Rais Samia analazimisha kuizanzibarisha Tanganyika kwa nguvu

Rais Samia analazimisha kuizanzibarisha Tanganyika kwa nguvu

Mkuu hapa hatuongelei suala la ardhi bali tunaongea kuhusu Samia kuvunja katiba ya nchi kwa kuwateua wapemba kushika nafasi za watanganyika. Mfano halisi ni yule mpemba wa NECTA. Ina maana hata huyu mpemba siku anatangaza matokeo hukumuona au unatetea ujinga bila sababu za msingi mkuu?
Mpemba sio mtanzania?. punguzeni haya magubu yanaishia kuwaumiza tu mioyo yenu.
 
Wapo wengi wenye kuuona una faida, sisi tunaolalamika humu JF tuna maoni tofauti na uhalali wa kinachoendelea kwenye maisha halisi,

Alikuwepo kiongozi wa serikali ya Mapinduzi akiitwa Mwakanjuki alikuwa na cheo cha Brigedia na alipigania uhuru wa Zanzibar, kwa sasa ni marehemu, asili yake ni mkoa wa Mbeya.

Abdallah Natepe kiongozi mwingine mwandamizi wa serikali ya Mapinduzi ambaye pia ni marehemu, huyu alianza miaka ile ya kabla ya mapinduzi yenyewe, mwenyeji wa mkoa wa Mtwara huku bara.

Ni vyema kutafuta habari za kina kuliko kudandia hizi harakati za chuki bila hata ya kuijua kwa kina historia.
Hata sasa wanaoona faida ya muungano ni viongozi, na uliowataja hapa kama sehemu ya faida ya muungano ni viongozi na sio wananchi wa kawaida. Sisi wananchi wa kawaida hatuoni faida ya a muungano. Na Leo hii ikiitishwa kura ya maoni ili muungano uwepo ama la, utavunjika ndani ya nusu saa. Msitake kulazimisha muungano wa mtutu wakati watu hawautaki.
 
Washakuwepo akina Januari Fuso, Ernest Mashimba, Omar Mapuri wakutokea Pemba.
 
Nenda huko pemba kama Kuna kiongozi mbara, au uTanzania ni one way traffic?
Acheni chuki, hakuna visiwa vyenye wenyeji wenye asili yake, tazama visiwa vyote duniani kuanzia kule Jamaica mpaka Comoro.

Visiwa huwa na mashombe wengi kwa sababu ni mchanganyiko wa watu wanaokutana mahali hapo, havina mwenyewe hivyo msitake kuja na nongwa zisizo na mpango wowote.

Omari Ramadhan Mapuri alitokea vipi mpaka akawa Mpemba?, au Mashimba amefikaje Pemba?.

Hakuna visiwa vyenye mwenyeji wake kwa asilimia mia moja, havipo.

Bob Marley Baba ni muingereza na mama ni mweusi kutokea Afrika.

Marehemu Fred Mercury alikuwa mzenji, Baba asili yake ni Pakistan na Mama mwarabu.
 
Hata sasa wanaoona faida ya muungano ni viongozi, na uliowataja hapa kama sehemu ya faida ya muungano ni viongozi na sio wananchi wa kawaida. Sisi wananchi wa kawaida hatuoni faida ya a muungano. Na Leo hii ikiitishwa kura ya maoni ili muungano uwepo ama la, utavunjika ndani ya nusu saa. Msitake kulazimisha muungano wa mtutu wakati watu hawautaki.
Muungano ni zaidi ya eneo husika, muungano ni makubaliano ya nafsi za aina nyingi kuwa kitu kimoja.

Akili hizi za chuki bahati nzuri zinaishia humu humu tu hazisambai huko mtaani.
 
Wapo wengi wenye kuuona una faida, sisi tunaolalamika humu JF tuna maoni tofauti na uhalali wa kinachoendelea kwenye maisha halisi,

Alikuwepo kiongozi wa serikali ya Mapinduzi akiitwa Mwakanjuki alikuwa na cheo cha Brigedia na alipigania uhuru wa Zanzibar, kwa sasa ni marehemu, asili yake ni mkoa wa Mbeya.

Abdallah Natepe kiongozi mwingine mwandamizi wa serikali ya Mapinduzi ambaye pia ni marehemu, huyu alianza miaka ile ya kabla ya mapinduzi yenyewe, mwenyeji wa mkoa wa Mtwara huku bara.

