Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

huwa sipendi kusikia Mkuu wa Majeshi anaitwa "Afande...Mkuu wa Majeshi" sielewi hili neno "afande" ni sahihi kulitumia kwa wenye vyeo vya juu?!

kwa uelewa wangu nilidhani kwa vyeo vya juu anatakiwa kuitwa "kamanda".
naomba ufafanuzi kwa wenye kujua maana huwa nahisi kumuita "afande" ni kama kudunisha cheo chake.
wataalamu naomba mtusaidie hapo.
Hapana, nadhani kinyume chake ndiyo sahihi. Ukiwa jeshini, juniors wako au surbodinates wako unawaita "kamanda" halafu wao wanakuita Afande. Hali kadhalikka, seniors wako wewe au superiors wako unatakiwa uwaite Afande.

CDF ni Afande wa kila askari wa JWTZ, na possibly afande wa kila Askari aliye ndani au nje ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, provided askari huyo hana title ya CDF or its equivalent
 
Kati ya vitu sijuagi ni vyeo vya kijeshi aisee naonaga kama hesabu za maumbo
Vyeo vyao vimekaa hivi:

Wale wasiokuwa na nyota mabegani;

PRIVATE ngazi ya kwanza kabisa; havai cheo chochote begani wala mkononi
LANCE COPLO- Ana "V" moja kwenye kwapa la mkono wa shati lake
COPLO- "V" mbili
SERGENT-"V" tatu
STAFF SERGENT-V" tatu pamoja na ngao ya bibi na bwana
SIR MAJOR AU WARRANT OFFICER II- Ana KOROKORO lina alama ya mwennge ukiwa umezungukwa na maua nadhani; huwa analivaa kwenye mkono wake wa kulia kama saa pamoja na fimbo

REGIMENTAL SIR MAJOR (RSM) AU WARRANT OFFICER I-ana KOROKORO lenye NGAO YA BIBI NA BWANA PAMOJA NA FIMBO.
Huyu huwa aneuliwa na Rais na huwa anakuwepo mmoja tu katika kila kikosi. Ni cheo kingine ambacho JWTZ wanakithamini sana mithili ya wanavyothamini cheo cha CDF. Huyu huwa pia ni mkuu wa nidhamu kwenye kikosi, na anaheshimika sana na maoifsia wa Jeshi hata wenye nyota amboa kicheo wako juu yake

Wale wenye kuanzia na nyota moja mabegani

SECOND LIUETENANT- nyota moja begani
LIUETENANT- nyota mbili begani
CAPTAIN-nyota tatu begani
MAJOR- Ngao begani; bibi na bwana
LIUTENANT COLONEL (LUTENI KANALI). Ngao na nyota moja begani
KANALI- Ngao na nyota mbili begani
BRIGADEER GENREAL- Mkasi na nyota moja begani
MAJOR GENERAL-Mkasi na nyota mbili begani
LIUTENANT GENERAL-Mkasi na nyota tatu begani
Huyu naye huwa anakuwa ni mmoja tu kwa Tanzania nzima, na anatteuliwa na Rais

CDF-Mkasi na nyota nne begani!!!!!!!

Naishia hapa ila kama kuna mwingine mwenye kuendelea zaidi ya hapa, basi naomba anisaideie kwa cheo cha FIELD MARSHALL
 
sasa tunataka jeshi la wananchi kwelikweli siyo jeshi la ccm

Ni ngumu sana ukifika vyeo vya ngazi fulani. Mfano sherehe hii ya kitaifa:

Brigedia Jenerali balozi Wilbert Ibuge mkuu wa mkoa wa Ruvuma akimkabidhi mwenge Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ambaye ni mkuu wa mkoa wa Mtwara

 
Kwani kupinduliwa kukoje? Ulitaka mpaka Nyerere akamatwe na wanajeshi wake kama yule wa Burkina Faso?
Hivi ungekuwa kwenye position ya Emiliano Mzena na Oscar Kambona kwa wakati ule ungemshauri Rais afanye nini awasubiri Wanajeshi pale Ikulu ?.

Na kwenda kujificha mpaka pale maasi yalipoisha ndio ndio unasema Mwalimu alipinduliwa aisee dude you're not serious at all.

Nasisitiza hata katika hilo gazeti la NYTimes halionyeshi Kama Mwalimu na Kawawa walipinduliwa.
 
uwiano unao zingatia vigezo, sifa na ujuzi, na kwa zama hizi bila shaka wasomi waenye sifa wa aina zote wapo wengi sana hakuna kisingizio, hizi sio zama za miaka ya 61, lazima mahitaji yaendane na zama tulizo nazo hivi sasa ili kuzidi kuimarisha umoja wetu na mshikamano kama Taifa moja.

kila mtanzania mwenye sifa anao wajibu wa kulijenga Taifa sawa na mwengine, hakuna mwenye haki zaidi ya mwengine.

Tunacho kishauri hapa ni katika kuimarisha umoja na uzalendo imara, na huo unatokuwepo kwa wale wote wenye sifa kushiriki bila kutengwa kwa maksudi au hila.
Kule kwenu Zanzibar hakuna wasomi wakristo?
 
