Rais Samia amteua Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

Nakubaliana na wewe mkuu ila sidhani kama kumtoa Lt. Gen M. E. Mkingule na kumpa ubalozi ni njia ya kumtafutia nafasi aliyekuwa Maj. Gen Othman ili kubalance kwasababu yule ni mnzanzibari uzuri wewe kama ulivyojieleza hapo unafahamu utaratibu na miongozo ukifuatilia vizuri utakuja kujua kwanini CoS kapewa ubalozi mkuu wangu P
 

Ukirukwa huwezi kubakizwa; utasukumwa kwenda kwenye ubalozi.
 
Safi sana lijamaa limejaa kiume kabisa yaani unaona kabisa hili ni CDF kakamavu, emoji ya msuli. Hongera Mheshimiwa Rais kutupatia jembe jingine.
 

Kijeshi, ingekuwa insult kwa Mkingule kujikuta ghafla yuko chini ya mtu ambaye alikuwa chini. Kuondolewa pale ilikuwa lazima.
 
Hoja nzito sana.... Uko sahihi mkuu
 
Huyu Generali ni Kabila gani ?
Ninachojua Mnadhimu katoke Upande a pili wa Nchi, tuna Balance
 
JWTZ mtu yeyote akifika cheo cha Brigadier General ujue ni jembe; usiulize uwezo wake. Ni Shimbo tu aliyetaka kulifanya Jeshi kama chombo cha siasa lakini pia hakufanikiwa.
 
Wale maluteni jenerelai waliorukwa wana umri mkubwa wanakaribia kustaafu. Nadhani wote watastaafu ndani ya mwaka mmoja au miwili tu. Anatakiwa CDF adumu angalu miaka mitano kabla ya kufikia umri wa kustaafu, kwa hiyo ilikuwa ni lazima kutafuta damu changa.
 
Toka maktaba :

Toka maktaba :
Up dates 19 May 2022 toka mitandaoni

Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo aliongozana na maofisa wajuu waandamizi bungeni wakati wa bajeti ya wizara ya ulinzi, spika wa Bunge akawatambulisha :


  • Luteni jenerali Mathew Edward Mkingule mnadhimu mkuu wa jeshi
  • Meja Jenerali Anthony Chacha Sibuti mkuu kamandi ya jeshi la nchi kavu
  • Meja jenerali Rajabu Nduku Mabele mkuu wa JKT
  • Meja jenerali Amri Salim Mwamy mkuu wa tiba jeshini
  • Meja jenerali Ibrahim Michael Mhona mkuu wa chuo cha ulinzi cha taifa NDC
  • Rear Admiral Ramson Godwin Mwaisaka mkuu wa kamadi ya jeshi la wanamaji
  • Meja Jenerali Shabani Mani mkuu wa kamadi ya anga
  • Meja jenerali Jacob John Mkunda operesheni na utendaji wa kivita
  • Meja Jenerali Salim Othman mkuu tafiti na maendeleo ya jeshi
  • Meja Jenerali Hawa Issa Kodi mkuu wa logistics na uhandisi jeshini
  • Brigedia jenerali Iddi Saidi Nkambi mkuu wa kamandi Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi MMJ
  • Brigedia Jenerali Fadhili Nondo mkuu vikosi Zanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…