Full Blood Picture
JF-Expert Member
- Jan 7, 2021
- 2,223
- 3,961
Rais Samia Suluhu Hassan amesema anamfuta kazi Mkuu wa Wilaya ya Mtwara vijijini, Hanafi Msabaha kutokana na kushindwa kusikiliza kero za wananchi hadi kupelekea wananchi hao kurudisha kadi za chama cha Mapinduzi (CCM).
Samia ameyasema hayo leo Jumapili Agosti 27, 2023 akifunga mafunzo ya uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika Shule ya Uongozi Kibaha, mkoani Pwani.
"Mnapopuuza kero zao sijui mtaenda kujibu nini kwa Mungu…..Mkuu wa Wilaya anahongwa, mradi unapelekwa usikotakiwa kiasi kwamba wananchi wanarudisha kadi za chama, Sina Imani na mkuu wa Wilaya anayesababisha kadi zirudishwe, Mkuu wa Wilaya Mtwara vijijini, namtimua Leo, siwezi kustahimili kadi zinarudishwa,”amesema Rais Samia.
View: https://www.instagram.com/p/CwcbU1FN79K/
bado atatumbua wengi, maana mambo ni mengi sana ya kuchanganya