Hata hii trillion 7 wanayopigia kelele zanzibar itapata trillion 1.3 kwa hiyo yenye faida ni zanzibar ila watanganyika faida ni ndogo ukilinganisha na eneo na idadi ya watu!
Rais kwa kuwa ni Mzanzibar anatumia ho mwanya ila kwa vile watanganyika hatuwezi kuhoji na ukihoji unasakamwa kama Ndugai!
The level of reasoning is very low! Ni mda wa wazanzibar kutumia kivuli ya Watanganyika kujimemesha!
Kwenye ajira pia hakuna uwiano juzi hapa wametangaza ajira bila shaka TRA asilimia 20 wanapewa Wazanzibar! Je hapo **** uwiano Sawa?
Viongozi wetu watanganyika mpo tu kwa vile mnataka madaraka kila kitu ndio mwalimu!
Kichwa chako kina Acid very conki., Kwanini Tanganyika muliamua kuunga na Nchi yenye idadi ndogo ya watu? Kwanini hamukuungana na Nchi kama Nigeria/Algeria nk., mkaamua Zanzibar tu
Idadi ya watu sio kigezo cha wewe kupata chingi huyu akapata kidogo kutokana na idadi yao., Zanzibar ni nchi huru kama ilivyokuwa tanganyika na ziliungana kwa hiari benefits zilitakiwa ziwe sawa bin sawiya lakini kwasababu Tanganyika na Mchongameno alikuwa na lengo la kuilaghai zanzibar ndio yanatokea haya yoote.,
Duniani kote hakuna aina muungano kama huu ni udhalimu mtupu.
Zanzibar ndio iliyotoa fedha nyingi zaidi za kigeni kuanzishwa BOT kuliko Tanganyika lakini tunapokuja kwenye mapato na BOT yenyewe inaonekana ni mali ya Tanganyika.
Kama mnaona zanzibar ni idadi ndogo ya watu basi vunjeni mkaungane na marekani na nchi nyengine wakubwa wenzenu lakini mnangania.
Ni nchi ya Zanzibar pekee duniani inalipa kodi 2., kodi moja ZRB ni kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar lakini kodi ya pili TRA hizi fedha zoote zinaenda Tanganyika na Zanzibar hawapati mgao wowote toka TRA ni vile Tanganyika mnaneemeka kupitia jasho la Wazanzibari, mnalipana mishahara, chakula na maposho mbali mbali na maendeleo yenu kujenga barabara, reli, sgr sijuwi mabwawa na kila kitu
Tokea uhuru hakuna maendeleo yoyote Tanganyika ilipeleka Zanzibar wao ni wao na watu wao tu., lakini ofisi za TRA kule Zanzibar zimetaradadi kila kona kuwakamua wazanzibari na ndio mana hamtaki kuwaachia.,
Zanzibar sasa imekosa meno hata kujitafutia misaada nje ya nchi mpaka kibali kitoke Tanganyika, Kina Lukuvi hao walisema makanisani hawataiwacha zanzibar kwa sababu muna maslahi makubwa kwenye maisha yenu kutokea Zanzibar.
Nchi kubwa zipo tele duniani kaunganeni nao iachieni Zanzibar wakaungane na jirani zao comoro nk