Rais Samia amteua Dkt. Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)

Rais Samia amteua Dkt. Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)

Kuna watu exposure inawabeba sana akiwemo Dr Dau na Mchechu, ni vile Siasa inafifisha juhudi zao wakati mwingine.

Kila la kheri Balozi kwenye Majukumu yako mapya, ni muhimu kutumia uzoefu wako uliopata huko Duniani kuja kuifanya Benki ya TIB kuendana na soko la Sasa
 
Tatizo ni mfumo wenyewe wa Muungano hauna tafsiri sahihi umevifanya vya Tanganyika vyote viwe vya muungano
Nyerere ndiyo alitaka iwe hivyo ili atumie loopholes hizo kwa Tanganyika kuimeza Zanzibar...luckily Karume senior alishtuka mapema. Lukuvi said it all katika ile famous video clip.
 
RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk. Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbasi, alisema Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa naye, amewateua wajumbe sita wa bodi hiyo. Aliwataja wajumbe hao niJacqueline Woiso, ambaye ni Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania, Tindi Mndolwa Mkuu wa Itifaki, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kitengo cha Diplomasia na Said Kamugisha, ambaye ni Mtaalamu wa Masuala ya uhamiaji naMwanasheria. Wajumbe wengine ni Omar Mohammed, ambaye ni Mkurugenzi wa Utaratibu na Usimamizi wa Utalii, kutoka Tume ya Utalii Zanzibar na Mdau wa Utalii Zanzibar, Mozza Salim Mauly ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Utali, inayojulikana kama Mauly Tours and Safari na Mdau wa Utalii Bara pamoja na Dk. Tereza Mugobi, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii na Mtaalamu wa Utalii. Pia, alisema Damas Mfugale atakuwa Katibu wa Bodi hiyo ya Utalii, atakuwa na jukumu kubwa la kuwasimamia wajumbe hao, kutekeleza majukumu yao ya kikazi. Wakati huohuo, Waziri Mchengerwa alimthibitisha Dk. Tereza Mugobi, kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utalii nchini, awali alikuwa anakaimu nafasi hiyo. Waziri Mchengerwa ameteua wajumbe hao, kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 3(2) cha Sheria ya Bodi ya Utalii, Sura ya 364 kama ilivyorekebishwa na kifungu cha Sheria ya Mabadiliko ya Sheria mbalimbali namba 4 ya mwaka 2019. Pia, alisema mchakato wa kuwapata wajumbe hao umefanywa ndani ya miaka mitatu.
Mkajenge vyoo vya dharura haraka pale kwenye vyoo vya njia ya oldvai NCAA ni aibu wageni kupanga foleni kupeana zamu ya kujisaidia kwenye matatundu mawili na wengine hulazimika kujisaidia nje na watoto wao!

BARABARA ZA ZA SERENGETI NI KIMEO KWA SASA chacharikeni!
 
Tunaemfahamu Dau tunahisi kama hili ni jukumu dogo sana kwake.

Ningetamani sana Dau apewe majukumu makubwa na mazito zaidi, lakini naamini Rais anaelewa anachokifanya. Dau ni trouble shooter mzuri sana na bila shaka jukumu hili halitamzuia kufanya mengine mengi zaidi.
Ki ukweli Dr. Dau ilitakiwa apewe zaidi ya kishirika kidogo kama hiko.
 
Kila CEO na mazuri na mapungufu yake, Hata kwa Dau pia alikuwa na mapungufu ila zaidi siasa tu ndio ambazo huwa sinaweza kuchafua jina la mtu ila kiutendaji Dr. Dau bado ni the best katika Management na kutoa results.

Ni sawa na miamba kama Lawrence Mafuru, Nehemia Mchechu wote hawa ni vichwa hasa katika masuala ya Management.

Exoosure na Experience ndo vinafanya watu kama hawa na Dr Dau waendelee kuaminiwa katika kila awamu, tusichukie hebu tujifunze qualities zinazowafanya wawe hapo juu walipo.
 
RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk. Ramadhan Dau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbasi, alisema Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa naye, amewateua wajumbe sita wa bodi hiyo.

Aliwataja wajumbe hao niJacqueline Woiso, ambaye ni Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania, Tindi Mndolwa Mkuu wa Itifaki, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kitengo cha Diplomasia
na Said Kamugisha, ambaye ni Mtaalamu wa Masuala ya uhamiaji naMwanasheria.

Wajumbe wengine ni Omar Mohammed, ambaye ni Mkurugenzi wa Utaratibu na Usimamizi wa Utalii, kutoka Tume ya Utalii Zanzibar na Mdau wa Utalii Zanzibar, Mozza Salim Mauly ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Utali, inayojulikana kama Mauly Tours and Safari na Mdau wa Utalii Bara pamoja na Dk. Tereza Mugobi, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii na Mtaalamu wa Utalii.

Pia, alisema Damas Mfugale atakuwa Katibu wa Bodi hiyo ya Utalii, atakuwa na jukumu kubwa la kuwasimamia
wajumbe hao, kutekeleza majukumu yao ya kikazi.

Wakati huohuo, Waziri Mchengerwa alimthibitisha Dk. Tereza Mugobi, kuwa Mkurugenzi wa Idara ya
Utalii nchini, awali alikuwa anakaimu nafasi hiyo.

Waziri Mchengerwa ameteua wajumbe hao, kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 3(2) cha Sheria ya Bodi ya Utalii, Sura ya 364 kama ilivyorekebishwa na kifungu cha Sheria ya Mabadiliko ya Sheria mbalimbali namba 4 ya mwaka 2019. Pia, alisema mchakato wa kuwapata wajumbe hao umefanywa ndani ya miaka mitatu.
Huyu si ndiye alikuwa mkurugenzi mkuu wa NSSF halafu alifanya ubadhirifu huko wa kufa mtu!!! au?
 
Back
Top Bottom