Rais Samia amteua Sophia Mjema kuwa Mshauri wake kwenye masuala ya wanawake na makundi maalum

Rais Samia amteua Sophia Mjema kuwa Mshauri wake kwenye masuala ya wanawake na makundi maalum

Mjema alipwaya sana

Sophia hana convicing Power yoyote

Hiyo nafasi za uenezi walizitendea haki akina Nape na Polepole

Humprey Polepole tatizo lake alilewa sifa na kujiona yeye ndio yeye mbele ya bosi wake

Hiyo ni kazi ya propaganda na mikakati

Waangalie wale wasemaji wa Yanga na Simba wanavyopiga domo na vijembe ndio kazi za uenezi kupiga domo na kujibu mashambulizi ya wapinzani

Chadema wamepeleka moto operation 255 kanda ya ziwa yeye hajaongea lolote anasubiri wabunge watoke mafichoni kwenye majimbo yao na kuanza kulia lia wapate huruma ya wananchi

Sophia alipwaya sana sana
Pia, nafasi ya Katibu Mkuu aliyepo amepwaya sana.
 
View attachment 2788882
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua ndugu Sophia Edward Mjema kuwa Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na Makundi Maalum.

Kabla ya uteuzi huu Bi. Sophia alikuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM.
Anakula pesa ya Bure tuu.

Nani Huwa anaenda kumshauri Rais zaidi ya cabinet na vyombo?
 
Haya ya Makonda kuwa mwenezi yasije kujirudia ya Salim kuwa Semaji la Taifa, mwisho wa siku ikawa ni mwengine

Tuweke akiba ya maneno na muda ni mwalimu mzuri
 
haya zuhura chapa barua nyingine chap ya kumteua makonda hiyo nafasi aliyoacha mjema.
Yaani zamu hii makonda hajapata bahati mbaya kama Kikeke ambaye walipreanounce uteuzi wake wa ukurugenzi wa habari akapigwa chini huyu ametangazwa kabla na kateuliwa vilevile!
 
Yaani zamu hii makonda hajapata bahati mbaya kama Kikeke ambaye walipreanounce uteuzi wake wa ukurugenzi wa habari akapigwa chini huyu ametangazwa kabla na kateuliwa vilevile!
Makonda anaishi kwa ushirikina na mbinu zote chafu
 
Duuh nepi nae wampe ushauri kina baba na vijana ndio pana mfaa.
 
Boznia huko Lushoto kaa mguu sawa wakati wa kupasha kiporo chako ni sasa ili ukaribie kilipo chungu.
 
Vipi akiamua kumuweka Chalamila? Sio dizaini ya akina Nape huyu? Hapa shime ni kukwepa sukuma gang kwa hali yoyote ile.

Pia usisahau, Makonda akishika usukani, huwa hana urafiki na msoga clan, mama na msoga clan ni damu damu. Unadhani anaweza ku-overlook hilo?
Mbona alimfungia kamba za viatu RizOne ??!
 
Back
Top Bottom