26 February 2020

Operesheni safisha Katumba 2020
View attachment 2277007
Akitowa taarifa ya operesheni hiyo inayojulikana kwa jina la Operesheni safisha Katumba 2020 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera ,Mkuu wa Brigedi ya Magharibi, Brigedia Jenerali Jacob Mkunda alisema kuwa katika operesheni hiyo walikamata bunduki 50.

Alifafanua kuwa katika bunduki hizo walizofanikiwa kuzikamata ni bunduki za kivita 13 aina ya SMG , Bunduki tatu aina ya G3, Raifo moja na Gobole 33.

Aidha wamekamata risasi 28 na mitego ya kukamatia wanyama 13

Brigedia Generali Mkunda alieleza kuwa katika msako huo wameweza kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 17 ambao na Raia wapya wa Tanzania wenye asili ya nchi ya Burundi katika ya watuhumiwa hao wanne wamekamatwa katika Makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilaya ya Mpanda na 14 wamekamatwa katika Makazi ya Wakimbizi ya Mishamo Wilaya ya Tanganyika

Alisema kuwa kwenye msako huu wameweza kubaini uwepo wa viwanda vya kutengeneza bunduki aina ya gobole kwenye makazi ya wakimbizi ya Mishamo ambazo zimekuwa zikitumika katika kufanyia ujangili wa kuua wanyama kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kwenye mapori ya akiba .


Kamanda wa operesheni ya safisha Katumba 2020; kanali Evance Mallasa akionyesha moja ya silaha zilizokamtwa
DSC01524AA-1024x577.jpg

Mzigo wa silaha zilizokamatwa katika makazi ya mishamo na katumba wanapoishi raia wapya wa Tanzania wenye asili ya Burundi

Source : michuzi jr
Huyu mwamba ana picha moja tu mtandaoni, inaonekana sio muuza nyago ni kazikazi[emoji16]
 
Hii staili ya kupandisha vyeo na kuteua alianza JPM ina maana ile safu ya juu haiamiki kwa Cha cheo Cha CDF.......??????
Ninachokiona mimi katika hili ni kwamba kuna vijana wengi wameingia Jeshini wakiwa na umri mdogo tofauti na ilivyokuwa hapo awali, kitu kinachopelekea vijana hao kufikia kwenye vyeo stahiki vya kuweza kupiga kick kidogo tu halafu wanafikia kwenye sifa ambazo CDF anatakiwa kuwa nazo. Kitu hiki sasa ndiyo kinachopelekea utaratibu huu uweze kutumika.

Kwa upande mwingine, seniors ambao wapo jeshini na ambao wana-qualify kuteuliwa kwa cheo cha CDF bila ya kupigwa kick kidogo; wao waliingia jeshini wakiwa na umri mkubwa kidogo, kitu kinachopelekea umri wao kuwa mkubwa kiasi kwamba kama ikitokea wakateuliwa, basi wanaweza kutumika kwa sehemu kidogo tu ya muda wao halafu baada ya hapo wanafikia umri wa kustaafu, na hicho ndicho kinachopelekea mchakato huu kuwa hivyo.

Kwa upande mwingine tena, seniors hawa walioingia jeshini kipindi cha nyuma baadhi yao au wachache wao ndiyo waliowahi kupigana vita vya Kagera kitu kilichoplekea waweze kupanda cheo kwa umahiri zaidi hadi kuwa jitrani kabisa na cheo cha u-CDF. Tofauti na hawa vijana wengine waliowahi kuingia jeshini baada ya vita vya Kagera, ngao yao wao ni shule na ndiyo inayowapelekea wapande vyeo. Tuseme kwa mfano kama kungekuwa na ujasiriamlai jeshini, nahisi kwa sasa jeshi linngeweza kuanzisha hata Universuty na bila ya ku-outsource lecturers wa university yao, walimu wangepatikana humo humo jsehini.

Kwa hiyo kwa sasa, naweza kusema jeshi letu llimetapakaa umahiri wa kila aina kuanzia kwenye medani za kivita hadi kwenye mambo mengine yanayoendelea uraiani kama vile maswala ya elimu
 
Kwasababu ana 'Akili' na pia anaweza Kupambana na Jeshi Kali Afrika kwa sasa la Rwanda chini yake Rais Paul Kagame.
So ukiwa na AKILI kwa taratibu za jeshi unastahili kurushwa Vyeo?,,,,Yaani kijeshi mtu anaweza kutoka kuwa Capteni na kuwa Luteni kanali,,,,bila kuwa Meja...
 
ndiyo mambo yanavyokwendaga, ni kuishi vizuri na boss wako na kuchapa kazi !! hongera kwake ila tunataka jeshi ligeuke liwe chanjo cha technologia na ubunifu nchini - sina uhakika kama Jeshi lina kiwanda hata kimoja, au limeshiriki vipi kwenye sera ya viwanda ya Taifa.
Sina uhakika pia kama jeshi linazalisha zao la Kilimo lolote kubwa liwe la Chakula ama Biashara la kimkakati nchini - haya ni mambo ambayo jeshi linatakiwa kufanya wakati wa kipindi cha amani.
Samia amekataa jeshi kujishughulisha na biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom