Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

inaonyesha ni mapendekezo ya mstaafu mabeyo kwa raisi ndio maana kupandishwa cheo na hapo hapo kuwa mkuu wa majeshi.

navofahamu jeshi kunarekodi zinazoweza kukubeba kutokana na ukaribu wa ngazi kubwa ndani ya jeshi
 
huwa sipendi kusikia Mkuu wa Majeshi anaitwa "Afande...Mkuu wa Majeshi" sielewi hili neno "afande" ni sahihi kulitumia kwa wenye vyeo vya juu?!

kwa uelewa wangu nilidhani kwa vyeo vya juu anatakiwa kuitwa "kamanda".
naomba ufafanuzi kwa wenye kujua maana huwa nahisi kumuita "afande" ni kama kudunisha cheo chake.
wataalamu naomba mtusaidie hapo.
upande wa polisi uko sahihi yaani kuanzia RPC wanatumia neno KAMANDA..... Upande huu wote ni maafande
 
Uteuzi mzuri wenye dalili za kuijibu hii hoja, Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu?. Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine? Tangu kuanzishwa kwake JWTZ mwaka 1964, baada ya Luteni Generali mmoja tuu mwenye jina la Abdalah, ambaye alikuja kuwa CDF, leo ndio Luteni Generali wa mwingine mwenye jina la Salumu ameteuliwa, akiwa ndie Mzanzibari wa kwanza kufikia cheo hicho, na hivyo kuweka a possibility ya Tanzania kuja kupata CDF kutoka upande wa pili wa Muungano in future.
NB. Naomba kuweka caveats ya kutuhumiwa mbaguzi, makabila na mdini, amini usiamini my concern were bonafide genuine kuuliza mbona ma CDF wote ni kutoka upande mmoja na dini moja?. Unaweza kukuta no one noticed anything mpaka baada ya concern, ndio watu wakajiuliza, hivyo ikabidi kaji affirmative action kafanyike kumuondoa Luteni Generali aliyefuata kwenye normal progression ya kuja kuwa CDF, ili to create a room ya mtu wa kwanza wa upande wa pili naye aweze kuwa Luteni Generali!. Na kwa faida ya wanajukwa hili Pasco Mayalla kabla ya kuwa mtangazaji wa RTD, alipitia JKT Makotupora na MMJKT, kisha akajiunga straight na JWTZ Airwing na kuajiriwa with MT. Number, na sasa ni askari wa akiba, ikitangazwa vita sisi ndio tunatangulizwa mbele ili tuwe chambo.
P
naunga mkono hoja yako kwa masilahi ya kujenga taifa imara na lenye uzalendo lazima pawepo na UWIANO sio tu kwenye nafasi moja moja bali ifanyike katika kila idara zote za Serikali.

Endapo tutafanya uwiano sawia ktk kila idara za Serikali basi Taifa letu litakuwa Imara kwa muda mrefu zaidi, sio sahihi kila miaka tunasikia watu wa dini fulani wanaishi wame kuwa marginalized wakati wanazo sifa zote za kitaaluma jambo hilo ni hatari kwa mustakbali wa Nchi yetu.

Awamu hii ya 6 imeliona hilo na sasa inalifanyia kazi hivyo ni vyema pia Idara zote za Serikali zikazingatia hilo kwa maslahi ya Nchi. Nchi imara lazima ijengwe na watanzania wote sio aina moja ya watu halafu wengine wakajiona hawana nafasi ya kulijenga taifa lao..hilo ni jambo hatari sana.

Nchi yetu itajengwa na watanzania wote kwa pamoja sio kundi au aina moja ya watu.
 
naunga mkono hoja yako kwa masilahi ya kujenga taifa imara na lenye uzalendo lazima pawepo na UWIANO sio tu kwenye nafasi moja moja bali ifanyike katika kila idara zote za Serikali.

Endapo tutafanya uwiano sawia ktk kila idara za Serikali basi Taifa letu litakuwa Imara kwa muda mrefu zaidi, sio sahihi kila miaka tunasikia watu wa dini fulani wanaishi wame kuwa marginalized jambo hilo ni hatari kwa mustakbali wa Nchi yetu.

Awamu hii ya 6 imeliona hilo na sasa inalifanyia kazi hivyo ni vyema pia Idara zote za Serikali zikazingatia hilo kwa maslahi ya Nchi. Nchi imara lazima ijengwe na watanzania wote sio aina moja ya watu halafu wengine wakajiona hawana nafasi ya kulijenga taifa lao..hilo ni jambo hatari sana.

Nchi yetu itajengwa na watanzania wote kwa pamoja sio kundi au aina moja ya watu.
Kwahiyo watu wasiteuliwe kwa uwezo iwe kwa uwiano wa dini? shame on you
 
Taarifa inaeleza kwamba Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, ili kuziba pengo lililoachwa na na Venance Mabeyo anayestaafu kwa mujibu wa Sheria.

Kwangu mimi General Mkunda ni jina jipya kabisa, Naomba mwenye kuufahamu wasifu wa kiongozi huyu atuwekee hapa tumfahamu, japo kwa ufupi tu ili tusiingie ndani sana kwenye mambo ya Kijeshi.

Natanguliza shukrani
Sifa kuu ni kada wa CCM
 
Yuko vizuri kwa kweli anastaili.namjua sana kama ni kifaa mmepata
 
Back
Top Bottom