Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali, na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF).

Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi.

====

RAIS, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Jenerali na amemteua kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (Chief of Defence Forces – CDF).

Kabla ya Uteuzi huo, Mkunda alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi (Chief of Operations and Training).

Rais Samia pia amempandisha Cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na amemteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (Chief of Staff – C of S).

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini (Commissioner for Research and Military Development) katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Vile vile amemteua Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Uapisho utafanyika tarehe 30/06/2022 saa saba mchana Ikulu, jijini Dar es Salaam.

View attachment 2276626

View attachment 2276683
Picha: Meja Jenerali Jacob John Mkunda
Hongera zake.Naona bado kijana.
 
Uyo
IMG_20220630_164603.jpg
 
Kuna watu Huwa wanaishi kama hawapo... Na unakutaa Wana impact sanaa

Watu wamefanya makubwa....ila sio watu wa show off.....
umenena mkuu, na mara nyingi kuwabaini watu wa namna hiyo inahitaji jicho la ziada maana huwa wanazibwa kwa maksudi ili wasionekane, lkn kwa umakini wa Mama lazima atawaona tu.
 
Ningekuwa mimi ndio mabeyo saizi angali nipo Ikulu naitwa Rais na nisngetoka madarakani mpaka nife namaanisha mungu aingilie Kati.
Faida ni ndogo kuliko hasara!
1) Kelele za jumuia ya kimataifa!
2) Usalama wako binafsi inakuwa issue maana wakati wowote na wewe unaweza kupinduliwa au hata kuuwawa!
.
.
. ETC JAZA!
 
Mkunda.(ng'unda) safisana!

Namkumbuka sana.jeneral logaa mkunda...alisumbua sana miaka ile DRC mwisho wasiku karudi kwao Rwanda.hadi leo sijui yupowapi.
Jasiri sana hawa wenye majina hayo.

Sent from my SM-A022F using JamiiForums mobile app
 
Hivi ungekuwa kwenye position ya Emiliano Mzena na Oscar Kambona kwa wakati ule ungemshauri Rais afanye nini awasubiri Wanajeshi pale Ikulu ?.

Na kwenda kujificha mpaka pale maasi yalipoisha ndio ndio unasema Mwalimu alipinduliwa aisee dude you're not serious at all.

Nasisitiza hata katika hilo gazeti la NYTimes halionyeshi Kama Mwalimu na Kawawa walipinduliwa.

Ndiyo maana nimekuuliza, unajuaje Rais amepinduliwa? Fafanua labda tutaelewana.

Naomba pia nikuulize, bila ya jeshi la Waingereza kuingilia kati Nyerere angerudi vipi ikulu? Maana wanajeshi walimfata mpaka Ikulu akaponea chupuchupu.
 
Vyeo vyao vimekaa hivi:

Wale wasiokuwa na nyota mabegani;

PRIVATE ngazi ya kwanza kabisa; havai cheo chochote begani wala mkononi
LANCE COPLO- Ana "V" moja kwenye kwapa la mkono wa shati lake
COPLO- "V" mbili
SERGENT-"V" tatu
STAFF SERGENT-V" tatu pamoja na ngao ya bibi na bwana
SIR MAJOR AU WARRANT OFFICER II- Ana KOROKORO lina alama ya mwennge ukiwa umezungukwa na maua nadhani; huwa analivaa kwenye mkono wake wa kulia kama saa pamoja na fimbo

REGIMENTAL SIR MAJOR (RSM) AU WARRANT OFFICER I-ana KOROKORO lenye NGAO YA BIBI NA BWANA PAMOJA NA FIMBO.
Huyu huwa aneuliwa na Rais na huwa anakuwepo mmoja tu katika kila kikosi. Ni cheo kingine ambacho JWTZ wanakithamini sana mithili ya wanavyothamini cheo cha CDF. Huyu huwa pia ni mkuu wa nidhamu kwenye kikosi, na anaheshimika sana na maoifsia wa Jeshi hata wenye nyota amboa kicheo wako juu yake

Wale wenye kuanzia na nyota moja mabegani

SECOND LIUETENANT- nyota moja begani
LIUETENANT- nyota mbili begani
CAPTAIN-nyota tatu begani
MAJOR- Ngao begani; bibi na bwana
LIUTENANT COLONEL (LUTENI KANALI). Ngao na nyota moja begani
KANALI- Ngao na nyota mbili begani
BRIGADEER GENREAL- Mkasi na nyota moja begani
MAJOR GENERAL-Mkasi na nyota mbili begani
LIUTENANT GENERAL-Mkasi na nyota tatu begani
Huyu naye huwa anakuwa ni mmoja tu kwa Tanzania nzima, na anatteuliwa na Rais

CDF-Mkasi na nyota nne begani!!!!!!!

Naishia hapa ila kama kuna mwingine mwenye kuendelea zaidi ya hapa, basi naomba anisaideie kwa cheo cha FIELD MARSHALL
Nimekupata vizuri sana,je ivi hawa wajeda umri wao kustaafu upoje,kwamaana unakuta mtaani kijana wa miaka 45 anakwambia mie ni mstaafu wa jeshi,je miaka yao ya kustaafu jeshi ipoje
 
Kuanzia private hadi sajenti V3 umri wao kustafu ni miaka 45.
Ni kutokana na kwamba Hawa watu wanafanya kazi za miguvu akili kidog so kwa age hiyo wanakuwa washachoka.
Kuanzia Staff Sargent Hadi RSM ni miaka 50-55
Kuanzia afisa Second liutenant na kuendelea umri wao ni miaka 60.

Kwa maafisa wa ngazi za juu Hadi 65
Huo ni uongo uliokithiri
 
Nimekupata vizuri sana,je ivi hawa wajeda umri wao kustaafu upoje,kwamaana unakuta mtaani kijana wa miaka 45 anakwambia mie ni mstaafu wa jeshi,je miaka yao ya kustaafu jeshi ipoje
Kadri unavyozidi kupata cheo cha juu, ndivyo kadri umri wako wa kustaafu uanvyozidi kuongezeka. Huyo aliyestaafu kwa umri huo nadhani atakuwa alikuwa kwenye rank ya CAPTAIN, na aliendelea kubaki hapo hadi umri wa miaka 45 ulivyotimia. Huyu alitakiwa awe MAJOR kabla ya umri huo na hivyo umri wake wa kusataafu nao ungepanda kutoka miaka 45 kwenda juu zaidi
 
Back
Top Bottom