Ni vyema kutafuta habari za kina kuliko kudandia hizi harakati za chuki bila hata ya kuijua kwa kina historia.
Haya uliyoyataja hapa yana faida gani kwa watanganyika?
 
Muungano ni zaidi ya eneo husika, muungano ni makubaliano ya nafsi za aina nyingi kuwa kitu kimoja.

Akili hizi za chuki bahati nzuri zinaishia humu humu tu hazisambai huko mtaani.
Unachekesha iweli. Kwa hiyo, watanganyika na wazanzibar waneungana kinafsi? Kivipi mkuu?
 
Acheni chuki, hakuna visiwa vyenye wenyeji wenye asili yake, tazama visiwa vyote duniani kuanzia kule Jamaica mpaka Comoro.

Visiwa huwa na mashombe wengi kwa sababu ni mchanganyiko wa watu wanaokutana mahali hapo, havina mwenyewe hivyo msitake kuja na nongwa zisizo na mpango wowote.

Omari Ramadhan Mapuri alitokea vipi mpaka akawa Mpemba?, au Mashimba amefikaje Pemba?.

Hakuna visiwa vyenye mwenyeji wake kwa asilimia mia moja, havipo.

Bob Marley Baba ni muingereza na mama ni mweusi kutokea Afrika.

Marehemu Fred Mercury alikuwa mzenji, Baba asili yake ni Pakistan na Mama mwarabu.
Maelezo mengi yasiyo na tija yoyote. Leo hii ukienda Zanzibar kama mtu wa bara unaweza kugombea uongozi? Naona porojo nyingi zisizo na kichwa Wala miguu.
 
Tulizoea kuona wazaznzibar (maarufu kwa jina la wapemba) wametapakaa kila mahali hapa Tanganyika wakifanya biashara na shughuli nyingine za kiuchumi. Hili kama watanganyika hatuna shida nalo. Hawa ni wajasiriamali na watafutaji kama walivyo watu wa mataifa mengine waliomo hapa nchini. Tunao wachina, wahindi, wakenya, n.k, na haijawahi kuwa shida.

Kinachoudhi na kusikitisha zaidi ni kitendo cha Rais Dr Samia kuwachukua wazanzibar (hata wasiokuwa na vigezo) na kuwapa vyeo hapa Tanganyika wakati watanganyika hawana kazi. Ukitembelea kwenye ofisi za umma utashangaa kuona utitiri wa wazanzibar wakiwa wamepewa nyadhfa mbali kama vile wakurugenzi, DAS, RAS, wakuu wa mashirika ya umma, wenyeviti wa bodi mbalimbali, n.k. Rais anafanya haya yote kwa makusudi na kwa lazima huku akiwaacha watanganyika wakipuyanga bila kazi. Huu ni zaidi ya uhujumu uchumi.

Ndugu wanaJF na wananchi kwa ujumla, tuhuma hizi hazijaanza leo. Soma baadhi ya nyuzi zilizowahi kuwekwa humu kulalamikia upendeleo unaofanywa na mamlaka kwenye teuzi mbalimbali:

1. Teuzi za Rais Samia zina upendeleo?

2. Teuzi za Rais Samia kulikoni?

3. Wafahamu Wajumbe wa Bodi ya TCRA iliyovunjwa

Kelele za watanganyika kukosa kazi baada ya kuhitimu zipo dhahiri. Hata humu JF siku za karibuni kumekuwa na nyuzi nyingi zinazoonyesha wasomi wa Tanganyika kuhitimu vyuo vikuu na kuishia kufanya kazi za ovyo ovyo wakati kazi walizostahili kufanya zinagawiwa ovyo kwa wazanzibar. Nyuzi zifuatazo ni sehemu ya ushahidi huo:

1. Nimekutana na Degree Graduate wa HR kutoka Mzumbe anauza Pub

2. Mzazi unasomesha mtoto aje kuuza chips na kuwa bodaboda. Inahuzunisha sana!

3. Graduates wengi tunapitia wakati mgumu sana, sema jamii inaona kama hatujielewi

MAONI YANGU
Idadi ya watu wa Zanzibar (Pemba, Unguja na visiwa vingine) haipindukii milioni moja. Tanganyika ina idadi ya zaidi ya watu milioni 64. Sasa iweje Zanzibar yenye watu wachache kiasi hiki wananchi wake wapewe kipaumbele huku watanganyika walio wengi wanaendelea kusaga meno?

