Rais Samia amtumbua Kamishna Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya

Baada ya muda utakuja sikia hao hao waliostaafu kuteuliwa Tena katika nafasi nyinginezo, kama vile hakuna wenye sifa za kushuka hizi nafasi.

Wanaofauli vyuo wako lukuki na hata ndani ya Serikali vijana walioko kazini muda bila kupanda daraja wapo!
Nchi ngumu sana.

Ndio maana KATIBA KATIBA mpya muhimu. Punguza madaraka ya Rais na kuwepo na usaili au kupigiwa kura Kwa Hawa watu kwenye nafasi mbalimbali
 
Maza kawaondoa vijana wote wa JPM(Wasukuma) 1. Mashimba, 2. Kalemani. 3. Dotto 4. Ngusa 5. Prof Makubi then kaweka waislam wenzake, kanda ya ziwa wakimchagua huyu maza watakuwa hawana akili
 
safi sn.
Dawa za kulevya kwa sasa zinauzwa kama njugu kama vile hakuna mamlaka ya kupambana na madawa ya kulevya.

Kwa sasa takwimu zinaonyeaha wauzaji na wasambazaji wameongezeka.
Kaji aliiweza sana ile nafasi lakini lile wimbi la 'mabadiriko' likamkumba.Akawekwa huyu naona maji yamezidi unga nae.Tumsubiri na Lyimo pia tuone atasurvive pale kwa muda gani.
 
Nakubaliana na wewe
 
Kwa hiyo kwa kuwa mtendaji wa kijiji ana mamlaka ya kumtia mtu ndani basi ni mkubwa kuliko waziri?

RC ni mkuu wa ulinzi na usalama hivyo kumtia mtu ndani si ajabu. Waziri kwenda kusaini kwa RC ni utaratibu wa kumjulisha kwamba yupo mkoani ili aweze kutoa ulinzi lakini si kwamba wanalingana ki- seniority.

RC na DC wote ni wawakilishi wa Rais katika maeneo yao lakini hawako sawa ki- seniority.

RC hawezi kuomba barabara ijengwe sehemu fulani mkoani kwake kwa sababu hilo ni suala la kibajeti.

Kwa hiyo acha kupotosha waziri ni senior kwa RC.
 
Ngusa samike si alikua msemaji wa familia wakati wa msiba wa Magufuli. Au nafananisha??
 
Mkuu kanuni za utumishi wa umma ni kama hazipo siku hizi. Mambo yanafanyika kienyeji tu..!
 

Well said mkuu!

Maana inayumbisha issues za maslahi (benefits)
 
Lakini KM na RAS si ni rank moja how come unasema ameshushwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…