Rais Samia anajua akikopa asilimia 21 ya mkopo unaenda Zanzibar. Watanganyika wamelala usingizi

Rais Samia anajua akikopa asilimia 21 ya mkopo unaenda Zanzibar. Watanganyika wamelala usingizi

Kuna watu wajinga sana humu! Wao ni kushabikia tu bila kufikiria nje ya box! Mama kashakopa sio chini ya trillion 10 mpaka sasa! Anaenda tena kudabua trillion 7 awagawie tena wazanzibar huku wenzangu na mimi akitokea mtu anahoji! Hapo hapo Watanganyika wanashirikiana na anaewahujumu humsakama aliyehoji! Akili ndogo sana hii!
Haupo sahihi.Siku hizi ni pasu kwa pasu na hiki ndicho kilichomchanganya Ndugai akajikuta anakuwa kambi rasmi ya upinzani Bungeni.
 
Muhimu ni deni liwe separated,kiasi kitakachokwenda zanzabar kijulikane ili kila upande uwajibike katika ulipaji wa deni Kwa kiasi ilichochukua,na sio deni loote liangukie upande mmoja wa jina la MKOPAJI itakuwa ni dhambi.
Anayewajibika kulipa ni Tanzania wala siyo Zanziba! UnaPosema Tanzania kiuhalisia ni Tanganyika maana mambo yote ya Tanganyika yako ndani ya Tanzania! Walishindwa kulipa umeme na wakasema mkitaka kukata kateni tutatumia vibatari, ni muujiza wakilipa wenyewe!! Sana sana Tanganyika watalipa halafu ......
 
Hakuna ubaya wowote tuache wivu Pemba ipo nyuma mno wacheni nayo inyanyuke na Zanzibar Kwa ujumla wake.

::Wenzetu wanataka kutekeleza Sera ya uchumi wa blue wanahitaji meli za uvuvi za kisasa,wavue watuuzie Samaki Kwa bei nafuu ili nyama nayo ishuke bei Kwa lazima.
Kwa hiyo huku Bara ndio tuwakopee na kuwalipia sio?? Kwa Nini wasikope Kwa jina lao???
 
Hii trillion 7 inakopwa kwa awamu ndani ya miaka mitano..
Ukijumlisha na ile 1.3 trillion itakuwa 8.3 trillion ndani ya miaka mitano..
Magu alikopa 29.6 trillion, hela ambazo zingetosha kumaliza miradi ila ni nusu tu ya miradi imekamilika na hela haionekani..

Hii Zanzibar inaongelewa sana kwaajili ya mama! Yani inaonekana ndio weak point yake baada ya kumkosa kila mahali. Hivi nyumbani ulipozaliwa panawezaje kuwa weak point yako?Marais waliopita walishirikiana vipi na Zanzibar kwenye mikopo kwamba mama amekuwa tofauti sana?
Hujui Samia ametatua kero 11 za Muungano ambazo zilishindikana kutatuliwa na Nyerere,Mwinyi,Mkapa,Kikwete na JPM!Ila yeye kazitatua ndani ya miezi michache tu tokea aingie madarakani!
Ajabu ni kwamba kero hizo na namna zilivyotatuliwa imefanywa Siri!Za chini chini ni kwamba mikopo ni Moja ya eneo alilotatua Samia Kwa kuwapa Zanzibar 21% ya kila mkopo unaochukuliwa JMT!
Hizo kero zimetatuliwa Kwa Zanzibar kuneemeshwa,Dr Philip Mpango kawasaliti wadanganyika maana mambo ya Muungano Yako chini ya ofisi ya Makamu wa Rais!
 
Mkuu inasikitisha sana! Badala ya kuhoji wanamsakama Ndugai laiti tungalijua tupo sehemu mbaya sana! Kwa mara ya kwanza Tanzania kwenye uchaguzi mkuu mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM atatoka Zanzibar kitu ambacho si sahihi kiutamaduni miaka yote! Ila kwa vile mama kashaona unaongoza wengi mazuzu watampitisha na kumpigia kura!