Ifike mahali katiba itamke bayana idadi ya nafasi wanazostahili wazanzibar (kwa kufuata uwiano wa idadi ya watu) badala ya kufanya teuzi kibubu na kusababisha malalamiko. Na tunapendekeza hili jambo liingizwe kwenye katiba mpya kabisa ili kukata mzizi wa fitna.

Nawasilisha.
Ndio maana hua nashikwa na hasira nikiona hawa chawa wakipigia chapuo huyo mama kugombea 2025. Namuomba tu mwenyewe wala asijaribu maana atakigawa chama cha ccm. Wananchi wengi hawatamchagua.
 
Unachekesha iweli. Kwa hiyo, watanganyika na wazanzibar waneungana kinafsi? Kivipi mkuu?
Karume asili yake ni huku bara. Mwinyi ni mzaramo wa Kisarawe. Wanasiasa wengi tu wana DNA za huku bara.

Sisi ni wamoja na hatuna sababu ya kutazamana kama vile tunapotoka kwenye matumbo ya mama zetu tunakuwa tukiwa na hati miliki ya Zanzibar na Tanganyika.

Ndio maana mwanzoni kule juu nimehoji juu ya umri wa sisi tunaojadili hii mada.
 
Uasili wa viongozi ni kigezo cha Rais Samia kusigina katiba kwa kutujazia viongozi wapemba hapa Tanganyika kinyume cha katiba?
 
Nenda huko pemba kama Kuna kiongozi mbara, au uTanzania ni one way traffic?
Unguja na Pemba ukizichanganya kwa pamoja zina idadi ya watu wasiozidi milioni mbili, Kinondoni peke yake ina watu milioni mbili, kwanini huyo kiongozi kutoka bara aende huko Pemba eti akagombee nafasi ya uongozi?.

Muungano unalo somo la upendo alilotuachia Mwalimu Nyerere na Hayati Mzee Karume.
 
Uasili wa viongozi ni kigezo cha Rais Samia kusigina katiba kwa kutujazia viongozi wapemba hapa Tanganyika kinyume cha katiba?
Pemba sio sehemu ya JMT?, Mbona marehemu JPM alitujazia wanyantuzu kina Mpina na wasukuma wenzake kina Makonda na hatukusema chochote?, akili zinazoelekea kufilisika ni zile zinazojikita kwenye kutazama mtu katoka wapi bila kutazama uwezo wake upo vipi na unaweza vipi kuleta mchango mpya kwenye sekta husika.
 
Sasa mbona unajipinga mwenyewe mkuu? Zanzibar yenye watu wasiopindukia milioni 1 kwanini iwe na viongozi wapemba na waunguja wamejazana huku Tanganyika kama panzi wakati vijana wa Tanganyika hawana ajira? Wewe unaona sawa au unatetea tu kichawa bila kutafakari?
 
Mbona huwezi kumkuta mmatumbi akiwa ameshika madaraka Zanzibar? Au mkuki kwa nguruwe? Kunya anye kuku tu, akinya bata kaharisha!
Brigadier Mwakanjuki RIP Mnyakyusa.

Abdallah Natepe RIP Mmakonde.

Omar Mapuri Mmakonde.

Tito Okello RIP Mjaluo wa Uganda.

Hao ni wamatumbi wanne kutoka huku bara ambao historia yao inaheshimika huko ZNZ, vijana wadogo humu JF jifunzeni kwanza historia yenu kabla hamjaandika chochote.
 
Sasa mbona unajipinga mwenyewe mkuu? Zanzibar yenye watu wasiopindukia milioni 1 kwanini iwe na viongozi wapemba na waunguja wamejazana huku Tanganyika kama panzi wakati vijana wa Tanganyika hawana ajira? Wewe unaona sawa au unatetea tu kichawa bila kutafakari?
Vijana wa Tanganyika waende shule wapambanie kesho yao, yaani vijana wa kizenji wasiendelee kisa kuna vijana wa kibara wanaofuga ulofa wao wenyewe? aah come on.

Wapemba walianzisha lile eneo la biashara pale Namanga Kinondoni, vijana wetu wa huku bara walikuwa wapi miaka hiyo?.

Tuachane na huu upumbavu wa kutazamana huyu anatoka sehemu gani na huyu anatoka sehemu gani, ni ishara mbaya ya ubaguzi ambao unagawa Taifa.
 
Back
Top Bottom