Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

Hongera zake; inawezekana Mkingule naye umri ulikuwa umekwenda. Yaani alikuwa anakaribia kustaafu kwa mujibu wa sheria.
 
huwa sipendi kusikia Mkuu wa Majeshi anaitwa "Afande...Mkuu wa Majeshi" sielewi hili neno "afande" ni sahihi kulitumia kwa wenye vyeo vya juu?!

kwa uelewa wangu nilidhani kwa vyeo vya juu anatakiwa kuitwa "kamanda".
naomba ufafanuzi kwa wenye kujua maana huwa nahisi kumuita "afande" ni kama kudunisha cheo chake.
wataalamu naomba mtusaidie hapo.
 
Jamaa mtu peace sana, nishawahi kua nae kwenye issue flan hivi(binafsi) sema kuonana nae ilikua mara chache walinzi wake ndo unaonana nao tuu, nadhan ilikua planned toke mda maana sio kwa ule ulinzi, ndio nmeelewa sasa ila hongera mno kwake kamanda.
 

Kila kamanda ni afande ila sio Kila afande ni kamanda.
 
Mungu huwa akiamua kukusimamisha hata kama ukiwa jalalani utainuka
 
Kapandishwa kutoka Meja jenerali kawa Jenerali

Mwenzake kapandishwa kutoka Meja jenerali kawa Luteni Jenerali

Hii ki-protocal imekaaje....??? hajarukishwa Cheo huyu mwamba
 
Kwa wale wasioelewa, Lt General anakuwa mmoja ktk jeshi la TZ. Kwa hiyo sio kweli kuwa amewaruka Lt Generals akamchukua Major General.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…