Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Samia anajifanya mtu wa dini, mpenda maridhiano nk, kumbe ana vinyongo na visasi moyoni
 
DPW
 
Kwa jicho la kiroho: Sakata la Dr. Slaa | Page 12 - JamiiForums Kwa jicho la kiroho: Sakata la Dr. Slaa
 
Sababu ya kumvua ni ipi?? Wewe uliyemvua slaa ubalozi MWENYEZI mungu naye atakuvua kila kitu siku si nyingi
 
Sisi tunajua alikua balozi hivyo ana cheo cha balozi hiyo haipingiki... warudishe muda nyuma kisha wasimteue kuwa balozi ndio itawezekana vinginevyo ni kupoteza muda na mambo yasiyo na msingi... asilimia kubwa ya nchi iko gizani sasa hivi hakuna umeme watengeneza juisi za miwa, mama lishe, wavuvi nk vitu vyao vinaoza sababu hamna umeme watu wanajikita na upumbavu eti kumvua mtu ubalozi...!! Tumerudi nyuma sana kama taifa...! .
 
Wewe mzee hebu jitafakari kama akili yako ipo sawa. Ulianza kuvuliwa upadri , Ukaingia kwenye siasa Chadema wakakuvua uanachama baada ya kusaliti chama chako na kuingia CCM. Leo hii tena umevuliwa Ubalozi cheo ulichopewa na CCM baada ya kuhama kutoka Chadema.

Kama mtu mzima lazima ujiulize wewe una matatizo gani? Kwanini kila ulipo jamii inakukataa.?

Nakushauri achana na mambo yote kaungame kanisani kwako ubaki muumini wa kawaida na utubu kwa Mungu akusamehe makosa yako.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Hakuna sehemu niliyosema kuwa mabalozi pekee ndo wana diplomat passport.

Huenda mie nikawa darasa la saba hebu wewe mwenzangu uliyesoma nisaidie kunijibu swali lang nisilolijua

Je hadhi ya mbunge na balozi ziko sawa kimataifa?
We Slaaa kwa Umuri wake haihitaji hizo mbbwe, nyie ndio wale mnashinda kubeti badala ya kupigania nchi, endelea kubet na kuwaza kwamba sasa Slaa atakoma.

Kwani wakati hajawa Balozi si alikuwa ana safiri? Kuna alicho kuwa anapungukiwa akisafiri?
 
Ni kawaida ya ccm kuwatumia watu kama toilet paper! Kifuatacho hapo ni kukamatwa na kupandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uchochezi
Ndio maana hata mabalozi wetu hawana faida kwa Taifa maana wanafanya kwa maslahi yao na watu wao tu.

Yaani Balozu akisimamia jambo kwa maslahi ya Taifa anavuliwa Ubalozi,,,πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Nyie ni wale wajinga wa jukwaa? Huu ujumbe kawaeleze wazee vijiweni juenda wakanunua huu ushauri wako
 
DKt Wilbroad Slaa amevuliwa hadhi ya ubalozi kuanzia leo Septemba 1, 2023.
Taarifa imetolewa hivi punde na Ikulu katika mtandao wa kijamii wa X ama Twitter.

Dkt Slaa alipewa hadhi hiyo mwaka 2017.
CCM bana, kisa tu kasema DP World ni matapeli, angesifia je kama wale chawa wengine?
Hapo ndipo tunatia mashaka na hiki chama kama ni genuine kweli kuongoza nchi yetu. Chama cha kimajungu majungu.
 
Kwa akili zako ndogo unafikir Dr. Slaa anapambania nchi?

Unafikir angekuwa bado yupo kwenye payroll angesema lolote?
Kwanza niseme, sikujui wewe unatokea wapi, kwa sababu sijawahi kukusoma popote humu. Kwa hiyo unapohoji akili zangu ninakuona kama wewe ni chizi tu.
Kuhusu Dr Slaa anachopambania; hapo pia inaonyesha ufinyu wako wa kutambua mambo. Hili swala lililosababisha kuvuliwa hiyo inayoitwa "hadhi", hata kama angekuwa anapambania maslahi yake, maadam yapo upande wa maslahi ya nchi, bado huoni uhusiano wake?

Wewe ni bwege.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…