Wapo wengi wenye kuuona una faida, sisi tunaolalamika humu JF tuna maoni tofauti na uhalali wa kinachoendelea kwenye maisha halisi,
Alikuwepo kiongozi wa serikali ya Mapinduzi akiitwa Mwakanjuki alikuwa na cheo cha Brigedia na alipigania uhuru wa Zanzibar, kwa sasa ni marehemu, asili yake ni mkoa wa Mbeya.
Abdallah Natepe kiongozi mwingine mwandamizi wa serikali ya Mapinduzi ambaye pia ni marehemu, huyu alianza miaka ile ya kabla ya mapinduzi yenyewe, mwenyeji wa mkoa wa Mtwara huku bara.
Ni vyema kutafuta habari za kina kuliko kudandia hizi harakati za chuki bila hata ya kuijua kwa kina historia.