Je kuna Mtanzania Bara au mtanganyika wanaweza kupata hata Udiwani au ubunge Zanzibar? Kwa nini sisi turuhusu hii kitu? Saizi kwa mazingira yetu mama Samia amalizie 2025 aiache Tanganyika!
 
Inakopa Tanzania au Tanganyika?
Kama ni Tanzania basi Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
Zanzibar si kuna serikali? Kwann isikope yenyewe? Hapa naona umuhimu wa majimbo,sababu Zanzibar haina tofauti na jimbo la Tanzania
 
Katika uhalisia Tanzania bara (serikali ya JMT) ndo italipa hilo Deni, Zanzibar ina mamlaka yake ya mapato na TRA haihusiki na mapato ya Zanzibar, kifupi Zanzibar ni Kama parasite ndani ya muungano.
Hiki ndicho haswa kinafahamika kama "kuvaliwa kwa koti la muungano" kutokana na aina ya muundo wa muungano tuliokuwa nao. Katiba iliyopo iliangalia hadhi ya nchi za nchi mbili huru, na wala si wingi wa watu waliopo ndani ya nchi hizi mbili kama sehemu muhimu ya kufanya majukumu ya pamoja.

Sababu kama hii ndiyo haswa ilipelekea iliyokuwa jumuiya ya awali ya Afrika Mashariki kuvunjika na kusababisha Kenya kujimilikisha mali nyingi sana za iliyokuwa jumuiya.

Mambo ya muungano ni kama vile ndoa halali ya watu wawili wa jinsi tofauti. Kila mwanandoa pale aingiapo kwenye ndoa ni sharti atambue mazuri na mapungufu ya mwenzake ili aweze kuchukuliana nayo. Ukiingia kwenye ndoa na kuanza kulalamika kuhusu mapungufu ina maana wewe ndiye mwenye matatizo, kwa kuwa ulipaswa kutambua toka hapo awali unaingia katika ndoa na binadamu mwenzako na wala siyo malaika.
 
Hapana, sbb nani analipa mkopo? Yaani kiuhalisi, Tanzania Bara inakopa, inalipa Tanzania Bara, haya mambo inabidi yasemwe vizuri.. Hata tozo tunazolipa, Zanzibar sidhani kama wao wanalipa, najua haipo.

Sbb ni kweli Tanzania Bara inakopa, na kulipa deni ni Tanzania Bara inalipa, deni la Taifa, Zanzibar haihusiki kulipa, sbb Zanzibar wao wanakusanya kodi yao na haihusiki huku Tanzania Bara, na Zanzibar hailipi deni la Taifa. Mimi nafikiri si sahihi Zanzibar kupewa sehemu ya mkopo, sbb kurejesha wao hawapo.

Mimi nilidhani, kama Zanzibar haihusiki kulipa deni la Taifa, pia haistahili kupewa sehemu ya mkopo wa Tanzania Bara. Sbb unapewaje % ya mkopo na ww hulipi huo mkopo?

Hii sio sawa. Kuna tatizo kubwa.
Si Zanzibar, Tanganyika wala Tanzania Bara mwenye uwezo wa kukopa na kulipa, Ni TANZANIA pekee.
 
Zanzibar si kuna serikali? Kwann isikope yenyewe? Hapa naona umuhimu wa majimbo,sababu Zanzibar haina tofauti na jimbo la Tanzania
Tuwe makini sana! Watanganyika tukizubaa kama hivi leo itakuwa hatari sana! Ila kwa vile tuna viongozi wengi sana wanaosaka vyeo wao ni kuunga mkono kila aina ya upuuzi!

Mfano hizo changamoto za muungano ndo zimemfanya Mzanzibar apate asilimia 21 ya mkopo!

Pia ajira zikitoka wao wanapata asilimia 20 mfano juzi zimetoka ajira TRA 1000 na kati ya hizo 200 zimepelekwa zanzibar! Hapo sio Sawa hata kidogo!
 
watanzania bara tulivyo mazuzu,ndugai kqhoji watu wakamjia juu,mpaka Wana ccm wenzake!!!, akili fupi kweli!!
 
