya
Utalii nchini, awali alikuwa anakaimu nafasi hiyo.

Waziri Mchengerwa ameteua wajumbe hao, kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 3(2) cha Sheria ya Bodi ya Utalii, Sura ya 364 kama ilivyorekebishwa na kifungu cha Sheria ya Mabadiliko ya Sheria mbalimbali namba 4 ya mwaka 2019. Pia, alisema mchakato wa kuwapata wajumbe hao umefanywa ndani ya miaka mitatu.
Inqleta tafsiri fani kurundikia mtu mmojq vyeo lukuki.

Hongera zake
 
Tunarudi pale pale, Utalii na Maliasili ni jambo la Muungano? . Huyo Mzanzibar anaingia hapo kwa lipi?

Ni Mtanganyika gani anaingia Bodi ya Utalii Zanzibar?
Ikiwa hakuna kwanini Bodi ya Tanganyika itumike kama kitengo cha ajira kwa Wazanzibar.

Haya ndiyo mambo Wazanzibar wanalalamika kwamba tusiongeze mambo yasiyo ya muungano kinyemela.

Wazanziba wanataka 11 tu, sasa kuwateua kwenye bodi za mambo nje ya Muungano si kuwatendea haki

Tuheshimu malalamiko ya Wazanzibar akini pia nao kama wanataka HAKI hawanabudi kuheshimu na kuitenda HAKI.

Vipi wanalalamika kunyimwa haki halafu wanakubali kula haramu inayotokana na kunyimwa haki

Huu ndio unafiki wa Wazanzibar, Nguruwe haramu mchuzi wake halali.

JokaKuu Pascal Mayalla
Tatizo ni mfumo wenyewe wa Muungano hauna tafsiri sahihi umevifanya vya Tanganyika vyote viwe vya muungano
 
Mkuu Nguruvi3, kwanza nani kakudanganya Dr. Dau ni Mzanzibari?. Mkuu Maalim Mohamed Said naomba atusaidie hapa!.

Pili hata ikitokea kweli ni Mzanzibari, Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye uraia mmoja tuu, uraia wa JMT, ambapo raia wote wa JMT kutoka pande zote za muungano, wana haki sawa, kwenye uraia hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari, wote ni Watanzania na wote ni sawa na wana haki sawa!.

Ila japo Tanzania ni nchi moja ya JMT, lakini ina sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar. Hii Tanzania Zanzibar is an archipelago yenye utawala wake wa ndani, ambao umeweka restrictions kwa mambo ya Zanzibar sio kwa Watanzania wote, bali ni kwa wale Watanzania wenye ukaazi wa Zanzibar pekee.

Nawashauri msipigie sana kelele jambo hili, tumeshauri tuwe ni nchi moja yenye serikali moja na rais mmoja, hivyo restrictions zitakwisha!, Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
P
Hilo la serikali moja ni gumu kutekelezeka maana Wazanzibari hawatokubali
 
Kwa hasara kubwa ya mabilioni ya yale magorofa pale kigamboni yeye akiwa CEO wa NSSF,asingefikiriwa kuteuliwa kwenye utumishi wa Umma kamwe abadan!

Actually alipaswa kuwajibishwa kwa hasara zile!
 
Wanatumia ujinga wa wadangika wengi kama Mtaji wa kufanya watakavyo lakini Mwenyezi Mungu kuna namna ataingilia kati ipo siku ! InshaAllah!

Mwenyezi Mungu anaona kila kitu vya wazi na sirini.

Mwenyezi Mungu anajua kuichunguza mioyo ya Wanadamu na kujua mawazo yao na hila zote na kila uovu.
 
Hiyo TTB yenyewe haijawai kuwa na ufanisi, utalii unakuwa kwa mwendo wa kinyonga hakuna ubunifu na wala hatutarajii mpya kutokana na hizo Teuzi, hofu ni wanyama wetu na maliasili kwa ujumla.....
 
Kuna mwaka walitangaza kazi nssf wakati tunapeleka cv zetu pale, nikaona mlinzi anaongea na binti aliyekuwa mbele yangu huku akiwa amefunua nyalaka zake akamwambia "dada hizi passport zako ungevaa hata ushungi, yaani wakiona pocha iko wazi hivi hawataweza shughulika na doc zako" kiukweli niliumia sana. Wakati wa huyu bwana was like kazi walikuwa wanapeana misikitini.
Hawa jamaa hawapaswi kupewa madaraka makubwa;huwa hawajui kutofautisha shughuli za serikali na msikiti!
 
Hivyo?

Hii kazi ngumu ya kuwapata hao wajumbe imefanyika kwa miaka mitatu?

Hawa watu watakuwa ni wa kipekee sana hawa. Ngoja tusubiri matokeo ya kazi ya watu muhimu kama hawa!

Namkumbuka "Abbas" wa Magufuli, kama yule 'comical Ally', wa Sadam, kumbe aliishia kwenye wizara ya Utalii?
Wahuni tu,sema udini ndiyo unawasumbua!
 
Vijana acheni kusambaza CV mjini bila connection hakuna kitu, utajitolea bure huku mchana unashinda njaa wenzako wanaenda kula wèwe unaanza kucheza magemu na kujifanya unaongea na simu za uongo
Mwambie Lucas Mwashambwa kila siku anatujazia magazeti ya kumsifia Rais Samia na chini anaweka namba ya simu
 
Back
Top Bottom