Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

Hongera zake; inawezekana Mkingule naye umri ulikuwa umekwenda. Yaani alikuwa anakaribia kustaafu kwa mujibu wa sheria.
LAKINI KULIKUWA NA MEJA GENARAL MAKANOZ ANAUMRI WA MIAKA 50 NA ALIKUWA MKUU WA NAVY BAADAYE MAMA KAMPELEKA RWANDA KUWA BAZOZI
 
Alifanya kazi mzuri sana kule Mishamo na Katumba na ni kamanda wa vita kwelikweli maana aliingia mpaka front line mwenyewe na askari, ingawa ki usalama ilikua ni hatari kulingana na cheo chake lakini ops ilifanikiwa Kwa zaidi ya 100% Vetting yake imekaa poa sana.
 
Wenzetu ni Sheria kabisa kuwa na Mwili na uzito unaotakiwa. Kinyume na hapo unachukuliwa hatua hata kuwa terminated. Nadhani sisi sheria haipo bali tunahimizana tu kufanya mazoezi
Uongo
 
Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali, na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF).

Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi.

====

RAIS, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (Chief of Defence Forces – CDF).

Kabla ya Uteuzi huo, Mkunda alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi (Chief of Operations and Training).

Rais Samia pia amempandisha Cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na amemteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff – C of S).

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini (Commissioner for Research and Military Development) katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Vile vile amemteua Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Uapisho utafanyika tarehe 30/06/2022 saa saba mchana Ikulu, jijini Dar es Salaam.

View attachment 2276626

View attachment 2276683
Picha: Meja Jenerali Jacob John Mkunda
Mkingule kaondolewa kumpisha Mzanzibari
 
Mutiny Nyerere asingekimbia Ikulu na wanajeshi wasingefukuza maofisa wao. Soma New York Times ya mwaka 1964. Kilishanuka ila bahati yake Nyerere alirudishwa madarakani na Waingereza

Nyerere hakuwai Kupinduliwa katika utawala wake yale ya mwaka 1964 yalikuwa maasi ya Jeshi therefore get your fact right and that NYTimes article haionyeshi Kama Nyerere alipinduliwa.
 
Hii staili ya kupandisha vyeo na kuteua alianza JPM ina maana ile safu ya juu haiamiki kwa Cha cheo Cha CDF.......??????
 
Uteuzi mzuri wenye dalili za kuijibu hii hoja, Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu?. Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine? Tangu kuanzishwa kwake JWTZ mwaka 1964, baada ya Luteni Generali mmoja tuu mwenye jina la Abdalah, ambaye alikuja kuwa CDF, leo ndio Luteni Generali wa mwingine mwenye jina la Salumu ameteuliwa, akiwa ndie Mzanzibari wa kwanza kufikia cheo hicho, na hivyo kuweka a possibility ya Tanzania kuja kupata CDF kutoka upande wa pili wa Muungano in future.
NB. Naomba kuweka caveats ya kutuhumiwa mbaguzi, makabila na mdini, amini usiamini my concern were bonafide genuine kuuliza mbona ma CDF wote ni kutoka upande mmoja na dini moja?. Unaweza kukuta no one noticed anything mpaka baada ya concern, ndio watu wakajiuliza, hivyo ikabidi kaji affirmative action kafanyike kumuondoa Luteni Generali aliyefuata kwenye normal progression ya kuja kuwa CDF, ili to create a room ya mtu wa kwanza wa upande wa pili naye aweze kuwa Luteni Generali!. Na kwa faida ya wanajukwa hili Pasco Mayalla kabla ya kuwa mtangazaji wa RTD, alipitia JKT Makotupora na MMJKT, kisha akajiunga straight na JWTZ Airwing na kuajiriwa with MT. Number, na sasa ni askari wa akiba, ikitangazwa vita sisi ndio tunatangulizwa mbele ili tuwe chambo.
P
Hapo kwenye chambo daah!Ni lazima mkuu utatokomea kusiko julikana,mambo ya kutawanywa maini kama wafanywavyo Ukraine si jambo dogo.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali, na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF).

Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi.

====

RAIS, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (Chief of Defence Forces – CDF).

Kabla ya Uteuzi huo, Mkunda alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi (Chief of Operations and Training).

Rais Samia pia amempandisha Cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na amemteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff – C of S).

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini (Commissioner for Research and Military Development) katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Vile vile amemteua Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Uapisho utafanyika tarehe 30/06/2022 saa saba mchana Ikulu, jijini Dar es Salaam.

View attachment 2276626

View attachment 2276683
Picha: Meja Jenerali Jacob John Mkunda
sasa tunataka jeshi la wananchi kwelikweli siyo jeshi la ccm
 
Back
Top Bottom