Hujui Samia ametatua kero 11 za Muungano ambazo zilishindikana kutatuliwa na Nyerere,Mwinyi,Mkapa,Kikwete na JPM!Ila yeye kazitatua ndani ya miezi michache tu tokea aingie madarakani!
Ajabu ni kwamba kero hizo na namna zilivyotatuliwa imefanywa Siri!Za chini chini ni kwamba mikopo ni Moja ya eneo alilotatua Samia Kwa kuwapa Zanzibar 21% ya kila mkopo unaochukuliwa JMT!
Hizo kero zimetatuliwa Kwa Zanzibar kuneemeshwa,Dr Philip Mpango kawasaliti wadanganyika maana mambo ya Muungano Yako chini ya ofisi ya Makamu wa Rais!
Leta uthibitisho twende sawa
 
Hakuna ubaya wowote tuache wivu Pemba ipo nyuma mno wacheni nayo inyanyuke na Zanzibar Kwa ujumla wake.

::Wenzetu wanataka kutekeleza Sera ya uchumi wa blue wanahitaji meli za uvuvi za kisasa,wavue watuuzie Samaki Kwa bei nafuu ili nyama nayo ishuke bei Kwa lazima.
Nyama ikishuka bei kwa lazima Tanzania inafaidika vipi?
 
Tuwe makini sana! Watanganyika tukizubaa kama hivi leo itakuwa hatari sana! Ila kwa vile tuna viongozi wengi sana wanaosaka vyeo wao ni kuunga mkono kila aina ya upuuzi!

Mfano hizo changamoto za muungano ndo zimemfanya Mzanzibar apate asilimia 21 ya mkopo!

Pia ajira zikitoka wao wanapata asilimia 20 mfano juzi zimetoka ajira TRA 1000 na kati ya hizo 200 zimepelekwa zanzibar! Hapo sio Sawa hata kidogo!
Hatuwezi kukubali hata kidogo,huu ni unyonyaji,basi tuwe na serikali 3 ili na watanganyika tuwe na yetu
 
Leta uthibitisho twende sawa
Kaka haya mambo lazima viongozi walio ndani ya system waweze kuwatetea watanzania! Wewe unaomba uthibitisho mimi nakufananisha na mtu kuomba uthibitsho wa bikra kwa mwanamke mja mzito!
 
Hata hii trillion 7 wanayopigia kelele zanzibar itapata trillion 1.3 kwa hiyo yenye faida ni zanzibar ila watanganyika faida ni ndogo ukilinganisha na eneo na idadi ya watu!

Rais kwa kuwa ni Mzanzibar anatumia ho mwanya ila kwa vile watanganyika hatuwezi kuhoji na ukihoji unasakamwa kama Ndugai!

The level of reasoning is very low! Ni mda wa wazanzibar kutumia kivuli ya Watanganyika kujimemesha!

Kwenye ajira pia hakuna uwiano juzi hapa wametangaza ajira bila shaka TRA asilimia 20 wanapewa Wazanzibar! Je hapo **** uwiano Sawa?

Viongozi wetu watanganyika mpo tu kwa vile mnataka madaraka kila kitu ndio mwalimu!
Sawa hata kama unalenga kupotosha ila 1.3t=18% ,,pili kulipa deni kila mtu atalipa.

Swali je hizo pesa zinakopwa kwa faida ya Nchi au kwa faida ya Zanzibar? Je wasipokopa kwani Zanzibar inazuiwa Kukopa?
 
Wawatetee kwenye nini? Mada yako yenyewe haina utafiti wala waku-google..
Kaka haya mambo lazima viongozi walio ndani ya system waweze kuwatetea watanzania! Wewe unaomba uthibitisho mimi nakufananisha na mtu kuomba uthibitsho wa bikra kwa mwanamke mja mzito!
 
Kwa sasa watanganyika ndio tutaomba poo kwa msoto
 
Back
Top Bottom